Elections 2010 Ripoti ya waangalizi wa uchaguzi inaleta kichefuchefu...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
SOURCE: ITV leo taarifa yahabari ya saa mbili usiku..........

Yaani nilichoona kimenishtua sana..........................waangalizi hawa hivi walikuwa nchi gani vile?

Wamedai yafuatayo:-

a) Wapigakura wengi hawakupiga kura kisa waliona CCM itashinda tu na hivyo kusababisha kura zilizohesabiwa kuwa kiduchu..........................ukweli ni kuwa TISS na NEC waliminya kura kibao..............................................

b) Walidai ya kuwa CCM bado ni chama imara wakati Chadema iliwaangusha ila kazi chafu ya TISS na NEC ndiyo inakiweka CCM madarakani......................

c) Hawakuongelea mahudhurio makubwa kwenye mikutano ya Dr. Slaa na kama hao wote yaani waliohudhuria walibaki majumbani hawakupiga kura......................................I just cannot take this boloney........................

d) mapoungufu ya NEC na TISS yamefumbiwa macho.........................................

la ajabu kuliko yote eti JK mchakachuaji in-chief ndie anayepewa hiyo taarifa.......................................kweli nimeamini hawa waangalizi na CCM lao ni moja kuhalalisha viongozi tusiyo wahitaji...........................hawa ndiyo walimhalalisha Hosni Mubarak ambaye leo kila mmoja amejua kumbe hachaguliki kabisa.,..........ni wizi wa kura tu ndiyo umemweka madarakani miaka 30..............
 
ha ha ha ha ha ha haaaa, chama kimoja almanusra kiwangize Watz mkenge , kiukweli bado kinahitaji miaka kama 10 hivi kukomaa.
 
Nasikia Bw. John Martini aliyeongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi mkuu uliopita kutoka EEC amekabidhi taarifa yake kwa JK. Kuna tetesi kwamba mambo nyeti katika taarifa hiyo yatabakia siri.
 
Huu sasa ndo umbumbumbu kama nimeelewa vizuri yaani eec wanaleta taarifa hafu wanampa Ki'wete badala ya kutusomea?
 
Haina maana yeyote nashindwa kuelewa muda wote huo toka mwezi Wa kumi mpaka sasa wanatuambia huu upuuzi Wa CCM...inasikitisha sana
 
Kama ripoti inapelekwa ikulu basi ni zawadi kwa rais. Isingepokelewa kama ingeandikwa "mh.rais umechakachua kura"haijawai kutokea iyo! Nakumbuka taasisi iyo ilitoa Interim Report katikati ya kampeni na ilikuwa inaonesha ukweli kwa Tzbara,je leo kipande icho kimemeza na nini? Hawa watu wanaitaka nyuklia yetu kwa nguvu. Toka nimesikia leo ktk habari,kamwe sitachangia wala kufikiri kuwa hawa watu walifanya uangalizi ktk URT. Nawaunganisha na REDET.
 
kwa nini wachafue hali ya hewa wakati watanzania tulisha kubali kwa hiari kutawaliwa na kikwete? Kungekuwa na maandamaano ya kupinga ushindi wake kwa nguvu zote nadhani riport ingekuwa tofauti.
 
wanasema eti uchaguzi ulikua huru na haki..............ya kweeeli hayo jamani?mbona sehemu zilizooonyesha kuwa na wapinzani wakurugenzi wa wilaya walikua wakipigiwa simu kulazimishwa kuwatangaza wagombea wa CCM kua ndo washindi?
 
David Martin yeye ni muandishi wa habari aliyebobea; kilichomkataza kuitisha mkutano wa wahandishi wa habari ili angalau awaelezea hayo waliyo yashuhudia ni nini- kama hana la kuficha
 
Nasikia Bw. John Martini aliyeongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi mkuu uliopita kutoka EEC amekabidhi taarifa yake kwa JK. Kuna tetesi kwamba mambo nyeti katika taarifa hiyo yatabakia siri.

Hiyo ni taarifa ya JK, tunaomba taarifa yetu sasa!
 
Hao ni NEC nyingine ila tofauti yao ni ngozi nyeupe.

hiyo ni nec ya kukwapua rasilimali zetu.

hawana cha kupoteza wakisifia dhulma, mradi tu wapate madini yao

hata watanzanua wakifa jwa njaa is ni=an of their bizness
 
Yaani kweli nilishangaa sana nilipoona picha kwenye blog ya michuzi, Kikwete akikabidhiwa riport na mtu wa EEC! Nikajiuliza inakuwaje aliyekuwa mgombea wa uchaguzi anakabidhiwa hiyo ripoti! Ina maana kwamba hiyo ripoti iko in favour of Kiwete na chama chake! Hawa EEC wanajipendekeza kwa serikali ya TZ kwa ajili ya maslahi yao binafsi......:A S thumbs_down:
 
Huu sasa ndo umbumbumbu kama nimeelewa vizuri yaani eec wanaleta taarifa hafu wanampa Ki'wete badala ya kutusomea?

Duniani amini watu wote lakini sio hawa weupe, ni wapuuzi kuliko hata weusi!!!!
 
Hawa wanajua kuendelea kumsifia kikwete kutawafanya waendelee kuchuma shamba la bibi kwa raha yao. Mimi napenda sana Misri walivyowatwanga waandishi wa habari kutoka magharibi wanasema wanapotosha jamii kwa habari zao za kupamba pamba sasa hawa nadhani bongo na iwe hivyo. Wameshatuona sisi mbumbumbu ndio maana. Siku ya siku itafika kikwete utaueleza umma kwa mdomo wako wala si kwa kulazimishwa utawaambia watanganyika ukweli. Ninaisubiri hiyo siku kwa hamu kupita maelezo
 
PHP:
Hiyo ni taarifa ya JK, tunaomba taarifa yetu sasa!

I am impressed by this commentary.......................................
 
PHP:
Hawa wanajua kuendelea kumsifia kikwete kutawafanya waendelee kuchuma shamba la bibi kwa raha yao. Mimi napenda sana Misri walivyowatwanga waandishi wa habari kutoka magharibi wanasema wanapotosha jamii kwa habari zao za kupamba pamba sasa hawa nadhani bongo na iwe hivyo. Wameshatuona sisi mbumbumbu ndio maana. Siku ya siku itafika kikwete utaueleza umma kwa mdomo wako wala si kwa kulazimishwa utawaambia watanganyika ukweli. Ninaisubiri hiyo siku kwa hamu kupita maelezo

Ungemwona JK alivyokuwa akikenua wakati anapokea hiyo taarifa bomu.........................ungelijua hata yeye anaelewa kazi ya kuchakachua haitazaa matunda yoyote yale..................................
 
Sioni sababu ya kulalamika kwamba Report hiyo alikabdihiwa nani... kinachopaswa kujadiliwa ni ukweli na usahihi wa kile walichokishuhudia...kama kweli CCM ni chama imara... KAMA kweli TISS NA NEC hawakuhusika kwa namna mmoja ya uchakachuaji na kama kweli tofauti ya watu Millioni 12 wote walisema eti hawaendi kupiga kura kwa sababu CCM itashinda yaonesha kwamba hata hao waandaji wa report hiyo ni mbumbumbu wa mambo ya Tanzania... labda wangesema tu kwamba daftari lilichakachuriwa with the benefit of hindsite, au watanzania waligoma kupiga kura mpaka wangehakikishiwa kwamba wizi ambao mara nyingi hufanywa na CCM umepatiwa Dawa.... kwan nini wakapigie kura wakati wanajua kwamba hata wakipiga CCM NI WEZI tu wataziiba...
 
Back
Top Bottom