Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mzee Mizengo Pinda kumekuwa na vilio katika halmashauri za wilaya kuhusian na ufusadi wala sijawahi kumsikia akisema kitu. hata zile halimashauri zilizokuwa zimepewa vyeti vichafu na makaguzi wa mahesabu wa serikali nyie mlimsikia Mizengo akisema kitu!

Ili Nchi inyoke sasa inahitaji mtu atakayesoma maoni ya wananchi, anayewapenda wapinzani na kuwapa nafasi sawa ya kuongoza nchi.

Vipi huyu POMBE?
 
Mkuu Mwanakijiji,

Ulikuwa umelala nini? Majemadari wengine hawakulala leo na tayari wameshatuwekea music wetu na tunacheza kwa styles zote zote kuanzia ndomboro mpaka music wa kizazi kipya.
 
..moderator unaweza kuiweka ripoti ya Richmond hapa jamboforums?

naona huko KHL kuna mzengwe wa kujisajili.
 
Hata sura they show no remorse yaani wamekomaa na sura mbaya sana za baadhi hapa . Mtahukumiwa na laana na mateso ya Watanzania viwe juu yenu.

My prediction is that . Next MP is Dr.Mwakyembe ama la atachukua uwaziri wa wizara nyeti .

Lunyungu,

You know better CCM inavyotawala; tangu lini wachapa kazi hodari Tanzania wakazawadiwa madaraka zaidi. Wale waharibifu ndio hupewa zawadi hizo nono za vyeo.
 
Lunyungu,

Mbona Spika alitangaza kikao kuanza saa mbili usiku na sasa hata saa moja haijafika?
 
Tunahitaji ushahidi zaidi kama kweli unayosema yametendeka, tunasubiri ukurasa mpya wa historia ya walalahoi wa Tanzania!!!!


Mama Mdogo endelea kuwa Mama mdogo mimi sina muda kulumbana na kukuthibitishia ila ukweli ni huo kwamba Malecela ndiyo anaongoza kiikao sasa hivi .Kama mimi sijaingia ama nimeingia wewe jali nalo kueleza hii ni JF kama ni uongo watasema hapa watu kwa uwazi.Narudia Malecela ndiye Mwenyekiti wa kikao cha cha Kamati ya uongozi wa Siasa as we speak .
 
NEXT PM?????? awe:JOHN POMBE MAGUFULI, mwasemaje wana JF?

Naam!!!!!!!!!!!!!!!Big up

kashfa zote za Pombe zimetengenezwa na hawa akina PM na kumu subject angle mbaya mbaya ili wa hakikishe wanafanikisha maudhui yao.

Pombe ni NONSENSE MAN anafaa kua PM
 
NEXT PM, if any, MKRISTO MWANAUME, it is stupi to think this way but that is the way it is.
 
Nani kawaambia mtoe mapendekezo yenu hapa kuhusu the Next PM? Itakuwa ni uvivu wa kufikiri kama mtu yoyote anadhani huo uteuzi (if at all upo??) utazingatia maoni yanayotolewa hapa.
 
Mama Mdogo endelea kuwa Mama mdogo mimi sina muda kulumbana na kukuthibitishia ila ukweli ni huo kwamba Malecela ndiyo anaongoza kiikao sasa hivi .Kama mimi sijaingia ama nimeingia wewe jali nalo kueleza hii ni JF kama ni uongo watasema hapa watu kwa uwazi.Narudia Malecela ndiye Mwenyekiti wa kikao cha cha Kamati ya uongozi wa Siasa as we speak .

Lunyungu tunakupata vizuri mwaga tu, ambaye hataki kuamini asubiri kusoma kwenye gazeti la uhuru wiki ijayo, au kusikiliza Radio Tanzania mungu akipenda.
 
Baada ya kupitia thread mbalimbali ndani ya JF na kurejea makabrasha yangu LUNYUNGU nakuamini kabisa kuwa ujumbe ulioleta ni kweli; Mzee Mzima toka Mvumi ndiye asimamia mambo. Twaamini busara zitatumika kwa kuzingatia ukweli uliofukuliwa na kufunuliwa!!!
 
Mtanzania.. sijaona ripoti kamili nimeona summary yaani kile kilichozungumzwa Bungeni, labda nilikuwa nimelala kweli LOL Ila ripoti yenyewe ina kurasa zaidi ya hizo za summary..
 
Kikao kinachofanyika sassa ni cha kamati ya uongozi ya CCM na hii inaundwa na wajumbe wote wa kamati kuu ya CCM waliopo bungeni.

Hii ni kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM na ipo kwenye kanu ni za bunge kwani hata wapinzani wana ya kwao.

Ni kweli kuwa Lowassa haongozi kikao husika ila wamemchagua mzee Malecela kuongoza kikao hicho , na kinaendelea kwenye ukumbi wa pius msekwa na bado kipo.

Rais hayupo kwenye hicho kikao ila yeye atakuwa kikao na wabunge wote wa CCM kilichotangazwa kuwa kitafanyika kuanzia saa mbili za usiku, .

kazi zinaendelea muda huu ni kuwa kila mmoja anajitahidi kujipanga kwa ajili ya kuangalia ama atatoka vipi au amwangamize vipi mwenzake.

JK kaja kutangaza kuwa na waziri mkuu mpya? hilo ndio swqali huku dodoma muda huu.
 
ripoti kali mno.

imoto inaunguza pande zote

mie liloniumiza ni jinsi gani watanzania tunavyokuwa wapenda majungu na wapenda domo nje ila tukiitwa tuthibitshe ukweli tunaanza kuuma uuma vidole.

ni aibu kutojiamini na kutokuwa jasiri wa kusema ukweli.

hii imeanza kunipa wasi wasi mkuu kuwa watanzania ni watu dhaifu na ni watu ambao tutachelewa sana kuendelea.

kumbe yanayosemwa amani yetu ni ya woga ni maneno ya kweli.

nnaamini kuna ukweli mwingi haujawekwa wazi kwa hofu.

nnaamini kuna mengi yatakuja juu mwaka huu.

hongera wenye kuitakia mema nchi yetu bila ya kujali itikadi zao iwe kisiasa au kidini cha msingi upuuzi wa kuinyonya tanzania na kuwakandamiza watanzania ukomeshwe

VEMA,KUMBE MAJI YAKIZIDI UNGA HUWA UNATOA MAPWENTI
 
Asante mzee mwanakijiji,uliyotuletea ni ripoti kamili wengine walitupa summary ya kilichosomwa leo bungeni hivyo upo sahihi tu na watu wanapaswa kuelewa hivyo,manaake ya kwako ina hata table of contents na footnotes.
 
Huku ni kuwa bado kikao kinaendelea cha kamati ya uongozi ya CCM na kimemteua mzee Malecela kuongoza kikao hicho.

Kinafanyikia ukumbi wa Pius msekwa na hicho ni kikao kwa ajili ya kujiandaa na kikao cha saa mbili usiku ambcho kitawahusisha wabunge wote wa CCM na hicho JK anategemewa kuwepo kwani tayari kashafika Dodoma na anaendelea kujipanga.

Kwa hapa wabunge wengi hawaonekani kwani inasemekana kuwa wanaisoma ripoti husika na wanaendelea nayo.

Nitawatumia taarifa nyingine hapo baadae kidogo kwani hali huku ni ya wasiwasi sana .
 
Niwafahamishe wale ambao hawajui kuwqa nini maana ya kikao cha kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM ni kuwa kikao hiki kinahusisha wajumbe wote wa kamati kuu ya CCM waliopo bungeni na mwenyekiti wao ni waziri mkuu.
 
Asante Mwanakijiji, hii CD uliyotuma ina miziki mingi zaidi ya ile iliyotumwa mapema. Wacha niendelee kucheza.

Mukiweza unganisheni hii na ile ya Mnyika ili kuweka mtiririko msafi.

Leo JF imevunja record yake kwa kuwa na wasomaji wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote.
 
Back
Top Bottom