Ripoti: Tanzania yaongoza kwa wanywa pombe

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,831
1,164
Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanywa pombe za viwandani barani Afrika, ripoti imesema. Idadi ya walevi wa bia imeongezeka kwa asilimia 35 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wakati ile ya watumiaji wa pombe kali imepanda kwa kiwango cha asilimia 25. Nchi zinazoifuatia Tanzania ni Zambia, Afrika Kusini, Malawi na Nigeria.
 
Kwa mwendo huu wa kitimoto na pombe ni lazima tuongoze..!
 
Kunywa pombe kwangu mie sio kashfa,ingekuwa Tanzania imeongoza kwa walevi hapo ningefedheheka sana!
 
Weka hiyo ripoti hapa. Tofautisha kati ya wanywaji na walevi, je Watanzania ni wanywaji au walevi kama ni wanywaji, haina shida. Ila kama ni walevi......Hiyo ni Noma.
 
Tanzania imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanywa pombe za viwandani barani Afrika, ripoti imesema. Idadi ya walevi wa bia imeongezeka kwa asilimia 35 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wakati ile ya watumiaji wa pombe kali imepanda kwa kiwango cha asilimia 25. Nchi zinazoifuatia Tanzania ni Zambia, Afrika Kusini, Malawi na Nigeria.

Harro Mwita hebu tufafanurie hapo kwenye rirangi jekundu, ni idadi ya wanywa bia au warevi wa bia? Harafu hiyo idadi ya wanywa bia kali ina include ire chang'aa ya kure nyumbani? harafu kwa kushika nafasi ya kwanza TZ imepata rikikombe au rimedali?
 
Ukipita salendar hapo kuna bonge la bango la beer ya ndovu basi wasituwekee hata mabango bac c
 
na kama hujui according to TBL wilaya ya kinondoni ndo inaongoza ikifuatiwa na wilaya ya geita mwanza
 
Huo utafiti unalenga kumnufaisha nani? achana nao hao, South africa ndiyo walevi ,bongo mnazijua pombe ama mnalamba tu!!!! labda walikuwa wanataka kuwahamasisha kutokana na kutouzika kwa bia kwenye soko la ndani
 
nakunywa pombe and i am nit ashamed, ila nikiwa mlevi ntaskia aibu

pamoja na hayo hii ni dalili ya frustrated society...
 
Huo utafiti unalenga kumnufaisha nani? achana nao hao, South africa ndiyo walevi ,bongo mnazijua pombe ama mnalamba tu!!!! labda walikuwa wanataka kuwahamasisha kutokana na kutouzika kwa bia kwenye soko la ndani
mkuu

amezungumzia za viwandani, sauzi wanapiga mataptap, kama kkenya na malawi na zimbabwe
 
Back
Top Bottom