RIPOTI MAALUMU:Upasuaji tishio kwa wajawazito-2

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,356
33,195
Na Florence Majani
WAKATI idadi ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji ikiongezeka, imebainika kuwa njia hiyo ina madhara makubwa ikiwamo kupata matatizo ya mgongo.

Mkunga na Mhadhiri wa Ukunga wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Sebalda Leshabari ameliambia Mwananchi Jumapili kuwa upasuaji si jambo zuri kwa wajawazito.
“Upasuaji si jambo zuri kabisa katika muktadha wa uzazi na ndiyo maana watu huita ni kujifungua kusiko kwa kawaida,” alisema.

Alitaja madhara yanayowapata wajawazito wengi baada ya kujifungua kwa upasuaji kuwa ni pamoja na maziwa kutotoka kwa siku kadhaa baada ya kujifungua.
“Maziwa yasipotoka ina maana mtoto anakosa yale maziwa ya kwanza ya mama ambayo huwa na virutubisho vyote,” alisema.

Aliongeza kuwa wajawazito wengi wanaofanyiwa upasuaji hulalamika kupata maumivu ya kichwa kwa muda mrefu pamoja na maumivu ya uti wa mgongo. Kuhusu wajawazito wanaochagua kujifungua bila sababu maalumu, Dk Leshabari alisema wengi wao wanasikiliza dhana potofu.

“Hakuna ukweli kuwa kuzaa kwa njia ya kawaida kunaharibu sehemu zao za siri. Mbali na hilo, tunawafundisha aina ya mazoezi ambayo hurudisha sehemu zao kuwa nzuri zaidi,” alifafanua Dk Leshabari.

Alisema, yapo mazoezi ya kubana misuli ya sehemu za siri ambayo mama aliyejifungua hufunzwa ili kuzirudisha kama zilivyokuwa awali na mazoezi hayo ni endelevu kwa mwanamke. Alisema wakunga wanatakiwa watimize wajibu wao, kwani wajawazito wanasikiliza uvumi wa mtaani kuwa njia hiyo inaleta madhara.

“Ni lazima mkunga amfundishe mwanamke mambo ya kufanya wakati wa ujauzito, atayarishe nini na aende wapi kujifungua,” alisema.
Wanawake watano waliohudhuria kliniki katika hospitali moja binafsi jijini Dar es Salaam, waliohojiwa na Mwananchi Jumapili walisema hawakupewa elimu yoyote ya jinsi ya kutunza ujauzito ili kuwaepusha kufanyiwa upasuaji.

Wanawake watano waliohudhuria kliniki ya ujauzito katika hospitali za umma, wote walikubali kupata elimu hiyo kwa kina, ikiwamo jinsi ya kumshika mtoto hata na kunyonyesha.
Mkunga Mkuu wa Hospitali ya Mwanyamala, Agnes Mgaya alisema timu yake inajaribu kuepuka upasuaji kwa asilimia kubwa.

“Inapotokea tunafanya upasuaji basi ujue kila jitihada zimeshindikana, kwa sababu upasuaji si jambo zuri,” alisema Mgaya.

Alitaja athari za upasuaji na kusema kwanza ni gharama kwa Serikali na hospitali yenyewe. “Tunatumia vifaa vingi kwa mjamzito wakati wa upasuaji wakati fedha hizo zingewekezwa katika maeneo mengine lakini pia tunatumia nguvu nyingi,” alisema.

Alisema mwanamke anayefanyiwa upasuaji hutakiwa kutofanya kazi ngumu kwa miezi sita, wakati mama aliyejifungua kwa kawaida, atafanya kazi zake baada ya muda mfupi.

“Mwanamke aliyefanyiwa upasuaji hushindwa kupanga uzazi kwa wakati mwafaka na wengine huuguza kidonda kwa muda mrefu,” alisema.

Mkunga huyu wa muda mrefu alisema, upasuaji si jambo zuri, lakini limekuwa likiongezeka kwa sababu ya ongezeko la matatizo ya uzazi. Madhara mengine
Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuchanika kwa kizazi kwa mama anayejifungua kwa njia ya upasuaji, wakati wa kujifungua kwa mara ya pili.
“Upasuaji unasababisha hatari katika kondo la uzazi wakati wa ujauzito unaofuatia,” inasema taarifa hiyo.

Lakini pia, upasuaji unasababisha familia ndogo. Kwa sababu mama hupangiwa asizae zaidi ya watoto watatu.

Taarifa hizo zinaongeza kuwa, watoto wanaozaliwa kwa njia ya upasuaji wengi wao hupata matatizo ya mfumo wa upumuaji.
Prisca Petro mkazi wa Dar es Salaam, alisema aliuguza kidonda kwa zaidi ya mwaka baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kauli ya mkunga
Mkunga Mstaafu, Angelina Mitande (73) aliyewahi kufanya kazi ya ukunga katika Hospitali za Muhimbili na mkoani Singida, ambaye kwa sasa anatoa huduma na ushauri kwa wajawazito katika Kijiji cha Chikunja, wilayani Masasi anasema, mjamzito anatakiwa apewe mafunzo ya kina mara tu anapogundulika kuwa na ujauzito.

“Zamani tuliwakataza wajawazito kula mayai, kwa lengo kuepusha mtoto asiwe mnene hali ambayo mara nyingi husababisha upasuaji wakati mama anajifungua, ” anasema Mitande.

Alibainisha kuwa jambo lingine analotakiwa kufanyiwa mjamzito ni kusingwa (massage) mara kwa mara tumboni kwa mafuta ya nazi au karafuu ili kumuweka mtoto katika mkao mzuri.

“Hakuna zoezi muhimu kwa mjamzito kama kukandwa tumbo. Hili ndilo hukifanya kiumbe kilichoko tumboni kigeuke chenyewe, katika mikao mbalimbali na kichangamke,” alisema.

Mitande anaonya kuwa mazoezi ni muhimu kwa wajawazito na anawataka kufanya kazi zote za nyumbani, kuwa wasafi na kula vyakula vyenye virutubisho.

“Wasichana wa sasa wanadeka sana na hudhani kuwa wakiwa wajawazito hawahitaji ushauri wa kijadi, wasidhani wataweza kuutua huo mtihani wa kujifungua bila elimu,” anasema
Mitande na kuongeza:

“Maji ya moto kwa mama aliyejifungua ni muhimu kwa sababu yanasaidia kutoa uchafu uliobaki tumboni mwa mama baada ya kujifungua na pia hupunguza maumivu na kuponya mapema majeraha yaliyopatikana wakati wa kujifungua.”

http://www.mwananchi.co.tz/mwananch...ipoti-maalumuupasuaji-tishio-kwa-wajawazito-2
 
Asante kwa elimu. Nimejifunza sana. Nimeshangazwa na wanawake kuchagua kupasuliwa kisa kulinda maumbile, hii mbaya sana, kisa kuogopa kuachwa, bila kuangalia upande wa pili kuwa operesheni inamfanya mtu asifanye kazi kwa muda mrefu nalo laweza kumfanya mama ashindwe kutimiza wajibu wake kwa baba na watoto mwisho wa siku kuachwa vilevile. Mungu atuepushe na hili.
 
Hili la kuchagua sidhani kama liko sana hapa kwetu; naowajua walofanyiwa operation; nikiwa mmoja wapo na marafiki zangu, ni madaktari walioshauri iwe hivyo kumuokoa mama na mtoto. Ni rare cases kukuta dada wa ki Tz anaomba apigwe kisu; na wengi wanaoomba hivyo nimeshasikia ni waathirika ili wasiambukize watoto kwa michubuko wakati wa kuzaa.

Na nataka nipinge kuwa operation ni mbaya kihivyo when necessary kwani hao the so called wakunga wangekuwa wazi watupe idadi ya waliowazalisha na ni wangapi walizaa salama na watoto wakawa hai. Hivi tunavyoongelea vifo vy wamama wajawazito na watoto tunaongelea wamama gani kama si hao wanaozalishwa na wakunga.

Haya mambo hayatabiliki. Mi si mvivu wala nini; mwanangu wa kwanza nilimzaa salama na kg 3.9; wa pili nilimzaa kwa kisu akiwa na kg 4.1 na si kwa kuwa njia ilikuwa ndogo ila ni kwa kuwa haligoma kushuka.

Hata kama aliyeongea ni doctor bado hii habari ni ya ki journalist zaidi kwani haija base kwenye scientific research.

Na suala la kuhusu elimu wanayotoa manesi kwa wazazi na watoto ambayo haitolewi kwenye private hospital naweza sema there is no need ndo maana hizi hospital binafsi hawaoni sababu ya kupoteza muda wao.
Nasema hivi kwa sababu kwanza huwezi kuta mtoto wa mwanamke mwenye elimu yake ana utapia mlo. Tuna google information za diet ya watoto wetu. Na wateja wengi wa private hospital ni watu walo elimika (middle na upper class)

Pili hatuna muda wa kusikiliza lecture za manesi wakati tumetoroka kazini kuleta watoto clinic; akipata chanjo akapima nataka niwhai ofisini.

Kwanza manesi wengine wanasemaga uongo kibao; hivyo akili zao changanya na zako. Mfano kuna siku nilimpeleka mtoto clinic regency nesi mmoja akajidai kunifokea wewe mbona mtoto hujamfunika; wakati kuna joto zaidi ya 30; ukifuata ushauri kama huu mtoto anaweza pata vipele au hata magonjwa yanayoletwa na unyevu nyevu wa jasho. Manesi wengi wanaamini watoto wanatakiwa wavalishwe nguo kadhaa regardless ya weather, wakati wanangu wanashindia 'carwash' na hawaugui. Lol.

Na Florence Majani
WAKATI idadi ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji ikiongezeka, imebainika kuwa njia hiyo ina madhara makubwa ikiwamo kupata matatizo ya mgongo.

Mkunga na Mhadhiri wa Ukunga wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Sebalda Leshabari ameliambia Mwananchi Jumapili kuwa upasuaji si jambo zuri kwa wajawazito.
"Upasuaji si jambo zuri kabisa katika muktadha wa uzazi na ndiyo maana watu huita ni kujifungua kusiko kwa kawaida," alisema.

Alitaja madhara yanayowapata wajawazito wengi baada ya kujifungua kwa upasuaji kuwa ni pamoja na maziwa kutotoka kwa siku kadhaa baada ya kujifungua.
"Maziwa yasipotoka ina maana mtoto anakosa yale maziwa ya kwanza ya mama ambayo huwa na virutubisho vyote," alisema.

Aliongeza kuwa wajawazito wengi wanaofanyiwa upasuaji hulalamika kupata maumivu ya kichwa kwa muda mrefu pamoja na maumivu ya uti wa mgongo. Kuhusu wajawazito wanaochagua kujifungua bila sababu maalumu, Dk Leshabari alisema wengi wao wanasikiliza dhana potofu.

"Hakuna ukweli kuwa kuzaa kwa njia ya kawaida kunaharibu sehemu zao za siri. Mbali na hilo, tunawafundisha aina ya mazoezi ambayo hurudisha sehemu zao kuwa nzuri zaidi," alifafanua Dk Leshabari.

Alisema, yapo mazoezi ya kubana misuli ya sehemu za siri ambayo mama aliyejifungua hufunzwa ili kuzirudisha kama zilivyokuwa awali na mazoezi hayo ni endelevu kwa mwanamke. Alisema wakunga wanatakiwa watimize wajibu wao, kwani wajawazito wanasikiliza uvumi wa mtaani kuwa njia hiyo inaleta madhara.

"Ni lazima mkunga amfundishe mwanamke mambo ya kufanya wakati wa ujauzito, atayarishe nini na aende wapi kujifungua," alisema.
Wanawake watano waliohudhuria kliniki katika hospitali moja binafsi jijini Dar es Salaam, waliohojiwa na Mwananchi Jumapili walisema hawakupewa elimu yoyote ya jinsi ya kutunza ujauzito ili kuwaepusha kufanyiwa upasuaji.

Wanawake watano waliohudhuria kliniki ya ujauzito katika hospitali za umma, wote walikubali kupata elimu hiyo kwa kina, ikiwamo jinsi ya kumshika mtoto hata na kunyonyesha.
Mkunga Mkuu wa Hospitali ya Mwanyamala, Agnes Mgaya alisema timu yake inajaribu kuepuka upasuaji kwa asilimia kubwa.

"Inapotokea tunafanya upasuaji basi ujue kila jitihada zimeshindikana, kwa sababu upasuaji si jambo zuri," alisema Mgaya.

Alitaja athari za upasuaji na kusema kwanza ni gharama kwa Serikali na hospitali yenyewe. "Tunatumia vifaa vingi kwa mjamzito wakati wa upasuaji wakati fedha hizo zingewekezwa katika maeneo mengine lakini pia tunatumia nguvu nyingi," alisema.

Alisema mwanamke anayefanyiwa upasuaji hutakiwa kutofanya kazi ngumu kwa miezi sita, wakati mama aliyejifungua kwa kawaida, atafanya kazi zake baada ya muda mfupi.

"Mwanamke aliyefanyiwa upasuaji hushindwa kupanga uzazi kwa wakati mwafaka na wengine huuguza kidonda kwa muda mrefu," alisema.

Mkunga huyu wa muda mrefu alisema, upasuaji si jambo zuri, lakini limekuwa likiongezeka kwa sababu ya ongezeko la matatizo ya uzazi. Madhara mengine
Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuchanika kwa kizazi kwa mama anayejifungua kwa njia ya upasuaji, wakati wa kujifungua kwa mara ya pili.
"Upasuaji unasababisha hatari katika kondo la uzazi wakati wa ujauzito unaofuatia," inasema taarifa hiyo.

Lakini pia, upasuaji unasababisha familia ndogo. Kwa sababu mama hupangiwa asizae zaidi ya watoto watatu.

Taarifa hizo zinaongeza kuwa, watoto wanaozaliwa kwa njia ya upasuaji wengi wao hupata matatizo ya mfumo wa upumuaji.
Prisca Petro mkazi wa Dar es Salaam, alisema aliuguza kidonda kwa zaidi ya mwaka baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kauli ya mkunga
Mkunga Mstaafu, Angelina Mitande (73) aliyewahi kufanya kazi ya ukunga katika Hospitali za Muhimbili na mkoani Singida, ambaye kwa sasa anatoa huduma na ushauri kwa wajawazito katika Kijiji cha Chikunja, wilayani Masasi anasema, mjamzito anatakiwa apewe mafunzo ya kina mara tu anapogundulika kuwa na ujauzito.

"Zamani tuliwakataza wajawazito kula mayai, kwa lengo kuepusha mtoto asiwe mnene hali ambayo mara nyingi husababisha upasuaji wakati mama anajifungua, " anasema Mitande.

Alibainisha kuwa jambo lingine analotakiwa kufanyiwa mjamzito ni kusingwa (massage) mara kwa mara tumboni kwa mafuta ya nazi au karafuu ili kumuweka mtoto katika mkao mzuri.

"Hakuna zoezi muhimu kwa mjamzito kama kukandwa tumbo. Hili ndilo hukifanya kiumbe kilichoko tumboni kigeuke chenyewe, katika mikao mbalimbali na kichangamke," alisema.

Mitande anaonya kuwa mazoezi ni muhimu kwa wajawazito na anawataka kufanya kazi zote za nyumbani, kuwa wasafi na kula vyakula vyenye virutubisho.

"Wasichana wa sasa wanadeka sana na hudhani kuwa wakiwa wajawazito hawahitaji ushauri wa kijadi, wasidhani wataweza kuutua huo mtihani wa kujifungua bila elimu," anasema
Mitande na kuongeza:

"Maji ya moto kwa mama aliyejifungua ni muhimu kwa sababu yanasaidia kutoa uchafu uliobaki tumboni mwa mama baada ya kujifungua na pia hupunguza maumivu na kuponya mapema majeraha yaliyopatikana wakati wa kujifungua."

RIPOTI MAALUMU:Upasuaji tishio kwa wajawazito-2
 
Hili la kuchagua sidhani kama liko sana hapa kwetu; naowajua walofanyiwa operation; nikiwa mmoja wapo na marafiki zangu, ni madaktari walioshauri iwe hivyo kumuokoa mama na mtoto. Ni rare cases kukuta dada wa ki Tz anaomba apigwe kisu; na wengi wanaoomba hivyo nimeshasikia ni waathirika ili wasiambukize watoto kwa michubuko wakati wa kuzaa.

Na nataka nipinge kuwa operation ni mbaya kihivyo when necessary kwani hao the so called wakunga wangekuwa wazi watupe idadi ya waliowazalisha na ni wangapi walizaa salama na watoto wakawa hai. Hivi tunavyoongelea vifo vy wamama wajawazito na watoto tunaongelea wamama gani kama si hao wanaozalishwa na wakunga.

Haya mambo hayatabiliki. Mi si mvivu wala nini; mwanangu wa kwanza nilimzaa salama na kg 3.9; wa pili nilimzaa kwa kisu akiwa na kg 4.1 na si kwa kuwa njia ilikuwa ndogo ila ni kwa kuwa haligoma kushuka.

Hata kama aliyeongea ni doctor bado hii habari ni ya ki journalist zaidi kwani haija base kwenye scientific research.

Asante nyumba kubwa kwa somo. Lilinishangaza sana hili, kuwa hapa Tz tumefikia hapa. Kumbe sio habari za kuaminika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom