Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
najaribu kuwaletea kipande kwa kipande juu ya wanaojiita jumuiya ya madaktari walioathiriwa na mgomo ambao jana walisikika wakiomba msamaha.hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya social media za madaktari.
angalia sms ya bwana huyu(Dr sakwala) alivyokua jasiri .....
Ni Sakala huyu aliyekuwa akibandika matangazo na kutuma sms za kuhamasisha wenzake wa Mwananyamala, leo anadai ameshawishiwa? Yani unagoma mara 3 kwa miezi 7 unasema umeshinikizwa?
pia kuna hili linakuja...
check na hii hapa chiniThis is a highly classified information
Dr. Sakala akiwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha BUGANDO alifikia hatua kukigeuza Chuo kama Tawi la CCM kwa kuwashawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM pamoja na kusambaza kadi, Dr. Nuru Mwambola, ambaye amejibadilisha jina na kujiita Nuru light alituhumiwa kuhujumu wenzake akiwa Makamu wa Rais pale Kairuki mpaka kufikia kupigiwa kura ya kutokuwa imani nae, Ni Nuru ambaye amekuwa Mwanachama mtiifu kwa CCM alikuwa akitumika kushawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM.
Ni kwa kutumia nafasi hiyo, walikwenda kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Wakili Makene tar 21.08.2012 na kumuomba awakutanishe na Stephen Wassira ili waweze kuonana na Rais. Wakili Makene aliwajibu kuwa Wassira yupo nje ya Dar ila ametoa maelekezo kuwa Rais yupo tayari kuwaona ila waombe msamaha kwanza kwa rais, serikali na wananchi.
Baada ya agizo hilo ndipo wakaendelea na mchakato wa kukusanya majina ya interns, na kwa taarifa zilizopo ni kwamba ni inters 150 tu kati ya 319 ndio waliotuma majina yao. Baada ya kutekeleza agizo la kuomba msamaha hapo jana, baadhi ya wajumbe wa kamati ya Madaktari wa CCM walikwenda wizarani ili kupata mrejesho, na Naibu Waziri aliwajibu kuwa Mwizi akikiri ameiba kinachofuata ni hukumu. Huko ndiko shinikizo la Msamaha lilikoanzia.
WAKATI WA MGOMO WA MADAKTARI "DR PAUL SWAKALA" alizungumza maneno haya…
'Nasikitika kuona kwa jinsi gani ambavyo tunataka kukata tamaa, ambacho nataka kusema ni kitu kimoja, moja kati ya kada ambazo unasoma course unit nyingi kuliko kada yoyote ni udaktari, nasikitika kuona kwamba tunataka kuwa desperate na kuamini kwamba bila kutibu, bila kukutana na mgonjwa, bila kuajiriwa na serikali, there is no life, hiyo sio kweli kabisa, kama mlango mmoja utafungwa ninaamini kuna mlango mwingine utafunguliwa, nina uhakika kwa mtu ambaye amesoma degree iliyokamilika huwezi kukosa kibarua cha kukuweka mjini, nab ado maisha yataendelea kuwepo, na bado unaweza ukaishi vizuri hata kuliko utakapoingia kwenye kada hii ya kutibu…..huyu ni daktari Intern alokuwa akiwakilisha Mwananyamala kwenye mikutano ya …MAT'''
…Leo hii anazungumza hivi tena:
"Tunatumia fursa hii kupitia kwenu waandishi wa habari kuwaomba radhi watanzania wote na kwa serikali kutokana na madhara yaliyosababishwa na migomo ile ambayo ushiriki wetu ulikuwa hauepukiki.Tunajua wapo watu walioathirika na mgomo ule,hivyo tunaomba radhi watanzania wote walioathirika na mgomo,pia kwa usumbufu uliojitokeza…"
(MTANZANIA JUMANNE, SEPTEMBER 18,2012)
angalia sms ya bwana huyu(Dr sakwala) alivyokua jasiri .....
"Damu yangu iliyomwagika na iwe chachu ya kutuimarisha na kuendelea kudai maslahi ya madaktari" Maneno ya Dr Ulimboka wakati mamia wakimuaga akielekea nje ya nchi. Mimi( yaani yeye Dr. Sakala) hata kama nitabaki peke yangu sitamsaliti na kurudi nyuma, wewe je?
Ni Sakala huyu aliyekuwa akibandika matangazo na kutuma sms za kuhamasisha wenzake wa Mwananyamala, leo anadai ameshawishiwa? Yani unagoma mara 3 kwa miezi 7 unasema umeshinikizwa?
pia kuna hili linakuja...
Stay tuned, ntaendelea kutiririka mpaka donge aliloahidiwa