Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Rekodi huwekwa na kuvunjwa. Tangu tupate uhuru hatujawahi kuwa na Spika wa Bunge aliyevaa itikadi ( Partisanship) kama Spika Ndugai. Spika huyu anakipendelea chama chake kuliko hata Mwenyekiti wa chama chake au hata kuliko Katibu Mwenezi.
Nadharia ya uhuru wa bunge kama mhimili inatiwa doa la kihistoria kwa ukereketwa wa Spika huyu. Yule mchora katuni aliyechora kichwa cha spika au ubongo wake ukiwa na picha ya mkuu wa mhimili mwingine hakukosea. Spika huyu bila kujali madhara kwa mhimili wa bunge, anashiriki bila hofu mikakati ya kifitina kuwahujumu wote wanaoonekana wana msimamo tofauti na chama chake.
Ukereketwa ni sumu ya uhuru wa bunge. Kwa sasa spika ndiye bunge na bunge ni spika. Chaguo la wananchi kwa maelfu, linaweza kufutwa na kalamu ya spika dakika moja.