NDUKI
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 3,423
- 2,414
Ushiriki wetu upo na utaendelea kuwepo kama vile utakiwavyo kuwepo, ushiriki wetu upo hai mithili ya ROHO, ipo pale DAIMA MILELE japo ni ngumu sana kuiona kwa MACHO yaliyo (nachelea kulitaja hili jina hapa, sababu kuu na iliyo ya msingi ni kwamba, pengine nasema pengine naweza kukiuka misingi ya fikra za wachache zinazoweza kupelekea kwa wao binafsi kuamini kuwa nimetoka nje ya maadili yaliyo na uadilifu, hivyo acha nitumie lugha mbadala walau japo haitabadilisha maana halisi ya kile kilichonuiwa kwa makusudi yaliyokusudiwa kunenwa) nasema hivi, ushiriki wetu upo HAI mithili ya ROHO japo ni ngumu kuiona ROHO kwa kutumia NAKED EYES lakini kwa hakika iliyo hakikika na kuhakikiwa ni kuwa haki ya kuwepo na uwepo ulio na haki ama hakika ushiriki wetu, UPO.Laiti ushiriki wetu ungekuwepo mithili ya mwili basi tusingekuwepo hapa mpaka mnamo majira haya yaliyotuwezesha kuchangia mchango huu yakinifu kwa yakini iliyoyakinika kwa kina, kwa kuwa tu mwili hufika kikomo cha muda hivyo ushiriki wetu haupo hapa mithili ya mwili uwavyo vile, lakini pia ushiriki wetu si kama NAFSI kwa vile tu NAFSI yahitaji mengineyo yajulikanayo ili kuweza kuwa pale, haiyumkini kuweza kuwepo pasina MWILI NA ROHO kuweza kuwepo, lakini kwa ROHO haitahitaji uwepo wa chochote kile kiwacho ili yenyewe iweze kuwepo ; ilikuwepo, ipo na yenyewe itakuwepo pale siku zote, pasina kujua huyu mwengine kuwa ipo pale kwa kutumia MACHO YALIYO (...). Isipokuwa tu kwa kutumia JICHO LILILOVAA NGUO (LILILOJIFICHA). Hivyo, kwa maelezo yaliyo machache nalazimika kusema kuwa ushiriki wetu upo na utaendelea kuwepo pia, si tu kwa kutia NENO au MCHANGO wowote ili tu kuweza kujulikana kuwa UPO laa hasha, ila kwa yeyote yule awaye IBADANI nae ameshiriki, japo sio ulazima wake nae aweke maneno ama mchango ili afanane kama kasisi ama mchungaji ili awe ndio ameshiriki HAPANA, lakini pia hata kwa kusikiliza tu yale yaendeleayo na yatokayo kinywani yakitokea moja kwa moja nyoyoni kupitia kunako (madhabahu) mahala hapo husika anakuwa ameshiriki pia, acha tushiriki kwa njia ipasayo kushiriki ; na njia ionekanayo inafaa kwa vile inavyo na vile itakavyo-kuwa ikionekana kuwa inafaa pia. Jimena anafaham kuwa #ulipotupo.
Last edited by a moderator: