Regina Mwalekwa wa Clouds FM alamba shavu BBC!

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,814
Mtangazaji mahiri wa Clouds FM ,REGINA MWALEKWA, ameaga resmi leo asbh hii, huku akibubujikwa na machozi ya Furaha kuwa anaiga familia ya Clouds FM na kuhamia BBC!

Binafsi namshukuru Mungu kwa mafanikio yake, ila zaidi nilijua Kiswahili fasaha kupitia yeye toka akiwa Radio One!

Mungu akutangulie huku uendako Dada Regina, kaiwakilishe Tanzania vyema, hususan tasnia ya habari!

attachment.php
 
Kama Ni Kweli Basi BBC Wamepata Jembe Kwani Dada Huyo Ana Karibia Sifa Zote Kuu Na Muhimu Za Mtangazaji Na Mwandishi Wa Habari. Sina Shaka Nae Na Hata Rekodi Yake Ni Nzuri. Binafsi Namtakia Kila La Kheri Huko Uingereza Aendako. Sifa Ziende Kwa Redio One Waliomwibua Kisha Clouds FM Kwa Kumtengeneza Na Kumsafishia Njia Ya Mafanikio. Hongera Na Heko Zako Dada Regie....................!
 
Nimekuwa nikijiuliza nini kinafanya Mtangazaji Bora kabisa kama huyu asipae kimataifa? Nadhani sasa swali langu limepata jibu. Namkubali zaidi ya sana, hasa katika kukuza lugha ya kiswahili na matumizi fasaha ya lugha hiyo....

Kaitangaze Tanzania Mama, Kaikuze Lugha yetu adhimu ya Kiswahili Kimataifa....Kila la heri
 
nimemsikia akiaga mpaka analia, amewasamehe wote waliokuwa wanamponda FB, Instagram na Jamii forums.

Mwenye hekima hujifunza kila wakati hata kutoka kwa wapumbavu. Amejifunza nin kutoka kwa hao waliokuwa wanamponda?
 
huyu dada ni jembe. Mi namuamini sana. Walimfanyia figisu radio one akatoboa. Amekwenda clouds napo nimepaona ni padogo kwa u great thinker wake. Kila la heri da Regina huko uendako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom