Refa Ampa Kadi ya Njano Marehemu Kwa Kupiga Mbizi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
4446934.jpg

Thursday, May 06, 2010 10:42 PM
Refa wa mechi ya ligi nchini Croatia bila kujua alimlima kadi ya njano mchezaji aliyeanguka kwenye eneo la penalti akimlaumu kwa kujiangusha wakati ukweli ni kwamba mchezaji huyo alikuwa amefariki dunia uwanjani. Goran Tunjic mchezaji wa timu ya Mladost FC mwenye umri wa miaka 32 alianguka kwenye eneo la penalti katika mojawapo ya purukushani zilizotokea kwenye lango la timu pinzani.

Refa wa mechi hiyo bila kujua kuwa mchezaji huyo alianguka kutokana na matatizo ya kiafya, alimfuata mchezaji huyo na kumuonyesha kadi ya njano akisema kuwa mchezaji huyo alikuwa amejiangusha mwenyewe kwenye eneo la penalti ili timu yake ipewe penalti.

Tukio hilo lilitokea kwenye dakika ya 35 ya mechi kati ya Mladost FC na Hrvatski Sokola.

Baada ya kuona mchezaji huyo ametumia muda mrefu chini na wala hanyayuki ilibidi madaktari waitwe uwanjani ambapo iligundulika kuwa mchezaji huyo alikuwa amekumbwa na shambulio la moyo.

Pamoja na jitihada zote za madaktari, Tunjic alifariki dunia ingawa aliwahishwa hospitali iliyo karibu na uwanja huo.

"Madaktari walijaribu kumsaidia lakini hawakuweza kuokoa maisha yake", alisema msemaji wa timu hiyo.

"Alinguka chini na kufariki hapo hapo", aliongeza msemaji huyo.

Taarifa zilisema kuwa Tunjic alikuwa hana matatizo yoyote ya kiafya kabla ya kifo kumkumba uwanjani.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4446934&&Cat=6
 
Plz habari zingine ziwe zinaangaliwa sehemu ya kuwekwa kwani kama hii inaonekana kama ni kweli kumbuka issue ya Marc Vivian Foe na yule mchezaji wa simba 1979.
 
Back
Top Bottom