RC Makalla amuagiza Kamanda Wambura kuwapora silaha majambazi kabla hawajazitumia, amtaka awape ‘show’ kali

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,273
42,211
Habari wanajamvi

Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana RC Makalla kwa kauli yake leo juu ya uhalifu na ujambazi unao endelea jiji la Dare-es -saaam kwa kuwataka jeshi la polisi kuwapora haraka silaha majambazi kabla hawajazitumia.

Ni ukweli ulio wazi majambazi wameanza kutishia amani na usalama wa jiji la Dares-es-salaam yani utafikiri walikuwa likizo sasa wamerudi kuendelea na kazi na hawa watu ni majambazi na jeshi la polisi haliwezi kutumia demokrasia kupambana nao bali dawa yao ni moto tuuu.

Nimpongeze wazi kabisa Amos Makalla kwa kumwambia wazi kamanda Wambura kuwa watu wamekuja na moto lazima wakabiliwe kwa moto kabisa tena mkali na Wambura ameambiwa awape show kweli kweli.

Watanzania lazima wajue kuwa majambazi hawawezi kukabiliwa kwa njia ya demokrasia maana na maneno matupu bali vitendo na hawatakiwi kukamatwa bali kupigwa shaba maana wao wanaua hadharani kabisa na kuleta hofu kubwa.

Mimi sikubaliani kabisa na huu mtindo wa kusema Wambura amekamata majambazi watano.... hivi ana wakamata wanini kwanini asimalizane nao uko uko field, yani hawa majambazi tufanye kazi ya kuwalipia ugali tena wabure?

Dar.jpg

Wasalaam
 
Polisi ni mwizi namba moja. Kuna wakati natamani tupate RPC mjeda aliyesomea Mambo ya upelelezi awafukue majambazi na kumalizana nao.

Polisi wengi wanaficha wahalifu maana wanakula nao, kama hakuna uhalifu then polisi anakuwa jobless hapo anajua hata dili hazitakuwepo.
 
Hiyo ni kweli kabisa kuna askari ambao wanashirikiana na hawa waharifu. Mimi Nina mifano hai kabisa, miaka mitatu iliyopita dereva wangu akishirikiana na mlinzi wangu walifanya mbinu na kuvunja nyumbani kwangu wakati niko safarini na kufanikiwa kuniibia vitu vingi.

Nilipotoa taarifa polisi mtego uliwekwa ili kumkamata yule dereva, bahati mbaya kumbe yule dereva alikuwa wanafahamiana na askari kanzu mmoja aliyekuwemo mule ofisini wakati mpango wa kumkamata unafanywa, akampigia simu yule dereva na kumuambia kuwa anatafutwa hivyo asirudi nyumbani kwake. Ikawa vigumu kumkamata yule mwizi kwasababu ya yule askari kanzu!!!

Yule askari kanzu akiitwa MWAKILASA alikuwa kituo cha Kawe kwa muda mrefu akahamishiwa kituo cha polisi kipya BUNJU/MBWENI!! kama bado yuko kazini afande Wambura amtazame kwa jicho la karibu sio askari muaminifu!!!
 
Miaka ya nyuma kuna ndugu yangu alitapeliwa na madalali fake, alipoenda polisi haohao polisi walianza kumuuliza sura za matapeli. Baadaya kuwaelezea sura za matapeli ndipo polisi walianza kutaja majina ya matapeli. Polisi hao hao walianza kuwapigia simu matapeli kwa kuwa walikuwa na namba zao. Hapo ndipo tunajifunza kwamba polisi wanawajua baadhi matapeli na wezi vizuri sana.
 
aiseeeeeeeeeee
 
Habari wanajamvi

Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana RC Makalla kwa kauli yake leo juu ya uhalifu na ujambazi unao endelea jiji la Dare-es -saaam kwa kuwataka jeshi la polisi kuwapora haraka silaha majambazi kabla hawajazitumia ..

Ni ukweli ulio wazi majambazi wameanza kutishia amani na usalama wa jiji la Dares-es-salaam yani utafikiri walikuwa likizo sasa wamerudi kuendelea na kazi na hawa watu ni majambazi na jeshi la polisi haliwezi kutumia demokrasia kupambana nao bali dawa yao ni moto tuuu...

Nimpongeze wazi kabisa Amos Makalla kwa kumwambia wazi kamanda Wambura kuwa watu wamekuja na moto lazima wakabiliwe kwa moto kabisa tena mkali na Wambura ameambiwa awape show kweli kweli.....

Watanzania lazima wajue kuwa majambazi hawawezi kukabiliwa kwa njia ya demokrasia maana na maneno matupu bali vitendo na hawatakiwi kukamatwa bali kupigwa shaba maana wao wanaua hadharani kabisa na kuleta hofu kubwa.

Mimi sikubaliani kabisa na huu mtindo wa kusema Wambura amekamata majambazi watano.... hivi ana wakamata wanini kwanini asimalizane nao uko uko field, yani hawa majambazi tufanye kazi ya kuwalipia ugali tena wabure?

Wasalaam
Hii siyo kujichukulia sheria mkononi au?
 
Polisi ni mwizi namba moja. Kuna wakati natamani tupate RPC mjeda aliyesomea Mambo ya upelelezi awafukue majambazi na kumalizana nao.

Polisi wengi wanaficha wahalifu maana wanakula nao, kama hakuna uhalifu then polisi anakuwa jobless hapo anajua hata dili hazitakuwepo.
Umemaliza mkuu,hii mada ifungwe.
 
Nashauri hawa majambazi wakikamatwa na Silaha ni kumiminia shaba tu ndio dawa,juzi wameua raia mwema pale mbezi
 
Ukishakuwa Well enough informed unaenda tu field na Mchoro wa kujua wapi nimalizane nao kabisa field wapi niwajeruhi wawe hai bado kwa ajili ya upepelelezi ili kupata hio chain yao, Hao Casualties nao ni wakuhoji hardly with interrogation ya hali ya juu wakishafungukwla unabeba unaenda kuzika wazima wazima, Majambazi hawahitaji diplomasia wala kukaa nao mezani hapo ni Moto moto
Jeshi la polisi linahitaji decison makers wenye roho mbaya haswa hata kama wataonekana soft kwenye jamii
 
Kazi za maelekezo hazifanyiki hivyoo..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom