RC Hapi apokea taarifa ya uchunguzi wa mradi wa maji Pagawa Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
RC HAPI APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI MRADI WA MAJI PAWAGA-IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wahandisi wote waliomdanganya kuhusu taarifa za mradi wa Maji wakati akiwa kwenye ziara yake ya IRINGA MPYA tarafa ya Pawaga, huku mamlaka ya maji IRUWASA ikitakiwa kujitathmini.

Hayo yamejiri baada ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda mapema mwezi September wakati wa ziara yake kuchunguza mradi huo wa Maji uliozua sintofahamu katika usimamizi wake. Kamati hiyo iliyoundwa na wataalam kutoka vyombo mbalimbali imewasilisha taarifa yake kwa Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake leo.

Pamoja na mambo mengine, mradi huo wenye thamani ya bilioni 4.8 umebainika kuwa na mapungufu kadhaa yakiwemo yafuatayo:-

1. Sampuli za matofali ya zege ya kujengea matanki ya kuhifadhia maji hazikupelekwa maabara kupimwa ili kujiridhisha na ubora kabla ya uzalishaji kuanza kinyume na mkataba. Mkandarasi ametengeneza matofali ya zege 18,000 na mwingine 6082 bila sampuli kupimwa maabara.
Wahandisi wa halmashauri ya Iringa walimdanganya Mkuu wa Mkoa kuwa upimaji umefanyika maabara.

2. Mfumo dhaifu wa usimamizi wa mradi huo uliosababisha wakandarasi kujiamulia mambo na kufanya kazi kwa mazoea bila usimamizi madhubuti. Mamlaka ya maji Iringa IRUWASA ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mradi.

3. Kushindwa kujiridhisha halmashauri ya Iringa juu ya uhalali wa dhamana ya benki “ Bank Guarantee” katika benki husika kama ni kweli wakandarasi wametoa taarifa sahihi. Tayari wakandarasi wameomba kupewa malipo ya awali ya zaidi ya milioni 700.
4. Wahandisi wote walioandikwa kwenye mikataba na wakandarasi wakati wa kuomba kazi hawapo site na taarifa haijatolewa kwa mamlaka husika.

Kufuatia taarifa hiyo, RC Hapi ameagiza kuchukuliwa sampuli za matofali hayo ya zege yapatayo 24,082 na kupimwa maabara ya wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Iringa kuona kama yanakidhi ubora, na ikibainika kuwa hayakidhi Mkandarasi atalazimika kutengeneza mapya kwa gharama zake mwenyewe.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa kutofanya malipo yoyote hadi hapo watakapojiridhisha na benki husika kama hati ya dhamana (Bank guarantee) iliyowekwa na mkandarasi ni halali na haina mashaka.

Katika hatua nyingine, Hapi ameagiza Katibu tawala Mkoa kukaa na mamlaka ya maji IRUWASA na kuweka mfumo wa pamoja wa kusimamia miradi ya maji Mkoani Iringa ili kuendana na agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli la kuhakikisha miradi ya maji inasimamiwa vema.

Kwa wahandisi waliotoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa Mkoa, Hapi ameagiza mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kali.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amefanya kikao na wahandisi wa maji wa halmashauri zote kujadili namna bora ya kusimamia miradi ya maji mkoani Iringa.
IMG_20181029_171231_320.jpeg
 
Ni taarifa ya kamati maalum aliyounda kuchunguza mradi wa maji wa bilioni 4.8 Tarafa ya Pawaga

Kamati yabaini wahandisi walimdanganya RC,taratibu hazikufuatwa na kazi imeanza.

#SerikaliIpoKazini #IringaTupoKazini #HapaKaziTu #MajiNiUhai View attachment 915237
IMG-20181029-WA0091.jpeg
 
Back
Top Bottom