Ratiba ya M4C- Operesheni Pamoja Daima, Ruvuma, Tabora na Tanga

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468

Kama ambavyo jana umma wa Watanzania ulitaarifiwa kupitia kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wanahabari, Chama leo kinaanza operesheni ya takriban wiki mbili kwa nchi nzima (mijini na vijijini).

Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.

Timu hizi zinajumuisha viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu, Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na wabunge wote wa CHADEMA katika maeneo husika.

CHADEMA itatumia operesheni hii ya wiki mbili kuandaa umma wa Watanzania juu ya masuala kadhaa muhimu kwa hatma ya nchi yao;

1. Mjadala wa rasimu ya pili ya katiba mpya- Bunge Maalum la Katiba Mpya
Wakati huu ambapo nchi Watanzania wanasubiri vikao vya Bunge Maalum la Katiba,
pamoja na Tume ya Warioba kufanya kazi nzuri kwa kukusanya na kuzingatia
maoni ya watu (ambayo CCM wanayapinga wakiweka mbele maslahi ya chama
chao badala ya Watanzania wenye nchi yao), bado kuna masuala ambayo;

(a) yanahitaji msisitizo yaendelee kubakia kwenye rasimu

(b) yanahitaji kuboreshwa

(c) yanahitajika kuongezwa kwa sababu hayamo

2. Kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni kuamua
Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hii ni moja ya shughuli ya 'kufa na kupona' mwaka huu kwa sababu kuna
mamilioni ya Watanzania hadi sasa Serikali ya CCM imewanyima haki yao ya
kikatiba ya kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao, maendeleo yao kupitia kura.

3. Uchaguzi wa ndani ya chama ambao hadi sasa unaendelea katika ngazi ya msingi
nchi nzima hatimaye ngazi ya taifa.

4. Masuala ya Watanzania na umiliki wa rasilimali zao ambazo kwa sasa zinaonekana
kuwanufaisha wageni, watawala na watu wenye mahusiano na watawala, pia hali
ya ugumu wa maisha inayozidi kuwakabili wananchi ikiwa na uhusiano na uongozi
mbovu unaokumbatia ufisadi na sera zilizoshindwa, yatapewa kipaumbele kikubwa
katika ziara hii.

5. Bila kusahau kwamba 'all politics is local', hivyo chama kitatumia fursa hii
kuzungumza na wananchi juu ya kero mbalimbali zinazowakabili na CHADEMA
inaweza ku-offer nini. Na mengine kadha wa kadha yenye umuhimu kwa
maendeleo ya watu.

Ifuatayo ni ratiba ya leo na kesho kwa timu tatu za angani ambazo zinatumia usafiri wa helkopta 3;

Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa;

Mbambabay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo kisha kwa leo watamalizia Songea Mjini

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed

Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini

Timu ya Kamanda Tundu Lissu na John Heche

Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga mjini

* Tutawapatia updates kadri muda unavyokwenda. Accounts za CHADEMA mitandaoni ikihusisha pia 'vyombo' vya chama kama websites na blogs, ndizo zitakuwa vyanzo rasmi vya taarifa za uhakika kwa kila kinachoendelea field.

Tutashirikiana na mods pamoja na watu wengine wote hasa walioko fields kwenye timu zote 6 kuhakikisha Watanzania wanapata taarifa sahihi, za uhakika, kwa wakati, huku pia tukiomba uvumilivu wenu na subira inapolazimika, ili kupata vitu vizuri maana mikutano itafanyika maeneo ya vijijini na mijini.

Punde tutatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za watu kama vile, kwa nini helkopta (tena idadi imeongezeka, hakuna chama cha siasa kiliwahi kufanya kama hivi kwenye operesheni kama hii), kwa nini PAMOJA DAIMA (wengine wanafikiri ni tofauti na M4C).

Haya karibuni kwa ajili ya M4C- PAMOJA DAIMA hii ndiyo habari yenyewe kwa sasa.
 
Zitto kabwe atakua anazungukia pande/nyanda/mikoa gani kwenye hiyo M4C daima?
 
Hizi operesheni zimekuwa nyingi mpaka nyingine nimezisahau, watz nao ni wagumu kuelewa halafu wepesi kusahau
 
...

....Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.

.....Nahapa Sombetini kikosi cha nchi kavu ...brigade maalum... Arusha kimemaliza kazi.....ccm arusha iko ICU
.
 
Hizi operesheni zimekuwa nyingi mpaka nyingine nimezisahau, watz nao ni wagumu kuelewa halafu wepesi kusahau

Mkuu ushajiuliza kwa nini Makampuni ya simu kila siku wanakuja na vitu vipya? Mfano SAMSUNG walipo toa S3 walisema ni the best phone ila baada ya muda mfupi wakaja na S4 so CDM nao ndo wanacho fanya wanaleta product pya na hii ni kufanya wadau wasichoke na product ya mwanzo, umenielewa?
 
...

....Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.

.....Nahapa Sombetini kikosi cha nchi kavu ...brigade maalum... Arusha kimemaliza kazi.....ccm arusha iko ICU
.

Mkuu unanikupusha ile vita ya Mmarekani na Sadam Hussen, Jamaa alikuwa anashambulia juu na chini uku Sadamu Hussen akijipa matumaini na kutamba kuwa eneo la Baghdad litakuwa eneo maalumu kwa ajili ya makaburi ya Wamarekani. Kuja kutahamaki Marekani wameshatia timu mpaka Ikulu ikabidi jamaa akajifiche kwenye mashimo.
 
Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa;

Mbambabay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo kisha kwa leo watamalizia Songea Mjini

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed

Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini

Timu ya Kamanda Tundu Lissu na John Heche

Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga mjini

* Tutawapatia updates kadri muda unavyokwenda. Accounts za CHADEMA mitandaoni ikihusisha pia 'vyombo' vya chama kama websites na blogs, ndizo zitakuwa vyanzo rasmi vya taarifa za uhakika kwa kila kinachoendelea field.

Naona safari hii CDM mmesikia kilio cha Watanzania.Big up sana.Nakubaliana na uchaguzi wenu wa maeneo ya kushambulia,wananchi wa Tanga wameisubiri CDM kwa mrefu mno. Maeneo ya Arusha,karatu etc tayari wananchi wanataka mabadiliko hivyo sioni sababu ya kuendelea kuyarudiarudia
 
Mkuu unanikupusha ile vita ya Mmarekani na Sadam Hussen, Jamaa alikuwa anashambulia juu na chini uku Sadamu Hussen akijipa matumaini na kutamba kuwa eneo la Baghdad litakuwa eneo maalumu kwa ajili ya makaburi ya Wamarekani. Kuja kutahamaki Marekani wameshatia timu mpaka Ikulu ikabidi jamaa akajifiche kwenye mashimo.

....Hili shambulio linakwenda kuingamiza ccm
 
Back
Top Bottom