Tetesi: RAS Singida atoa notice ya kuwafukuza kazi watumishi zaidi ya 20 kwa kufoji vyeti

Acha uongo umesema amefanya kazi zaidi ya miaka 30 wakati huohuo unasema alifoji miaka 1998. Acha kutudanganya
”Alifoji cheti 1998 kulikompelekea kusoma cheti na diploma anayoifanyia kazi hivi sasa". Kama unashindwa kuelewa hapo,basi wewe ni ZERO,oh samahani,wewe ni Bashitian.
 
Alifoji vyeti mwaka 1998.
Kisha kaitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 30. Hesabu imenipoteza hapo. Ila kuhusu usahihi wa taarifa mimi siyo Tomaso
"Alifoji cheti mwaka 1998,akasoma cheti na hatimaye diploma anayoifanyia kazi sasa". Wapi hujaelewa? Bashitian nini wewe? Mimi kuna mjomba wangu alikuwa ni darasa la saba,ulipotoka waraka wa serikali kuwa waajiriwa wote wa serikali wawe kidato cha nne,alisoma QT halafu akafanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2003. Wakati waraka unatoka,alikuwa ni dereva wa taasisi fulani kwa muda wa miaka 9. Mpaka sasa bado ni dereva wa hiyo taasisi. Kwa hiyo hesabu ya utumishi wake wa serikali unaanzia wapi?
 
Bashite hata akisikia kuna watu wamefoji vyeti itabidi akaushe tu maana akijifanya mjuaje watu watamwambia ukweli.
 
Unaongeza Mapembe Uote Bashite

[HASHTAG]#BashiteOnyeshaVyeti[/HASHTAG]
[HASHTAG]#AchaManenoOnyeshaVyeti[/HASHTAG]
 
Mtu ambaye ni mtumishi zaidi ya miaka 10 huyo ana uzoefu masuala ya kutaka cheti chake si sawa labda kama utendaji kazi wake ni mbovu
 
Acha uongo umesema amefanya kazi zaidi ya miaka 30 wakati huohuo unasema alifoji miaka 1998. Acha kutudanganya
Kama alikuwa anafanya kazi kama mlinzi halafu baadae akajiendeleza, alichokisema mwanzisha mada kinaeleweka
 
Hi wanabodi!!!

Nimepenyezewa ujumbe wa karibu kutoka singida kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa huo ametoa kusudio la kuwatimua kazi watumishi zaidi ya 20 kwa tuhuma za kufoji vyeti vya kidato cha nne.

Mtoa habari anasema Mama yake ambae ni mtumishi wa zaidi ya miaka 30 katika utumishi wa umma ambaye kabakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wa umma leo amezimia zaidi ya mara tano hivyo kushindwa kabisa kupeleka barua ya maelezo kwa RAS ya kwanini asichukiliwe hatua za kinidhamu.


Mods Habari hii ni ya kweli kabisa kama mtathibisha ni habari ya uongo kuhusu RAS kutoa notice YA kuwachukulia hatua za kinidhamu waliofoji nipigwe BAN KABISA
Kwakweli ni kilio cha ukoo kimetamalaki kijana aliyenipa ujumbe kwasasa upo safarini kutoka UDSM kwenda kumpa Mama yake matumaini ya kuishi tena. kijana amesema ni kweli mama yake alifoji vyeti miaka ya 1998 hivyo kumfanya kupata mafunzo ya certificate na badae Diploma ambayo anaitumikia kwa kufanya kazi katika taasisi nyeti mpaka sasa.

Kijana amesema akifika usiku huu nyumbani kwao atatumia barua ambayo mama yeke amepewa na mwajiri wake na utetezi ambao mama yake ameutoa lakini ameshindwa kuuwasilisha hadi sasa baada ya kuzimia mara kadhaa.

Mods: habari hii ni ya kweli kabisa kama mkichunguza na kukuta kuna uongo nipigwe BAN aidha baadhi ya watumishi waliokumbwa na kadhaa hii wengi wao kwasasa ni wazee wa miaka 50 mpaka 58 wanaomba msaada wa waandishi na wanasheria
Wanaomba msaada wa nini,waondoke tu.Kinachofuata ni kupelekwa mahakamani kwa tuhuma za kuiibia serikali na kutakiwa kulipa hela zote walizoiba with interest!Nawahurumia sana. Lakini my question is why did they do it for God's sake? Ni tamaa tu za kijinga.
 
Back
Top Bottom