Rais wenu 'tuu bize'

Shishye

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
269
1
Nimelikumbuka jambo moja ambalo niliwaahidi watanzania wenzangu wakati natafuta funguo za Ikulu! Ama kwa hakika watanzania wanadanganyika kirahisi sana. Nilijifanya nitashughulikia kwa nguvu zangu zote kurekebisha mikataba ya madini ambayo illingiwa kifisadi. Ni ukweli usiopingika hadi leo kwamba nchi yetu inapata 3% tu kama kodi ya mrahaba, 97% inatokomea kwa wakoloni. Sio tofauti na ilivyokuwa kabla sijaingia madarakani.

Ahadi hiyo ilinipa ujiko sana hadi watanzania kama kawaida yao wakaanza kudanganyana eti kwamba mimi na raisi aliyepita moshi na pua; wakaunganisha na uwongo mwingine wa zile nyumba za mawaziri kuwa eti mimi nilikataa kununua ili nije kuwachukulia hatua. Yote hayo sikuyazungumzia chochote maana yalikuwa yananijengea ukali mimi mpendwa wao ambaye nilijua kiukweli hayo si matendo yangu wala kamwe sitathubutu kwenda kinyume nayo.

Anyway, siku chache baada ya kuingia ikulu nikajifanya nina moto wa hili na lile; hasa kukutana na watendaji wakuu wa idara mbalimbali wa wizara na uongozi wa serikali. Nilikaa na wakuu wa wilaya na mikoa; makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wao na kupeana mikakati ambayo niliahidi kuwa ningefuatilia utekelezaji wake mara kwa mara.

Siku zilivyozidi kwenda nikagundua huyo si mimi. Mambo kama hayo hayakuwa kipaumbele kwenye malengo yangu ya kuingia ikulu. Ndipo nikarejea list yangu ya vipaumbele na kuachana na hayo yote! Niko bize nazuru dunia. Wengi wamechonga sana lakini habari ndio hiyo.

Baadaye nikazuka kisanii kwenye TV yao ya taifa na maswali niliyokwisha kujiandalia huku nikiwashawishi waniulize maswali niwajibu laiv. Kiukweli nilikuwa nawakebehi tu ili nijue walikuwa na mambo gani ya msingi ya kuniambia. Maswali meeengi waliyonitumia hayakunigusa wala hayakuwa kwenye mwelekeo wangu wa utelekelezaji, hivyo niliwaahidi kuwa nitafanya mikutano ya hadhara baadaye niyajibu. Uzuri wa bongo, ikitoka imetoka.

Muda si muda nitakuja na ripoti nzuuuuri ya kuwazuga tena, nina hakika haya yote ya safari zangu na utendaji wangu mtakuwa mshasahau na kusamehe; nitakuja kuwakumbusha tena kuwa bado nina miaka mitano mipya ijayo ya kuwaongoza, I mean ya kuendelea kutalii nchi za nje. Na nchi yetu inavyosifika kwa kuwa na watu wapole, wema, wapenda amani, wenye imani kubwa na mapenzi mema kwa taifa lao na chama tawala, watanichagua tena kwa mwitikio wa kishindo hata zaidi ya kipindi kilichopita.

Sina shaka na kupewa miaka hiyo mingine mitano. Watanzania wana imani kubwa na mimi. Kwanza wengi wanajua utendaji wangu ni wa hali ya juu. Wachache wanaojifanya kupinga tutawashughulikia tu kwa vyombo vyao wenyewe. Kumbukeni tu kuwa, mkiona mtu anakimbilia ikulu 'mwogopeni kama ukoma'.
 
habari ndo hiyo cuba itahakikisha inaisaidia Tanzania kupunguza maralia ..
tuu busy
 
JK kwa sasa ni Raisi na Foreign minister hamjuagi.
Lazima avinjari dunia nzima hana uhakika wa 2nd term.
Mkwere uyo bwana kwereka kwa raha zako
 
Hajui chakufanya, alishakiri hajui kwanini watanzania ni masikini, hajui nini wajibu wake. Wanamtandao wamemzonga kila akiingia Ikulu wapo nyuma yake kumdai atimize ahadi alizowaahidi, anawaonea aibu na kuwachekea chekea, hana utashi wa kukemea mafisadi wakati wananchi wanambana wakitaka kujua hatma. Njia pekee kwa mjinga ni kukimbia na ndicho bwana huyu anakifanya. Ana buy time siku ziende na kama shamba lisilo na mwenyewe litaendelea kuwepo bila kujali kila anaekuja analima na kuvuna na kuondoka. Poor Tanzania, laiti 2005 Watanzania wangejua kutenganisha Sura nzuri/ U handsome (Kama wapambe wakewalivyokua wakidai na kujinadi) na utendaji wa kazi. Huyu bwana hakuwahi kuwa na record yeyote nzuri ilotambulika kiutendaji lakini kwakua alikua na tabasamu kubwa na uhandsome wanavyodai watu wakamchagua.

2010 Uchaguzi huo..... sijui vigezo gani tena vitaletwa.

Yetu macho
 
ya 'rahisi' wetu kuwa bize yanakuhusu nini wewe??? wenyewe twaona sawa tu.....tunakushangaa ujue
 
tetetetete TOO LATE TO CATCH THE TRAIN. Mkwere anakula kuku kwa mrija. si ulimwona alivyokuwa anasupp. mambo ya watoto ya kubembea mita 50 high. Kwa kifupi hajui pa kunazia kwa hiyo sasa hivi anakula pension. KAMA MAISHA BORA AMESHINDWA KUWAPA WATANZANIA ameona ni BORA AJIPE YEYE MAISHA BORA NA MAFISADI
 
habari ndo hiyo cuba itahakikisha inaisaidia Tanzania kupunguza maralia ..
tuu busy

Teh Teh hapo ndipo patamu kwanini, Cuba watajitolea kufanya iyo kazi ukizingatia ni Nci ya Kijamaa rai wao hujitolea sana, wana siasa ya ujamaa na kujitegemea kwahio ni nguvu kazi na elimu, hapa kwetu sijui kama tutatoa support ili kuliondoa hilo tatizo la maralia, hawa wa Cuba watakuaja na elimu nyini ya kuwaelimisha watanzania na pesa kidogo, tatizo hilo sasa watanzania wakisikia pesa ni kidogo hawata volunteer kwa wingi labda vijijini ndiko wata volunteer huku mijini wao wange volunteer endapo fund ingekuwa kubwa. Mkichunguza miradi mingi mtaona

 
Back
Top Bottom