Rais wangu JK usimchague Makongoro kwenye baraza jipya, atakuchafua

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Kwa wanajamvi kwa ujumla.

Natumanini wote mtakuwa mmesikia hukumu iliyovuta hisia za watu wengi ya jimbo la Segerea. Ni kilio na furaha kutegemeana na upande uliopo.

Lengo langu la leo si kujadili hukumu bali kumpa ushauri rais wangu Jakaya M. Kikwete kuwa asimchague au asimrudishe Mh. Makongoro Mahanga katika baraza jipya la mawaziri analotarajiwa kulitangaza muda wowote wiki hii.

Kwa nini nasema hivi?

Ni wazi ushindi wa Makongoro licha ya kuonekana na mawaa mengi machoni pa wananchi ambao ni wapiga kura lakini sheria haijamtia hatiani.

Kutokana na hilo la ushindi wa Makongoro kuwa na mawaa, sikiliza kilio cha wapiga kura indirect kwa kutomrudisha Makongoro katika baraza jipya atakuchafua.

Ukifanya hivyo utakuwa umetibu makovu ya wengi ambao wanaamini kabisa Mahanga kapendelewa na kurudisha imani kwa wananchi katika hukumu ile hakukuwa na mkono wako ili umrudishe barazani licha ya kesi kuonekana kumkalia kooni.

Endapo ukimrudisha wakatokea wajanja na kupitisha maneno katika media au vyovyote vile utakuwa na wakati mgumu wa kujitetea japokuwa naamini huwajibiki kujitetea kwa yoyote yule.

Ni kweli lakini uchungu wa wananchi ambao wangependa kusikia sauti yako kupitia baraza la mawaziri kwa kutoiona sura ya Mahanga inaweza kuwa mbaya sana 2015 kwa utakayempa kijiti akupokee endapo atarudi tena.

Kwanza utendaji wake ni wa kawaida sana na safu yako bado ina watu wengi ambao wanaweza kuwa mbadala kwa huyo mtu mmoja ambaye aaweza kukuchafua pasipo sababu.

Naomba ulione hili kwa uzito wake.

Karibuni kwa mjadala huu.

Losambo.
 
Mwenye shibe huwa hamjui mwenye njaa!

Ni kweli hata kama una shibe ni vyema ukatambua watu wengine wanalala na njaa au kufa kabisa kwa kukosa mlo.

Ni vema kiongozi wetu akaliona hili sisi wenye njaa kwa kutomrudisha huyu mtu ambaye bado ushindi wake hauna mvuto kabisa.

Naamini wapo wanaCCM wengi wa kucover nafasi yake awape nafasi badala ha kumng'ang'ania Makongoro!!!!!!
 
Akimteua Mahanga na Aibu ya mhimili wa mahakama leo atajishushia hadhi..mwizi wa masanduku ya kura yule.

Naunga mkono hoja kabisa, Makongoro abaki kuwa mbunge wa kawaida baada ya kushinda kesi yake.

Hakuna haja ya kumn'gang'ania mtu ambaye usafi wake unatilisha mashaka.

Na kama akifanya hivyo atazidi kukoleza pilipili kwenye kidonda kibichi, watu watazidi kuichukia serikali na kuamini mhimili wa mahakama iliingiliwa ili abwebwe!!!!!
 
Haha haha haha haha!!!!! Kibanga umenifurahisha sana. Unakusudia JK anaweza kumrudisha kwenye baraza lake kwa sababu huo ni upepo tu na utapita?

Ikiwa ni hivyo basi ikulu itakuwa haina washauri!!!!!

haha. Majungu au ni upepo tu utapita.
 
pamoja na ushindi kwa hakika mahanga amani hanayo moyoni, hata kama kuna tabasamu usoni. Maana kuudanganya moyo, uwezo huo hanao.

naona umeamua kum-pre-empty prezidaa.
 
pamoja na ushindi kwa hakika mahanga amani hanayo moyoni, hata kama kuna tabasamu usoni. Maana kuudanganya moyo, uwezo huo hanao.

naona umeamua kum-pre-empty prezidaa.

Kuna msemo wanasema unaweza kudanganya nafsi za wengine lakini si nafsi yako. Hata mwizi hawezi kujiibia na akifanya hivyo jua ni mazoezi ya kuibia wengine.

Makongoro Mahanga nafsi yake itamsuta mpaka anaenda kaburini kama kweli alichakachua matokeo!!!!!!.
 
Kwan Baraza kuu limekubali Jakaya ndo Rais? Maana kama mnalalamika Bin Mrisho nae aliiba kura iweje mpeleke malalamiko ya mwizi wa kura za ubunge kwa mwizi wa Kura za Urais?
 
Kwan Baraza kuu limekubali Jakaya ndo Rais? Maana kama mnalalamika Bin Mrisho nae aliiba kura iweje mpeleke malalamiko ya mwizi wa kura za ubunge kwa mwizi wa Kura za Urais?

Mkuu hata kama aliiba lakini sheria za nchi hii haziruhusu kabisa kuhoji matokeo ya urais na kutuaminisha kwamba labda kweli alishinda kihalali.

Lakini la Makongoro lipo wazi sana, hivyo kwa kuwa lipo chini yake asilifumbie macho eti kwa sababu yeye aichakachua!!!!
 
Akimteua Mahanga na Aibu ya mhimili wa mahakama leo atajishushia hadhi..mwizi wa masanduku ya kura yule.
JK anajichafua? Lini alikuwa msafi? Huoni maamuzi ya mahakama yamepata influence yake? Makongoro ni wa kushinda kesi ya wazi ya wizi kama hakuna mkono wa mkulu? Basi subiri utaona kama hajapandishwa cheo na aliyemhukumu naye kupewa aidha ujaji mkuu au jaji kiongozi siku chache zijazo! Utaniambia nilisema!
 
Kwa maoni yangu akifanya hivyo atakuwa kafanya jambo la ajabu na hatakuwa na haya machoni pa wapigakura au watanzania kwa ujumla.

Situmaini kama ni mtazamo wa watu ndiyo ulitoa hukumu ya Mahanga kabla ya hukumu ya jaji.
 
Na hata alipokuwa anahojiwa baada ya kutangazwa mshindi alikuwa anaona haya kuwakabili watu machoni ila kiukweli nafsi inamsuta sana.
 
Na hata alipokuwa anahojiwa baada ya kutangazwa mshindi alikuwa anaona haya kuwakabili watu machoni ila kiukweli nafsi inamsuta sana.

Ni kweli kabisa. Ni kweli ukisikia miujiza ndiyo ile.
 
Kwan Baraza kuu limekubali Jakaya ndo Rais? Maana kama mnalalamika Bin Mrisho nae aliiba kura iweje mpeleke malalamiko ya mwizi wa kura za ubunge kwa mwizi wa Kura za Urais?

Hilo nalo neno! Nchi yenye mfumo hovyo hovyo!
 
Back
Top Bottom