Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,516
- 9,317
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejisalimisha kwa polisi ili kuanza kutumikia kifungo cha miezi 15 jela.
Wakfu wa Zuma Foundation uliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa kiongozi huyo ameamua kuheshimu agizo la korti na kwamba alikuwa njiani kuelekea katika kituo cha polisi cha wilaya ya Kwa Zulu-Natal.
Msemaji wa polisi Lirandzu Themba amethibitisha kuwa Zuma yuko chini ya ulinzi wa polisi baada ya kujisalimisha.
Dakika chache tu kabla ya muda wa mwisho aliyopewa na korti kujisalimisha kwa hiari kabla ya polisi kumkamata, Zuma aliondoka nyumbani kwake Nkandla akisindikizwa na msafara wa magari.