BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesimamishwa Uanachama wa chama Tawala cha African National Congress (ANC) akidaiwa kukataa kupiga Kura ndani ya Chama pamoja na kushiriki kuanzisha Chama Pinzani.
Imeelezwa kuwa Zuma aliyeliongoza Taifa hilo kwa miaka 9 na kujiuzulu baadaye kutokana na kashfa za Rushwa na kutoa upendeleo wa Tenda za Serikali kwa Wafanyabishara, hakuwahi kuchukuliwa hatua na chama hicho hadi alipotangaza kuunga mkono chama cha uMkhonto we Sizwe (MK).
Aidha, katika siku za karibuni, Zuma amedaiwa kuanzisha mashambulizi ya wazi kwa Rais Cyril Ramaphosa ambaye ni mrithi wake na aliwahi kuwa Makamu wake wa Rais. Wachambuzi wa Siasa nchini humo wamedai uamuzi wa Zuma kuunga mkono chama kingine unaweza kuigharimu ANC katika Uchaguzi.
=========
Mr Zuma, 81, had been a lifelong member of the ANC.
He joined aged 17 with no formal schooling and soon rose through the ranks of the ANC's military and intelligence wings, followed by top posts in his home state of Kwa-Zulu Natal and ultimately the deputy presidency and presidency.
Correspondents say this year's election is viewed by many as the most competitive since the ANC came to power in 1994.