Rais wa Tanzania na Kiingereza, wa Ujerumani na Kijerumani!

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Wakuu,
Katika dhifa ya kitaifa aliyondaliwa Rais wa Ujerumani, Jk kwanini hakuhutubia kwa Kiswahili chetu, ilihali mgeni wake kahutubia kikwao? Wapi kuthamini vya kwetu jama!
 
hhahaha mi mwenyewe nimeshangaa jk kapiga kingeli chake kaja mjerumani kapiga kijerumani ila tumeaibika
 
Wakuu,
Katika dhifa ya kitaifa aliyondaliwa Rais wa Ujerumani, Jk kwanini hakuhutubia kwa Kiswahili chetu, ilihali mgeni wake kahutubia kikwao? Wapi kuthamini vya kwetu jama!
Kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele.
 
Hilo ni tatizo Watanzania, hata katika makongamano mbalimbali tunapenda kujishaua na Kiingereza tena Kiingereza chenyewe kibovu. Utakuta wakati wa kufungua miradi yuko mgeni mmoja tu toka nje ya nchi na wasikilizaji wengi ni sisi Watanzania tena vijijini, unaona mwenyeji anaongea Kiingereza. Hii ni aibu.

Wakati majirani zetu nao hasa Kongo, Burundi, Rwanda na sasa Sudan Kusin wanajitahidi kujifunza na kuongea Kiswahili kwa maana kwamba wanaona umuhimu wa kutumia Kiswahili sisi tunang'ang'ania Kiingereza hata mahali ambapo hakuna ulazima wa kutumia Kiswahili.

Katika mikutano ya AU Kiswahili kimeingizwa kuwa moja ya lugha rasmi wakati wa mikutano,lakini sitashangaa kuSIKIA viongozi kutoka Afrika Mashariki wanahutubia kwa kutumia lugha ya Kiingereza. SHAME ON US.
 
Sijaona tatizo kuongea kiingereza. Tatizo ninaloliona ni sisi Watanzania kukariri kwamba kwasababu iki hivi basi inatakiwa kwenda hivi.
 
Ni aibu kwa wasomi wetu; wanaojinyanyapaa wenyewe na kujiona duni kwa kuzungumza kiswahili ambacho ni lugha ya taifa.
 
Nampongeza rais mstaafu wa Msumbiji Chisano, kujionea fahari kuhutubia kwa kiswahili; ambayo itakuwa ni lugha ya Afrika.
 
Wezetu lugha ni kwa ajiri ya biashara; nenda nchi zilizoendelea kila nchi ni kidume kwa lugha yake na ukijifanya unaongea Kiingerza chako, France,Italy,Germany, Netherlands hata China wezetu wanakuwa wanakuangalia tu.
Kiingereza ni USA & UK.
Tujifunze kukienzi Kiswahili tuwapo nyumbani na wageni wapate watafasili wao, Lugha ya mama ni lugha muhimu sana na mzungumzaji uwa na uhakika badala ya Kuongea kwa kutafasili maneno ya Kiswahili kwa kiingereza.. Hii ni aibu ....
 
Kwa ngazi ya uprofesa ni sahihi kuongea Kiingereza ili kuthibitisha ueledi wake.
 
Wakuu,
Katika dhifa ya kitaifa aliyondaliwa Rais wa Ujerumani, Jk kwanini hakuhutubia kwa Kiswahili chetu, ilihali mgeni wake kahutubia kikwao? Wapi kuthamini vya kwetu jama!

Kama unajisikia fahari na kikwenu msipeleke mabakuli ya kuomba msaada kwao!
 
Kiingereza kiko kwenye katiba pia, ni official language pale kinapotakiwa!
 
Sijaona tatizo kuongea kiingereza. Tatizo ninaloliona ni sisi Watanzania kukariri kwamba kwasababu iki hivi basi inatakiwa kwenda hivi.

Safi. Naunga mkono hoja. Kwani kuna ubaya gani kutumia kingereza!
Ni lugha ya kimataifa.
 
Mkuu ulishapata kibali cha kuishi nchini? Vipi ikitokea kwa sasa tukaamue urudi kwenu somalia utajisikiaje?

mi na vibali vya kuishi nchi 2.na ninaweza kwenda nchi yeyote bila kuomba visa ubalozi,kama mtu wa somali ana hizo sawa

wewe mahakama ya kadhi ndio uende somalia jina lako na ilo nchi vinaendana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom