john mapinduzi
Member
- Feb 25, 2009
- 99
- 17
Amali za taifa
Kwa ngazi ya uprofesa ni sahihi kuongea Kiingereza ili kuthibitisha ueledi wake.
Wakuu,
Katika dhifa ya kitaifa aliyondaliwa Rais wa Ujerumani, Jk kwanini hakuhutubia kwa Kiswahili chetu, ilihali mgeni wake kahutubia kikwao? Wapi kuthamini vya kwetu jama!
Hata katiba inayopendekezwa bado haijachapishwa na mpiga chapa wa serikali mpaka kwanza iandikwe kwa kingereza kisha itafsiriwe kwa kiswahili!
Sijaona tatizo kuongea kiingereza. Tatizo ninaloliona ni sisi Watanzania kukariri kwamba kwasababu iki hivi basi inatakiwa kwenda hivi.
Ni shida ya huyo mjerumani kutokujua kingereza. Sasa mjerumani mzima hata kingereza hajui anakuja kuongea kijerumani chake.
Sijaona tatizo kuongea kiingereza. Tatizo ninaloliona ni sisi Watanzania kukariri kwamba kwasababu iki hivi basi inatakiwa kwenda hivi.
Nakumbuka alikuja Rais wa china aliongea kichina lakini rais aliongea kingereza ni aibu sana. Jiulize watu wangap wanajua kichina kulinganisha n kiswahil dunian tunapuuzia tunafikir ni vitu vidogo hiv ni vitu vya muhim sana kama taifa tatizo hatuna dira tupotupo tuu. kama mgeni ni Muingereza angeongea 'kingereza chake lakini kwa jana angeongea kiswahili hata kama ni maskini inaonyesha unajithamini na kujiamini hata wenyewe wanapenda tujidhamini na tutaheshimika
Mkuu mwache aongee tu kijerumani chake maana kimempa mafanikio makubwa tangu enzi izo na kama kuendelea walishaendelea wenzetu tangu miaka iyo wewe unaeongea icho kiingereza umepata maendeleo gani mana hata kutengeneza sindano atuwezi kazi kulalamika njaa tu na kukinga vibakuli kuomba misaada.
Jambo hili la kung'ang'ania kiingereza na kukiacha kiswahili, ni jambo analolipenda sana raisKikwete sijui kwa nini. Alipokuja rais wa china, kikwete alihutubia kwa kiingereza pia.Wakuu,
Katika dhifa ya kitaifa aliyondaliwa Rais wa Ujerumani, Jk kwanini hakuhutubia kwa Kiswahili chetu, ilihali mgeni wake kahutubia kikwao? Wapi kuthamini vya kwetu jama!