Rais wa Niger na Wabunge washikiliwa na Jeshi

Mwe !!! Mfano wa kuigwa na nani ??? Hivi wewe unaujua mtutu wa bunduki au unausikia tu ??? Usifanye mchezo na mapinduzi ya kijeshi. Kama umechoka amani basi hamia huko huko Niger au uende hapa jirani tu na kwetu uone madhara ya umwagaji damu. Nadhani wewe siyo m-TZ, labda unatokea huko huko wanakomwaga damu. Usituletee huo muflisi wako wa amani na siasa. KWENDA ZAKO HUKO.

Hakika wewe ni Mzee kibiongo, hata ufahamu wako una kibiongo. Palipo amani (ya kizushi) pana uharibifu mwingi....kama ilivyo Tanzania. isome taarifa kabla ya kucomment ...The situation in Niamey remains unclear - there has apparently been no large-scale deployment of military personnel.
Watu kama wewe ndio huwa mnaonyeshwa picha za kimbari wakati wa uchaguzi mnaambiwa vyama vya upinzani vitaleta mauaji kama hayo na mnaamini.

Wake up!!!!!!!

Watawala wamewageuza wa-tz matambara ya deck, na hulioni hilo.
 
SOURCE:http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/8523196.stm

..............Supreme Council for the Restoration of Democracy (CSRD), the
..... the spokesman for the coup leaders, wearing a military uniform, was surrounded by a large group of soldiers.
He called on the people of Niger to "remain calm and stay united around the ideals postulated by the CSRD", to "make Niger an example of democracy and good governance".
"We call on national and international opinions to support us in our patriotic action to save Niger and its population from poverty, deception and corruption," he added.

The situation in Niamey remains unclear - there has apparently been no large-scale deployment of military personnel.

I like the highlighted part. I pray and hope that they have good motive for their country.
 
Unajua mapinduzi ya nguvu siku zote ni mabaya lakini kuna wakati ni lazima itokee fujo ili kuweza kuweka mambo sawa. Mapinduzi ya Zanzibar 1964 ni mfano mmojawapo. Na haya ya Niger naweza kusema ni muhimu. Huyu Rais Tadja amebadilisha katika kwa nguvu na ulaghai mkubwa ili kuendelea kuhodhi madaraka. Dunia nzima na upinzani wamepiga kelele lakini wapi. Katika hali hiyo ni kheri kuvunja ili kuanza upya. Wanajeshi ndio wasusiwe ila baada ya hapo hakuna kiongozi wa Niger atachezea katiba kama alivyofanya Tadja.
 
Hold on,Sasa hawa wanafiki wakuu wa nchi na serikali za nchi wanachama wa AU walipotoa azimio kwamba hawatambui mapinduzi ya kijeshi hapa watasema nini coz Jamaa alibadilisha katiba ili agpmbee third term..Sasa mimi naunga mkono walichofanya wanajeshi,hao ni wazalendo na wanamapinduzi tunaowataka Africa.

Pia,kuna uwezekano hapo kuna mkono wa magharibi pia hasa kama jamaa anawauzia iran uranium.pia kuchezea constution ni against democratic ethics.So kama wanajeshi nao wamepewa support na America basi hili nalikataa coz still tunakaribisha makucha ya imperialism Africa.Sitaki any revolutionary move yenye external influence
 
Hakika wewe ni Mzee kibiongo, hata ufahamu wako una kibiongo. Palipo amani (ya kizushi) pana uharibifu mwingi....kama ilivyo Tanzania. isome taarifa kabla ya kucomment ...The situation in Niamey remains unclear - there has apparently been no large-scale deployment of military personnel.
Watu kama wewe ndio huwa mnaonyeshwa picha za kimbari wakati wa uchaguzi mnaambiwa vyama vya upinzani vitaleta mauaji kama hayo na mnaamini.

Wake up!!!!!!!

Watawala wamewageuza wa-tz matambara ya deck, na hulioni hilo.

Haya, anza wewe sasa. Nakuuliza unaujua mtutu wa bunduki ? Fighthing is the most primitive way of solving problems. Umeyasikia ya Musoma ????
 
Haya, anza wewe sasa. Nakuuliza unaujua mtutu wa bunduki ? Fighthing is the most primitive way of solving problems. Umeyasikia ya Musoma ????

yaani unafananisha yaliyotokea Musoma na masuala ya katiba + siasa????
arghhhhh!!!!?????????
Pole sana
 
UOGA WENU NDO UMASKINI WENU,UKOMBOZI HUJA KWA DAMU KUMWAGIKA,PASIPO MWAGIKA DAMU PANA UONEZI MKUBWA...Tanzania ni mfano mzuri wa namna ambavyo pasipo mwagika damu panachezewa.Hebu angalia Burundi,Ruanda nk Sehemu ambapo watu walimwaga Damu angalau sasa wanaheshimiana
 
Unajua mapinduzi ya nguvu siku zote ni mabaya lakini kuna wakati ni lazima itokee fujo ili kuweza kuweka mambo sawa. Mapinduzi ya Zanzibar 1964 ni mfano mmojawapo. Na haya ya Niger naweza kusema ni muhimu. Huyu Rais Tadja amebadilisha katika kwa nguvu na ulaghai mkubwa ili kuendelea kuhodhi madaraka. Dunia nzima na upinzani wamepiga kelele lakini wapi. Katika hali hiyo ni kheri kuvunja ili kuanza upya. Wanajeshi ndio wasusiwe ila baada ya hapo hakuna kiongozi wa Niger atachezea katiba kama alivyofanya Tadja.

Viongozi wa nchi wanapojisahau na kuwafanya wananchi wanaowaongoza wajinga matokeo yake ni hayo. Huwezi kuwa mtawala wa mamilioni ya watu halafu ukafanya rasilimali za nchi kama mali yako wewe na rafiki zako; wanajeshi mara nyingi wanachukua nafasi kama hizi kufanya vitu vyao!! Inatokea mara nyingi wanaofanya mapinduzi sio viongozi wakuu wa majeshi bali hao wa kati na chini!!
 
Africa ipo kaazi kweli kweli.

Kenya Waziri anafukuza waziri. Niger jeshi lashikiria viongozi. Nigeria Rias kitandani takribani mwaka sasa. Bongo tambarare.

tena tambarare yenye utelezi, lakini mwungwana wala hajali, mradi jua linachomoza na linazama, mitaani watu hawaandamani. kwake bizinesi as usual.
 
dah, wanajeshi hawa koboko wanataka nini hasa

hapa kwetu tambarale
 
Huyu jamaa anastahili maana alijisahau. Franco Phone countries bwana! Ufaransa inachofanya inahakikisha kila Rais wa zilizokuwa koloni zake anakuwa recruited in France masonic lodges na baada ya hapo wanahakikisha wanamlea kiasi kwamba hata kama atawaua watu wake wote hawajari ili mradi tu anaonyesha mapenzi kwa Ufaransa.
Rwanda walichoamua nakiunga mkono kabisa. Wafaransa wanaziharibu nci walizozitawala Afrika kwa kuweka marais wasiojari kabisa demokrasia.

Bwana Ndahani tatizo siyo wafaransa wala wakoloni kama unavyojaribu kusema. Tatizo ni sisi waafrika yaani watawala wetu na sisi watawaliwa tunaokubali kutumiwa na wageni kwa manufaa yetu binafsi na yao bila kujali mustakabali wa nchi zetu.

Na nchi zetu haziwezi kupiga hatua kimaendeleo kama kila tatizo tutatafuta visingizio na kulaumu wengine mara utumwa, ukoloni, wafaransa, waingereza, wamarekani, mara wachina, utandawazi, mapenzi ya mwenyezi mungu na blah blah nyingine nyingi.

Na wala siyo nchi za Franco phone pekee zenye matatizo haya hata huku kwetu mashariki tuna matatizo hayo na wala hatukutawaliwa na wafaransa.

Maendeleo ya Africa na ya Tanzania yataletwa na waafrika wenyewe. Kila mwafrika na hasa wazalendo wa afrika.
 
Tatizo la nchi za Kiafrica, utajiri wa rasilimali unaleta laana. Viongozi wananunuliwa na multinationals kwa hongo kidogo tu kwa sababu ya ubinafsi wao wanaacha wananchi wakiteseka. Mamadou kaonja utamu wa uranium hataki tena kuondoka.

Acha apinduliwe.
 
hiyo ndio krokwini ya ugonjwa huo wa kupenda madaraka safi sanaaaaaaaaaaaa wanajeshi...
icon10.gif
 
Taht is what they deserve all who temper with the constitution to become life president. Ni october mwaka jana alibadili katiba ili aendelee kutawala wakati muda wake umeisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom