Rais wa Malawi auza ndege ya rais na magari 60 ya kifahari..je ni mtego kisiasa?

amethubutu, ameweza, anasonga mbele...she is walking the talk wakati hapa kwetu they are simply talking the talk!

hawana uthubutu wala uwezo, sana wakizidiwa huangua vilio hadi bungeni...what a shame, kama mtoto kanyimwa pipi au kakataliwa safari ya kwenda beach kutembea.
 
Mshahara wa JK , Pinda na Bilal ni zaidi ya wa Obama na Makamu wake Joe Biden kwa mwaka kwa mujibu wa Zitto Kabwe.
 
SI KWAMBA SERIKALI HAIJUI KUWA KUNUNUA, KULIHUDUMIA TOYOTA LAND CRUISER v8(na yote yanayofanana na hayo) NI GHARAMA KUBWA bali ni ulaji wa baadhi ya watu maana kama watu wanapata 10% kwa nini asipigie debe? jamani tujifunze kwa wenzetu wa-RWANDA na KENYA wao waziri hatembelei STATION WAGON ni VOLKSWAGEN PASSAT(saloon car). Kwa staili hii tunatengeneza taifa/kizazi wasiojua umuhimu wa kubana matumizi. La muhimu apatikane kiongozi kama Joyce Banda na kuamua. Waziri Mkuu wa Norway akisafiri kwenda popote duniani hupanda ndege za Abiria ingawa ni 1st Class hapa kwetu Prof. Mukandala wa UDSM (mfano mmojawapo) hata akienda MWANZA/BUKOBA lazima apande 1st Class tena kwa gharama za chuo/serikali? tutafika? Tena siku hizi kuna mchezo wanacheza dereva wa LAND CRUISER anatangulia na gari kama ni Mwanza toka Dar then kesho yake Mkuu anapanda ndege anamkuta dereva anamsubiri Airport. WHAT A SHAME WATANZANIA?

Hata kama Mama Rais Banda wa Malawi anatumia ni mbinu ya kisiasa ya yeye kuchaguliwa kwenye uchaguzi ujao mi binasi naona ni mbinu nzuri kuwafanya wanachi kuamini kuwa unawajali kuliko Anasa za magari ya kifahari

Unapozungumzia Rwanda kutumia hizo gari ni saw a siyo Rwanda tu hata Zanzibar v8 ni za kuhesabu ila kwa nchi kubwa kama tz ni ngumu hebu imagine kiongozi atoke dar hadi kagera kwa saloon au escudo kweli inawezekana na kama ww ni mtu unayeyajua magari gari hiyo inaweza kudumu kwa muda gani,tusiwe tu watu wakulalamika kwa vitu ambayo hatujui undani wake,tafakari kwanza kabla ya kupost chochote
 
Mkuu naomba mfano japo mmoja kwa kwa yale unayo mlani.

RED: Nadhani ulimaanisha mlaani... Umeniomba sababu moja ila kwa leo nakupa tatu.

1. kitendo cha kuwadanganya wananchi wake kuwa Ziwa Nyasa lote ni la Malawi... ,

2. Kuwadanganya wananchi wake hasa vijana kuwa amewatafutia nafazi za kazi 10,000 huko Korea ya Kusini wakati akijua hakuna mkataba wowote aliokuwa ameingia na Wakorea.

Malawi gov

3. Kujiingiza kwenye kundi la walokole wakati hawezi kushi kama mlokole wa kweli.

Malawi Pres.Banda says ‘I worship at Prophet T.B. Joshua as a follower of God
 
Maigizo tu. Hata sie tuliuza nyumba kwa bei chee na sasa tunajenga kifisadi huku tunapangisha mahoteli kwa bei za miujiza. Kenya nao waliuzaga magari makubwa kwa bei chee na kununua benzi za hatari kwa same prices.

Siasa tu hizo ila maumivu lazma yawepo kwa maskini
 
Rais wa Malawi..Bi Joyce Banda ambaye ni mwanamke wa pili Afrika kuwa rais, ameipiga mnada ndege ya serikali iliyokuwa ikitumiwa na rais aliyemtangulia marehemu Bingu wa Mutharika.

Pia ameyapiga mnada magari 60 ya kifahari aina ya MERCEDEZ BENZ ili ipatikane pesa ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo madawa ya hospital, huduma ya maji, elimu, mishahara madaktari na wahudumu wengine serikalini.

Unauonaje uamuzi wake?

Haya ndio Mambo ya msingi, sio kupigia debe ushoga. Now u r wth me prezidaa.
 
Bi. Banda anastahili kupongezwa uamuzi wake ni mzuri na unaonyesha jinsi alivyoweka mbele maslahi ya wananchi wake wa Malawi.
 
The $15 million raised from last year’s sale of a luxury Malawi presidential jet fed the poor and bought military equipment, the President said on Wednesday amid allegations it may have been embezzled.

“It was me who said let’s sell the jet and the Cabinet agreed three things to benefit Malawi...to buy maize, buy military equipment such as patrol boats and pay for peacekeeping mission in the DRC,” President Joyce Banda said.

Malawi has contributed soldiers to the 3,000-strong UN intervention brigade authorized to go after armed groups ravaging DR Congo.
 
Kwa nini haikuwa elimu na afya kama sio barabara!!!!?????
Ni kuondoa ndege na kuimarisha jeshi ili akae vema!!!!!!

Eti na mahindi nayo yanahesabiwa ili wananchi waone nao wametumia!!!!
Afrika kama hatujalaaniwa sijui
 
kwa nini haikuwa elimu na afya kama sio barabara!!!!?????
Ni kuondoa ndege na kuimarisha jeshi ili akae vema!!!!!!

Eti na mahindi nayo yanahesabiwa ili wananchi waone nao wametumia!!!!
Afrika kama hatujalaaniwa sijui
kama sijakuelewa vile
 
Kwa nini haikuwa elimu na afya kama sio barabara!!!!?????
Ni kuondoa ndege na kuimarisha jeshi ili akae vema!!!!!!

Eti na mahindi nayo yanahesabiwa ili wananchi waone nao wametumia!!!!
Afrika kama hatujalaaniwa sijui

atleast wamezitumia pesa kwa busara ya kuridhisha.sipati picha hawa majambazi wetu huku tanzania wangezitumiaje.
 
atleast wamezitumia pesa kwa busara ya kuridhisha.sipati picha hawa majambazi wetu huku tanzania wangezitumiaje.

Busara ipi na ya kumridhisha nani!!!!????
Wewe ungekuwa kwenye timu ya planning ungefikia uamuzi huo??????
 
ameuza ndege amenunua vifaa vya kijeshi ikiwemo boti ya kisasa na kulipia wanajeshi walioko kongo na kununua chakula
Hapo jambo la maana alilofanya ni kununua chakula lakini ningemsapoti kama angenunua matrekta,mbolea na zana nyingine ili malawi waweze kuzalisha chakula kumbuka Malawi walishafanya hivyo na wakapata chakula cha kutosha
Majeshi ya malawi yaliyoko Kongo yanalipiwa na UN sio kweli pesa zinatoka kwa nchi husika hapo ni propaganda za kisiasa patrol boat ni kwa ajili ya kujiimarisha kutokana na hali tete ya usalama iliyoko zaiwa nyasa ingawa kwa hali halisi ni ngumu kupigana vita .matumizi pekee ya maana aliyofanya ni kununua chakula mengine ni uongo na ujinga ambao wanao viongozi wengi kutumia matumizi makubwa ya kijeshi wakati mazingira hayaruhusu
 
Big up Bi Joyce, wenye macho na wapenda nchi zao watakuiga uyafanyalo. Sisi watanzania tunasikitishwa na kikwete, Ocd anatembelea shangingi la million 200, mkuu wa wilaya million 200, Mkurugezi wa halmashauri milion 200, Afisa elimu wa wilaya million 200, viongozi wote wa taasisi wilayani hivyo hivyo. Mkoani hali kadhalika hivyo hivyo, Rais mpaka katibu mkuu wa wizara hivyo hivyo! Nchi inadaiwa deni la trion 22, inaongoza kwa kukopa na kupewa misaada, Je? Tutafika ? HAPANA! Kikwete unatupeleka pabaya na Pinda wako mnafiki.

Unafikiri haya yote hawayajui? Wameweka pamba wasikioni anaula nchi kwa mrija.
 
Unapozungumzia Rwanda kutumia hizo gari ni saw a siyo Rwanda tu hata Zanzibar v8 ni za kuhesabu ila kwa nchi kubwa kama tz ni ngumu hebu imagine kiongozi atoke dar hadi kagera kwa saloon au escudo kweli inawezekana na kama ww ni mtu unayeyajua magari gari hiyo inaweza kudumu kwa muda gani,tusiwe tu watu wakulalamika kwa vitu ambayo hatujui undani wake,tafakari kwanza kabla ya kupost chochote

Wewe ndiye unajichanganya mkuu wangu! Wanaopinga hawajasema hizi gari zisizinunuliwe kabisa bali zinunuliwe chache kwa madhumuni ya safari ndefu ambazo hakuna uwezekano wa usafiri mbadala!

Sasa hizi gari zimejazana mijini zikiwabeba maafisa wa Serikali kutoka Oysterbay,Masaki,Mikocheni na maeneo kama hayo kwenda maofisini. Ni matumizi mazuri fedha za wananchi? Kwanini huku wasinunuliwe magari madogo hata mabasi madogo kwenda na kutoka Ofisini maeneo ya Mijini?
 
Back
Top Bottom