Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf atembelea Tanzania

Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
596
Kwa taarifa,

Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, anawasili nchini leo mchana mida ya saa nane hivi. Atapokelewa na JK (mwenyeji wake na kuelekea "White House", katika dhifa iliyoandaliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Kesho atahutubia pale UDSM, "The Role Of Women In Africa Development" (Majukumu ya Wanawake katika Maendeleo ya Afrika)

Keshokutwa atakuwa Arusha, akitembelea kiwanda cha vyandarua katika kiwanda cha A to Z

Ziara yake ni ya kiserikali (Kikazi).

:behindsofa:
 
Kweli huyu mama ni msafi? Aliwahi tuhumiwa kuingia madarakani kwa mlungura lakini karibu nchini. Uje ujifunze mwongozo,taarifa mh. mwenyekiti.
 
Kwa taarifa,

Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, anawasili nchini leo mchana mida ya saa nane hivi. Atapokelewa na JK (mwenyeji wake na kuelekea "White House", katika dhifa iliyoandaliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Kesho atahutubia pale UDSM, "The Role Of Women In Africa Development" (Majukumu ya Wanawake katika Maendeleo ya Afrika)

Keshokutwa atakuwa Arusha, akitembelea kiwanda cha vyandarua katika kiwanda cha A to Z

Ziara yake ni ya kiserikali (Kikazi).

:behindsofa:

Yaani hat kuweka heading tu mgogoro? kweli hivi vyuo vitatuletea majanga nchini
 
Johson mwenyewe anatuhumiwa na chama chake tawala kuwa anawapa ndugu zake nafasi za upendeleo katika serikali yake
 
Niambie tatizo la hiyo "heading"...kuna aina nyingi za uandishi, na kama kweli umeona Tanzania hakuna vyuo basi ni bora kusoma headings za magazeti au kusikiliza vyombo vingine vya habari....hebu twende katika mdahalo kwa undani zaidi kuhusu hili,. Kwa mtazamo wako, ungependelea heading iweje?
 
...hebu twende katika mdahalo kwa undani zaidi kuhusu hili,. Kwa mtazamo wako, ungependelea heading iweje?

Unaweza kuandika Rais wa Liberia "aja" Tanzania

Kwa sababu kurudi inamaana kama ile uliyoieleza kuwa lazima iwe aliwahi kuwapo kwa wakati fulani. Sasa ingekuwa kwa mfano amewahi kuishi Tanzania, au amewahi kutoa lecture ama kusoma UDSM ndio "arudi" ingekuwa mwake

Vyenginevyo aja (yuwaja), kutembelea, kuzuru, kutua, kuwasili.....yangefaaa zaidi.
 
mpe somo huyo,na hawa ndo walimu wanaotufelishia watoto zetu kwa "ujuha" wao.
 
Nafurahi kwa sababu wewe ni mmoja wa watu makini..........tatizo hapo nini? "ARUDI" nilichomaanisha ni taarifa ya nini kinachoendelea, ila mimi sio mwalimu wa KISWAHILI kama wewe kwani mimi pia ni mwanafunzi wa lugha hii adhimu........Kukosoa kwako ni kuzuri sana, napenda wakosoaji kwani hao ndio "pushing factor" ya ukuaji wa lugha yoyote duniani. Nashukuru kwa mchango wako ndugu Shekispia.
 
Ndugu yangu Gaijin, asante kwa mchango mzuri wenye kuendelea kutufundisha lugha hii ya kiswahili. Hapo nimekuelewa vizuri
 
Kwa sasa Rais huyo wa Liberia, Mama Ellen Johnson-Sirleaf yuko Arusha
 
Alitua jana JNIA,mida ya saa 8,kukawa na kero maana kiwanja kilifungwa eti VIP analand!!!
Leo police na mizinga yao, walikuwa wamejipanga KIA kumsubiri huyu mama!
 
Unaweza kuandika Rais wa Liberia "aja" Tanzania

Kwa sababu kurudi inamaana kama ile uliyoieleza kuwa lazima iwe aliwahi kuwapo kwa wakati fulani. Sasa ingekuwa kwa mfano amewahi kuishi Tanzania, au amewahi kutoa lecture ama kusoma UDSM ndio "arudi" ingekuwa mwake

Vyenginevyo aja (yuwaja), kutembelea, kuzuru, kutua, kuwasili.....yangefaaa zaidi.
Haswaaaa. hata mimi sikukielewa kichwa cha habari nikadhani huyu mama amewahi kuishi hapa hivyo amerudi. Kabila alivyochukua mamlaka ilikiwa sahihi kusema Kabila Arudi Tanzania. Hapa ilikuwa na maana kuwa alikuwepo na sasa anarudi lakini kurudi kwake ni kivingine akiwa sasa ana mamlaka.
 
Back
Top Bottom