Rais wa 2015 - Watanzania fungueni macho, masikio na akili zenu

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Vyama vya siasa ndivyo vyenye fursa kubwa ya kututeulia wagombea wa Uraisi kwa mwaka 2015 hata katiba ikibadili na kuongeza mgombea binafsi hakuna jinsi mgombea binafsi anaweza kushinda kwenye siasa za kama za bongo zinazohitaji mtaji mkubwa wa watu, fedha nyingi na mtandao mzuri.

Ili kupata Raisi bora lazima kupata wagombea bora, wenye akili, maona, uchungu, ubunifu, weledi, wasio na kashfa, tamaa ya uongozi, wenye hekima na busara na wanao Muogopa Mungu kutoka moyoni na Rohoni. Lazima wapatikane wagombea ambao watairudisha Tanzania inayoheshimiana, vumiliana na kuwafanya watanzania wote waishi kwa amani bila dini, makabila, rangi, kanda zao kutumiwa kama vigezo vya kukubalika ndani ya nchi yao.

Tanzania lazima iwe na raisi ambaye atayaona makosa na uvunjifu wa sheria kama kosa na wala si kama kosa la kitaasisi ama wa kisiasa, kidini, kiitikadi au mrengo wowote ule. Wote wenye kuvunja sheria bila kujali vyeo, ukwasi, dini na kabila zao wanafikishwa mbele ya sheria.

Raisi ambaye atazingatia ustawi mpana wa Tanzania kiuchumi, kijamii na kujali rsilimali zetu kwa faida ya wote na wajukuu wetu kwa vizazi vijavyo na vijavyo.

Raisi amabye atatambua Watanzania wanapendana sana na ni ndugu, ila umasikini, ukosefu wa ajira, elimu mbovu na ukosefu wa elimu kwa walio wengi hasa wale wa vijijini na familia masikini ambao ndio walio wengi kunatengeneza matabaka ambayo yatatuletea balaa usoni.

Pampja na mengi ambayo siwezi kumaliza kuandika. Mgombea huyu ambaye lazima atokee kwenye chama kimojawapo cha siasa lazima tuwe makini.

Kila mwanachama mwenye mapenzi mema na Taifa hili arudi nyuma atafakari kwa kina. Arudi ndani ya chama chake akijua kwamba mgombea wake wa uraisi ndani ya chama chake anaweza kuwa Raisi wetu wote, watoto wake, wajomba , binamu na wajukuu zake ajiulize kabla hajaanza kumpigia kampeni ndani ya chama chake, je kweli huyu anaweza kuwaachia watoto wangu na wajukuu Tanzania yenye neema na amani au ni mroho tu wa kwenda Ikulu??

Vyama vya siasa lazima vijue 2015 ndivyo vinatuletea Rais ambaye atafuta makovu yetu kwa miaka 30 ya kukosa utawala, kukosa Raisi kama taasisi na kukosa kiongozi mkuu wa nchi kwa miaka 30.

Ushabiki uwachwe kabisa ndani ya teuzi za vyama kwani wagombea wao mmoja wapo ndiye atakuwa Raisi wetu. Sitaki kusikia watu wakijuta, sitaki kusikia watu wakilia tusije jikuta tuna viongozi wasiofaa wala elewa kazi zao achilia mbali wasio soma hotuba na mikataba kabla ya kusini na kuhutubia.

Tanzania itajengwa na sisi wenyewe tuliowakabidhi wamelewa lubisi.

Chief Mkwawa wa Kalenga
Revolutions is important if democracy failed
 
Nadhani rais ajaye itabidi awe Mkapa kupitia chama kingine cha siasa,maana vyama vilivyopo vimefilisika sera,vinginevyo bora jeshi litengeneze nchi kwanza.
 
Nadhani rais ajaye itabidi awe Mkapa kupitia chama kingine cha siasa,maana vyama vilivyopo vimefilisika sera,vinginevyo bora jeshi litengeneze nchi kwanza.

umekata tamaa mno na hii ni kwasababu matumaini yako uliweka kwa ccm. revive your hopes, there is an alternative party to take us through this wave of irresponsible government.CHADEMA BE YOUR CHOICE.
 
Kukata tamaa ni woga mbaya sana.Hebu kumbuka ulidhani Mkapa angeweza ku-make it 1995 na jinsi alivyosaidia kiunua uchumi wa watanzania na sio takwimu za uchumi wa Tanzania?Watu wapo tatizo ni chaguo sahihi
 
mimi nadhani ili kuepuka fitina na kuyakomesha makundi,tukodi raisi mstahafu kutoka nchi nyingine.mfano tunaweza kumkodi clinton.
 
Back
Top Bottom