Rais uwachunguze vizuri hawa wawekezaji wa Kampuni ya Tanzanite One Mining, kabla ya kusaini nao mkataba mpya

mgodi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,780
1,845
c5b1648fc8c8a9ba6a9fde4b38491f79.jpg


Naomba nianze kwa kumpongeza mh Raisi wetu Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi kubwa anayofanya ya kuhakikisha madini tuliyonayo hapa Nchini kwetu, yanawanufaisha Watanzania wote.
Lakini pia nimuombe mh Raisi, ajaribu kuangalia tena timu yake. Naamini bado kuna watendaji katika timu yake, wanamkwamisha mh Raisi kupata taarifa sahihi. Kama alivyosema ile siku anamuapisha mh Naibu Waziri wa pili wa madini, mh Dotto Biteko. Mh Raisi alisema, watendaji wangu nadhani hawajui nini nahitaji katika hii wizara.

Katika hili sakata la kusaini sheria + kanuni mpya na kampuni hii ambayo imeshaonyesha vigezo vyote vya kushindwa kujiendesha yenyewe. Tokea mwezi 11/2017 hadi sasa Januari 2018, hawajaweza kulipa mishahara ya wafanyakazi wote, kisa hana pesa.

Kwa sasa hakuna kazi zinazoendelea pale kampuni, wafanyakazi wa mgodini wanaenda kufanya tu usafi, na kuondoka. Vyakula vya wafanyakazi hakuna, zaidi ya ugali mahalage. Kampuni inamadeni kila sehemu, Tanesco walikata umeme kutokana na deni kuwa kubwa, ila ukarudishwa kwa msaada wa mkuu wa Wilaya.

Mengine siwezi eleza sana, najua kuna idara husika zinaendelea na kazi ya upelelezi. Ushauri wangu kwako, kama unampango wa kusaini nao tena mkataba na Tanzanite One ( Sky Associate), nakuomba mh Raisi wachunguze vizuri tena hawa watu. Pia kama ni Wazawa, jaribu kutumia shirika kama NSSF wawekeze kama wazawa, kwa kushirikiana na Mwekezaji toka Nje ya Nchi yetu, maana uwekezaji wa Migodi unahitaji wataalamu + mtaji wa uhakika, siyo hawa wanaobahatisha kila kukicha.

Nauhakika hata ukichunguza akaunti ya kampuni, sijui kama utakuta pesa ya Kitanzania 500m kwa sasa.

Wako katika kujenga Taifa.

819ec8bee7d14ea495b27ec8f89f7889.jpg

a0cc57b78eacf6c5f186b7a4a379bc37.jpg

Hapo ni wafanyakazi wakijaribu kuulizia hatima ya mishahara yao, lakini jibu linalotolewa ni kampuni haina pesa.
 
Wazungu wote ni wezi kwa kupitia mikataba hasa ya kichifu Mangungo.

Tunapaswa kujifunza, kwa makosa ya hapo awali kisha tufanye nao kazi kwa akili hasa kujitambua kuwa wazungu na wawekezaji kwa ujumla wanajiangalia wao tu na siyo wewe, Serikali , wananchi wala nani.

Mikataba iwe wazi na siyo kutiliana sahihi usiku wa manane kwenye vungu za vitanda na meza za mahotelini.
 
Wazungu wote ni wezi kwa kupitia mikataba hasa ya kichifu Mangungo.

Tunapaswa kujifunza, kwa makosa ya hapo awali kisha tufanye nao kazi kwa akili hasa kujitambua kuwa wazungu na wawekezaji kwa ujumla wanajiangalia wao tu na siyo wewe, Serikali , wananchi wala nani.

Mikataba iwe wazi na siyo kutiliana sahihi usiku wa manane kwenye vungu za vitanda na meza za mahotelini.
Ni kweli, mikataba kuwa wazi ingependeza zaidi
 
Back
Top Bottom