Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,447
- 2,838
Wakuu inakuaje? sasa twende kazi.
Siku mbili tatu hizi kumekuwa na hali ya sintofahamu kati ya serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ile ya Rwanda, kila mmoja akimtupia lawama mwenzake na kutishia kuvunjilia mbali uhusiano wao wa kidiplomasia nk.
Kwa upande wa Congo ndio wanaonekana kuwa wamechukia zaidi hadi kupelekea serikali yao kumfukuza nchini kwao balozi wa Rwanda, na pia kumwata balozi wao aliekuwa nchini Rwanda.
Kwa upande wa Rwanda yenyewe haioneshi kupanic wala kuchukizwa kivile, inaonekana ime relax ikisubiria kuona kingine kitachojiri kutoka katika serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Sasa basi... Rwanda ina uwezo wa kuichakaza na kuisambaratisha Congo kijeshi kwa njia zote, iwe kwa angani, majini au ardhini tena kwa muda mfupi sana.
Congo inaweza kuishinda Rwanda kwa maneno tu, maana wakongomani ni waimba miziki na wachezaji wakubwa, ila linapokuja swala la mapambano ya kijeshi na weupe sana wanashindwa hata na Burundi.
Kwanza toka Congo ilipopata uhuru jeshi lake halikuwahi kushinda vita yoyote ile. Wakati wa Mobutu jeshi la Congo lilichakazwa vibaya na waasi waliokuwa wanaongozwa na hayati Desire Kabila (father) na baadae jeshi hilo limeendelea kuchakazwa na makundi mbali mbali ya waasi wengi wao ni kutoka nchi jirani.
Sasa jiulize ikiwa nchi yenye raia zaidi ya milioni 1 inachakazwa na waasi wasiozidi elfu 5, huku waasi hao wakiwa na silaha za kuunga unga na mazoezi ya msituni yasiokuwa rasmi. Je watakapoingia kwenye vita na nchi yenyewe si ndo yatakuja kutokea yale ya Mobutu na Idi Amini!!
Hivi kweli Tshisekedi anaamini kuwa nchi yake inaweza kuipiga Rwanda au ndo kifo kinamwita, au wazee wa kazi (Kabila's team) wanamshauri ujinga ili akipigwa akikimbia Kabila arudi kuongoza Congo?
Maana katika hali ya kawaida haiwezekani nchi inayoshindwa vita na waasi elfu 3, ijidanganye kuwa inaweza kupambana na nchi yenye wanajeshi zaidi ya laki, wenye ueledi mkubwa wa kivita, silaha za kisasa na wanajeshi wa kutosha.
Katika EAC nzima, nchi ambazo Rwanda inaweza kuhofia kwa namna fulani kupambana nazo ni Tanzania na Kenya tu ambazo majeshi yao yameshafanya mambo makubwa ndani na nje ya mipaka yao Tanzania ikiwa inaongoza kwa kufanikiwa oparation mbali mbali katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Comoros nk. Ila hizo zingine Rwanda inaziona kama vile ni nchi zinazolindwa na makundi ya sungu sungu tu na sio wanajeshi kamili.
So chonde chonde Tshisekedi watu bado wanakuhitaji uendelee kuwa raisi wao. Usije kuingia kwenye mtego ambao utashindwa kujinasua. Kagame alimhofia Kikwete tu mjeshi mwenzake na anajua watu wa kicheka cheka kama JK maamuzi yao yanakuwaga na athari kubwa kwa wengine. Lakini nyinyi wengine anawaona vikaragosi wake.
Tena kwa Congo ndo kabisa hawezi kutuma jeshi lake kupoteza muda wao. Sana sana ataajiri vijana kutoka katika makampuni mbali mbali ya ulinzi waje kumaliza kazi.
Pichani juu ni jeshi la Rwanda na picha ya chini ni jeshi la Congo.
Siku njema kwa wasomaji na wachangiaji wote. Asanteni.