Rais Tshisekedi azua jambo, waziri mkuu agoma kujiuzulu

Juuchini

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
1,300
1,659
KINASHASA, DRC

LICHA ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupiga kura na kumchagua rais mpya katika uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 23, mwaka jana, bado nchi hiyo imeendelea kubakia bila Serikali ikiwa ni wiki nne sasa tangu Felix Tshisekedi, alipoapishwa kuliongoza taifa hilo.

Mawaziri mbalimbali wa Serikali iliyokuwepo wameanza kujiuzulu mmoja baada ya mwingine, huku hatima ya Serikali mpya ikiwa bado haijajulikana.

Duru za kisiasa zinasema kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi, ameshindwa kuunda Serikali kutokana na mgawanyiko unaoikumba jamii ya wanasiasa nchini humo.

Wakati huo huo Waziri Mkuu, Bruno Tshibala, bado hajajiuzulu wadhifa wake kama Waziri Mkuu wala kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Serikali yake, licha ya kuwa aliombwa kufanya hivyo.

Kwa upande wa uundwaji wa Serikali, kazi kubwa iko mikononi mwa Rais mpya, Tshisekedi, kwa vile ni rais ambaye anatakiwa kuteua Waziri Mkuu kutoka kambi ya walio wengi bungeni.

Kwa mujibu wa sheria, chama au muungano wa vyama unaopata zaidi ya viti 250 ndio wenye sauti na ambao utakuwa na ushawishi wa kulidhibiti Bunge hilo la DRC kwa miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), vyama hivyo vimenyakuwa jumla ya viti 288 kati ya 429 bungeni, huku vyama vya upinzani vikiambulia viti 141 tu.

Chanzo: Mtz digital
 
Mwenye kuunda serikali hapo ni Rais Kabila, chama chake kina wabunge wengi na anajenga ushawishi chinichini japo hayupo ofisini. Juzi kawaita viongozi wa chama chake na kusaini makubaliano ya siri ya kuwa mtiifu kwake. Tshekedi ana kazi sana kwani hana wabunge.
Kwani hakuna option ya kulivunja bunge? Kama siyo wale wale ving'ang'anizi, anaweza kulivunja bunge na kuiamrisha tume iitishe uchaguzi upya ndani ya siku 90. Njia hiyo pekee ya kumvusha hapo alipo.

Kinachoonekana wazi ni kuwa Kabila anataka kurudi kama waziri mkuu, na kumpora huyo rais mamlaka kwa kutumia bunge.

Hutu Tshisekedi asipopata washauri wazuri wa namna ya kumwokoa kwenye kitanzi anachowekewa ataishia kuiharibu zaidi Kongo.
 
Kibaya zaidi analindwa na walinzi wale wale wa Kabila na hajapata nyumba ya kuishi yenye hadhi ya Rais, anaishi kwake.
 
Hahahaha, JKK for 2024/2025

Mkuu hii game niidokeza humu
FCC washapangwa tayari
Mwenye kuunda serikali hapo ni Rais Kabila, chama chake kina wabunge wengi na anajenga ushawishi chinichini japo hayupo ofisini. Juzi kawaita viongozi wa chama chake na kusaini makubaliano ya siri ya kuwa mtiifu kwake. Tshekedi ana kazi sana kwani hana wabunge.

MTC | 101|
 
KINASHASA, DRC

LICHA ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupiga kura na kumchagua rais mpya katika uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 23, mwaka jana, bado nchi hiyo imeendelea kubakia bila Serikali ikiwa ni wiki nne sasa tangu Felix Tshisekedi, alipoapishwa kuliongoza taifa hilo.

Mawaziri mbalimbali wa Serikali iliyokuwepo wameanza kujiuzulu mmoja baada ya mwingine, huku hatima ya Serikali mpya ikiwa bado haijajulikana.

Duru za kisiasa zinasema kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tshisekedi, ameshindwa kuunda Serikali kutokana na mgawanyiko unaoikumba jamii ya wanasiasa nchini humo.

Wakati huo huo Waziri Mkuu, Bruno Tshibala, bado hajajiuzulu wadhifa wake kama Waziri Mkuu wala kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Serikali yake, licha ya kuwa aliombwa kufanya hivyo.

Kwa upande wa uundwaji wa Serikali, kazi kubwa iko mikononi mwa Rais mpya, Tshisekedi, kwa vile ni rais ambaye anatakiwa kuteua Waziri Mkuu kutoka kambi ya walio wengi bungeni.

Kwa mujibu wa sheria, chama au muungano wa vyama unaopata zaidi ya viti 250 ndio wenye sauti na ambao utakuwa na ushawishi wa kulidhibiti Bunge hilo la DRC kwa miaka mitano ijayo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), vyama hivyo vimenyakuwa jumla ya viti 288 kati ya 429 bungeni, huku vyama vya upinzani vikiambulia viti 141 tu.

Chanzo: Mtz digital
Le triangle de la mort(FCC,CASH,LAMUKA)
Mungu awasaidie wakongomani maana wako kati ya pembetatu ya kifo
 
Kwani hakuna option ya kulivunja bunge? Kama siyo wale wale ving'ang'anizi, anaweza kulivunja bunge na kuiamrisha tume iitishe uchaguzi upya ndani ya siku 90. Njia hiyo pekee ya kumvusha hapo alipo.

Kinachoonekana wazi ni kuwa Kabila anataka kurudi kama waziri mkuu, na kumpora huyo rais mamlaka kwa kutumia bunge.

Hutu Tshisekedi asipopata washauri wazuri wa namna ya kumwokoa kwenye kitanzi anachowekewa ataishia kuiharibu zaidi Kongo.
Chisekedi no puppet wa Kabila na hakushinda hivyo mambo no yaleyale wakongo sio Kama Kama bongo kwa akina jecha na jaji kibaraka
 
Kazi ipo sana sasa hivi tshishekedi na Vital Khamere (CASH) hawana option bali ni kuungana na Kabila na vyama 18 vinavyounda( FCC) ili kumdhibiti Fayulu wa LAMUKA kwani wiki iliyopita kapiga mikutano miwili GOMA na KIKWIT ni balaa!!!!!
Na Vital Khamere ndio MTU wa Kati ,kati ya Kabila ( FCC ) na Felix ( CASH ) , Fayulu na Moise Katumbi bado wana nguvu ,ingawa inadhibitiwa chini kwa chini kupitia kwa Kyungu wa Mwanza

MTC | 101|
 
Kibaya zaidi analindwa na walinzi wale wale wa Kabila na hajapata nyumba ya kuishi yenye hadhi ya Rais, anaishi kwake.
Hahahaha, asee

Mkuu walinzi wale wale kivipi yaani ?
Yaani Felix alitakiwa awe na VIP protection tofauti na ya serikali ?

au VIP protection ile ile ( kwa maana ya watu wale wale wa JKK ) ndio wako na Felix sasa?

MTC | 101|
 
Na Vital Khamere ndio MTU wa Kati ,kati ya Kabila ( FCC ) na Felix ( CASH ) , Fayulu na Moise Katumbi bado wana nguvu ,ingawa inadhibitiwa chini kwa chini kupitia kwa Kyungu wa Mwanza

MTC | 101|
emoji769.png
Baba kyunguwa kumwanza kawa boss wa wabunge wa kitaifa depute national

Kyungu ni mtu wa ku take advantages keshamkubali felix.
 
Hahahaha, najua kuwa ndio rais wa bunge la taifa,huyu Mzee wa kiruba mjanja mjanja sana,anajua kucheza na nyakati na fursa

Yuko na Felix kwa ajiri ya Ku neutralize wakatanga maana Kyungu wa Ku mwanza ni baba wa wakatanga ,na amekua akitumika hivi kipindi chote

MTC | 101|
 
Baba kyunguwa kumwanza kawa boss wa wabunge wa kitaifa depute national
Kyungu ni mtu wa ku take advantages keshamkubali felix.
Yeah hiyo nafasi kwa Mzee Gabriel kyungu wa ku mwanza ni muhimu ili kubalance na kuwadhibiti LAMUKA ,huyu Mzee wa katangee wanamuelewa sana

MTC | 101|
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom