Rais Samia: Wapinzani nimewapa kazi ya kukutana na kuzungumza, walete mapendekezo yao tukubaliane

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma leo tarehe 18 Oktoba, 2022



Zitto Kabwe- Kiongozi Mkuu wa Chama, ACT Wazalendo
Nikiwa kiongozi wa kitaifa, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa juhudi kubwa zinazofanyika kuwaweka watanzania pamoja bila kujali itikadi zao. Kuwepo kwangu hapa ni ishara hiyo. Hauangalii vyama vya siasa vya watu, bali unawaangalia watanzania kwa pamoja na hili napenda kukushukuru sana na kukupongeza sana.

Kazi ambayo umefanya tangu kuingia madarakani ama kwa kukutana na vyama vya siasa kimoja kimoja, au kupitia kikosi kazi ambacho ulikiunda kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kuboresha siasa zetu, hali ya siasa nchini imekuwa ya utulivu sana.

Hakuna njia nyingine yoyote ya kuifanya nchi yetu iende mbele isipokuwa njia hii unayopita ya kujenga maridhiano ya kitaifa na kwa hili, kwa niaba ya viongozi wote wa kisiasa nchini napenda kukupongeza na kukushukuru sana. Nakuomba uendelee hivihivi, usiache juhudi hizi za mageuzi ya kisiasa.

Ninaamini kuwa baada ya kikosi kazi kumaliza kazi yake tutaanza kuona mabadiliko ya kisheria yatakayoweka Sawa Ushindani wa kisiasa.

Nataka niwaombe nyie, kama wananchi wenzangu wa mkoa wa kigoma, Rais wetu ana dhamira njema sana. Rais wetu ana maono na matamanio makubwa, siyo kwa nchi tu, bali na Kigoma. Na niongee kama mwami, mama huyu hapa, mpokeeni, tufanye naye kazi, tushirikiane naye, tulete mabadiliko ktk nchi hii.

Samia Suluh Hassan- Rais
Sekretarieti ya mkoa imeweza kupata hati safi ya ukaguzi kwa miaka 3 mfululizo na halmashauri zote nazo zimepata hati safi kwa mwaka wa fedha 2020/21. Hongereni sana kigoma. Ni matarajio yangu kuwa usafi huu utaendelea.

Kupitia TRA, mapato ya Kigoma kwa mwaka 2020/21 yameongezeka hadi kufikia bil 19.2 kutoka bil 16.2 mwaka 2020/21 ikiwa ni ongezeko la tsh bilioni 3, sawa na 18.5%

Kwa ushiriki wenu katika zoezi la sensa ya watu na makazi, tunatarajia kwamba karibuni hivi, tutapata idadi halisi ya wakazi wa kigoma. Lakini nina hakika, taarifa zikija, takwimu zikija, watoto watakuwa wapo wengi zaidi kuliko watu wazima na wazee. Kwa maana hiyo, hii inatupa mwelekeo kwamba tuweke zaidi mkazo kwenye shughuli za watoto hasa afya, elimu, maji na mambo mengine ili watoto wetu hawa wakue vizuri, wawe wanakigoma wema, waijenge kigoma baadae.

Serikali imetenga bil 42 kwenye mwaka 2022/23 kwenda NIDA ili kutengeneza vitambulisho vya taifa milioni 13 ili wale ambao hawajapata waweze kuvipata.

Leo mmemsikia mwanangu Zitto hapa, nilikuwa natayarisha masikio atakwenda kusema nini, lakini mwisho wa maneno yake yote kasema Nawakabidhi mama huyu, mpokeeni. Inamaana hakuna, yale yaliyokuwa yakisemwa kabla, maendeleo kwa wananchi ndicho walichokuwa wakipigia kelele, maendeleo sasa yanafanywa kwa wananchi, kelele zitahamia upande mwingine.

Na bahati nzuri hata upande mwingine ule wa kisiasa nimewapa kazi wenyewe wakutane, wazungumze watuletee tuone yale yanayo tekelezeka, tukubaliane nao, tuyatekeleze kwa haraka.

Kwa hiyo ni kweli kwamba kufanya watanzania wote waichangie tanzania yao, wafanye kazi kwa ajili ya Tanzania yao kunaleta amani na utulivu na maendeleo yanakwenda haraka, nawashukuru sana vyama vya siasa kwa kazi nzuri wanayofanya katika majadiliano na maridhiano.

Kilichobaki tuendelee kuzalisha, tuendelee kuchapa kazi ili Serikali ikusanye zaidi, maendeleo yaje zaidi na taifa letu liimarike zaidi na zaidi.
 
Vijana, pambaneni jua lichomoze aseee, angalieni kijana mwenzenu ambaye kwa sasa anajiita mzee pale ACT, sasa analamba asali na aonyeshi upinzani kwa serikali au hata kuishauri bali anafagilia hata negative issues!.
 
Mm nafikir sababu hatujapata ratiba ya kikosi kazi ikitupa mrejesho,basi ndio tutafanya tathimin.
 
..Mwenyekiti wa CCM hatakiwi kuvipangia majukumu au nini cha kufanya vyama vingine vya siasa.

..Rais SSH aachane na imani kwamba ana haki ya kutumia madaraka na vyombo vya dola kudhibiti vyama vingine.

..Vyama vyote vipewe nafasi ya kufanya shughuli zao kwa usawa bila kubugudhiwa na vyombo vya dola.
 
..Mwenyekiti wa CCM hatakiwi kuvipangia majukumu au nini cha kufanya vyama vingine vya siasa.

..Rais SSH aachane na imani kwamba ana haki ya kutumia madaraka na vyombo vya dola kudhibiti vyama vingine.

..Vyama vyote vipewe nafasi ya kufanya shughuli zao kwa usawa bila kubugudhiwa na vyombo vya dola.
Baaasi....otherwise ni longo longo tu kama zingine
Anataka mapendekezo gani?

Aache woga
 
Hali ya uchumi ni mbaya.

Maswala ya siasa za majukwaani ni ziada tu.

Wanasiasa mnapofikiria kuwekeana mazingira mazuri mfikirie na wananchi pia wanaopigwa na jua na makali ya tozo.
 
..Mwenyekiti wa CCM hatakiwi kuvipangia majukumu au nini cha kufanya vyama vingine vya siasa.

..Rais SSH aachane na imani kwamba ana haki ya kutumia madaraka na vyombo vya dola kudhibiti vyama vingine.

..Vyama vyote vipewe nafasi ya kufanya shughuli zao kwa usawa bila kubugudhiwa na vyombo vya dola.

Kawapangia, kawatuma na wanayafanya yote waliyopangiwa na waliyotumwa. Wewe keyboard warrior endelea kuamini vinginevyo ambavyo havitafanyika hata ndotoni
 
Kawapangia, kawatuma na wanayafanya yote waliyopangiwa na waliyotumwa. Wewe keyboard warrior endelea kuamini vinginevyo ambavyo havitafanyika hata ndotoni

..watu kama nyinyi sijui mna matatizo gani.

..kwanini hampendi nchi yetu iendeshwe kwa kuzingatia HAKI?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom