Rais Samia vunja mifumo hii utusaidie wananchi wa maisha ya chini Morogoro hasa wilayani Kilosa, tunaonewa

tawakkul

Member
Oct 12, 2022
88
67
Habari wakuu JF!

Iko hivi;

Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu atakayepinga kuwa katika awamu ya sita kumefanyika ujenzi wa shule, hospitali, zahanati, vituo vya afya miundombinu ya hali ya juu kuliko awamu zote.

Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu atakayekataa kuwa awamu ya sita imeleta upendo, mshikamano, amani na maelewano zaidi ya jamii hasa kwa upande wa vyama vya siasa.

Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu atakayetaa kuwa awamu ya sita imefungua nchi na kukuza diplomasia zaidi na nchi jirani.

Kifupi ni kwamba hakuna atakayekataa kuwa awamu ya sita ina muelekeo wa kuifanya nchi kupiga hatua ya juu zaidi kimaendeleo.

Lakini leo hii akitokea (Japo ni kusadikika) Dr Pombe Joseph Magufuli, wakashindana na Dr Samia Suluhu Hassan rais wa nchi yetu, iwe kwenye uchaguzi wowote ule, wa chama au wa taifa, Dr Pombe Joseph atashinda pa kubwa sana.
1672560352941.png



Unafikiri ni kwa nini atashinda pakubwa!?

Unafikiri ni kwanini wakati wa ufunguzi wa ujazaji maji wa bwawa la Mwl Nyerere pale Morogoro/Pwani, alipokuwa akitajwa hayati Pombe Magufuli watu walikuwa wanashangilia sana?


Ukipita kwenye vikao au vikundi vya wananchi wenye maisha ya chini na ukijaribu kumuelezea hayati Pombe Magufuli, wengi wao wanatamani angekuwepo leo hii kama rais.

Hiki ninachokiandika hapa ni hali halisi na siyo “uchawa”, siwezi kuwa chawa wa mtu ambaye hayupo duniani. “TUACHE KUPINGANA NA UKWELI, HUU NDIYO UKWELI.”

SOMA UKWELI WENYEWE HUU HAPA;
Ni kwamba kwenye nchi hii kuna watu wamejijengea mifumo kandamizi(oppressive systems), mifumo onevu(bully systems),mifumo ovu (evil systems). Hii ni mifumo migumu sana kuivunja. Rais Samia bado hajaonekana kuivunja mifumo hii. Hata rais wa awamu ya nne JK alishawai nukuliwa akisema …..”kuna watu wana uwezo na nguvu za kifedha, ukiwagusa nchi itatikisika hii” hapa alikuwa anamaanisha mifumo ninayoizungumzia.

Kuna watu wanahakikisha wanapata nafasi za uongozi serikalini na kwenye chama au anahakikisha anapenyeza watu wake kwenye uongozi kisha anajenga mifumo kwenye taasisi zote za serikali kama vile polisi, mahakama, TAKUKURU, TRA, Ardhi na kwenye mamlaka mbalimbali za serikali.

Baada ya kujenga mifumo hiyo, akitaka kitu fulani kwa njia ya panya au akitaka kulindwa kwa jambo hovu kwake ni rahisi tu.

Kwa mfano akitaka ardhi maeneo fulani, anachukua simu anapiga kwa mtu wake wizara ya ardhi kila kitu kinakamilika muda mfupi tu, na hata kama eneo hili kuna watu wanaishi watafukuzwa au kuamishwa kwa visingizio mbalimbali ili yeye apewe eneo hilo.

Mara nyingi watu wenye mifumo kama hii huwa hawagushwi, ukimgusa tu utakiona ‘cha mtema kuni’. Na siku zote wanapenda kuwaonea watu wenye maisha ya chini na elimu duni kwa kuwapora maeneo yao.

Mfano pale mkoani Morogoro kiegea kuna mtu maarufu kwa jina la ‘Jero’ amehodhi eneo kubwa kwa njia ya panya, ole wako uingie anga zake utajua kwanini nzi wanapenda vitu vilivyooza. Ni mbabe, mtemi na mkatili. Anawatuma ‘chawa’ wake wanakudunda na hakuna atakayekusaidia. Ukienda taasisi yeyote ya serikali utaambiwa ‘tutalishughulikia’ na ukijaribu kwenda mahakamani inawezekana ukatiwa hatiani na ukafungwa wewe.

Mfano mwingine ni mwenyekiti wa chama cha CCM wilayani Kilosa, huyu ni maarufu kwa kupata mashamba makubwa makubwa kwa njia zisizo sahihi na kuyamilikisha kwa familia yake.

Bwana huyu amejijengea mifumo onevu na ni migumu kuivunja. Waziri mkuu mwl Majaliwa anamfahamu sana huyu, alishawai mparua pale Kilosa kwa mifumo yake ovu. Ni mtu anayetumia uongozi wake kujipatia maeneo makubwa na kisha kuandika majina ya ndugu zake(Nadhani anaikwepa sheria ya maadili ya viongozi wa umma).
1672560537443.png


Waziri mkuu Majaliwa Majaliwa, anategemewa sana kuweza kuivunja mifumo ovu.

Kuna shamba Na. M 19 lililopo Mbigiri Magole lenye zaidi ya ekari mia nne, shamba hili lilikuwa linalimwa na kikundi(ushirika) cha wananchi wa hali ya chini wakijaribu kujinasua kutoka kwenye dimbwi la umasikini kwa kulima kilimo cha miwa, yeye kalipoka na amemmilikisha ndugu yake.

Wanakikundi hawa walilipata shamba hili kutoka kwa mmiliki wa awali kwa makubaliana ya pamoja ya kulima miwa ya sukari. Wanakikundi walikopa benki zaidi ya milioni mia tano(500milioni) na kulianda shamba, kuchimba visima na kuanza kupanda miwa.

Baadaye shamba liliingia kwenye mgogoro na benki na kutangazwa kupigwa mnada. Yeye mwenyekiti wa CCM wilaya Kilosa badala ya kuwasaidia wananchi hawa kutatua mgogoro na benki, kwa kutumia cheo chake na pesa alizonazo kalipata shamba lililokuwa linapigwa mnada kwa bilioni moja kapewa kwa milioni mia tatu tu.

Viongozi wa kikundi hicho wamejaribu kuomba msaada kwa viongozi wa serikali wa wilaya mpaka mkoa, na kila walipokwenda wanaambiwa ‘tutalishughulikia’.

Hapo awali wanakikundi hao walikubali kulilipa deni hilo la bilioni moja kwa awamu, lakini huyu mwenyekiti wa CCM kwa kutumia cheo chake na pesa alizonazo kaingilia kati na kulichukua shamba hilo.

Kana kwamba haitoshi viongozi wa kikundi hiki wanabambikiziwa kesi na kutishiwa kufungwa jela. Mahakama, polisi, taasisi za ardhi, kuanzia uongozi wa kata mpaka mkoa kote ana mifumo yake utamfanya nini.

Magufuli alikuwa na ujasili wa kupambambana na mifumo hii na ndiyo maana leo hii ukitaja jina lake mbele ya wananchi wa hali ya chini wanamshangilia sana.(Huu ni ukweli na tusijifanye hatuuoni, dawa ni kuufanyia kazi).

Mfano mwingine ni jamii ya wafugaji, hawa wana mifumo yakutisha, hatari na onevu.
Mfugaji anaingiza mifugo yake kwenye shamba la mkulima, mkulima akijaribu kuitoa anapigwa bakora na virungu vya kutosha, anaambiwa “acha ng’ombe ile ishibe” akienda kutoa taarifa polisi anakamatwa yeye mkulima anawekwe ndani na anafunguliwa kesi ya uchochezi.

1672560656338.png


JE, RAIS WETU MCHAPA KAZI DR SAMIA SULUHU HASSAN, MWENYE NIA YA KUIKOMBOA NCHI KWENYE UMASIKINI UNAWEZA KUIVUNJA MIFUMO HII OVU?

Tuna amini unaweza kwa vile wewe ni mcha Mungu na mpenda haki.

Na Mheshiwa rais ukiweza kuivunja mifumo hii utakuwa rais bora kupata tokea katika historia ya nchi hii. Madarasa, zahanati, madaraja, hospitali, ruzuku mbolea, mabwaya ya umwagiliaji, mapatano na vyama vya siasa vyote umefanya. Lakini kumbuka binadamu hapendi kuonewa, vunja mifumo hii onevu ili umalize kazi.

Mkuu wako wa mkoa wa Morogoro Fatuma ameonyesha kujaribu kupambambana nayo. Ameanza kwa huyu mtu anayeitwa ‘Jero’, sinzani kama ataweza kwa mwenyekiti wa chama wilaya ya Kilosa!.

Watu wanausemi.

"WACHA INYESHE TUONE PANAPOVUJA, NA UKITAKA USIFUATWE NA NZI ACHANA NA VILIVYOOZA."​
 
Back
Top Bottom