Salaam, Shalom.
Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.
Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;
1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA
Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!
Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.
2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.
Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.
3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA
Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.
4. UTAKATISHAJI FEDHA
Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.
5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI
Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.
Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.
6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.
Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.
HITIMISHO
Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.
OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.
Amen.