GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,102
Rais Samia Hassan ameyazungumza hayo leo katika hafla ya kusimikwa rasmi mkuu wa kanisa la KKKT Askofu Dkt Alex Malasusa katika kanisa la Azania front jijini Dar es Salaam
Rais Samia ameshangazwa kwanini tatizo la vijana kutokuoa au kuolewa linaongezeka nchini Tanzania wakati vijana wamefikia umri wa kuoa na kuolewa
Rais Samia ameshangazwa kwa sasa vijana wa kike ndio wanaohudhuria sana kwenye mambo ya kidini na kuwaacha kundi kubwa la vijana wa kiume wakipotea na hivyo kusababidha ombwe kubwa kwenye jamii
Kwa mujibu wa Rais Samia Hassan,Taarifa ya ripoti ya mahusiano ya jamii inaonyesha maeneo ya mjini tatizo la vijana kutooa na kuolewa linazidi kuwa kubwa zaidi ukilinganisha na vijijini
Aidha Rais Samia amesisitiza kuna migogoro mikubwa sana ndani ya familia hasa ndoa na hivyo kupelekea vijana kulelewa kwa kukosa maadili
Kwa mujibu wa Rais Samia zaidi ya migogoro elfu thelathini na tisa ya ndoa imeripotiwa
Rais Samia amewaomba wa Tanzania warudi kwenye misingi yetu ya asili ambapo vijana walilelewa kwa maadili makubwa sana ,Akitolea mfano enzi zao ilikuwa ngumu sana kwa mwanaume kumtongoza mwanamke na mwanamke akakubali kirahisi rahisi kwani wanawake walikuwa na misimamo tofauti na leo
Rais Samia ameiomba jamii wazazi na walezi kuwafundisha watoto maadili mema kwa kuwapeleka kwenye imani zao ili kuwajengea misingi bora ya ufahamu na maisha hapo baadae
##
Maswali ya kujiuliza kama Taifa,
1.Tatizo la vijana kuoa na kuolewa ni mambo ya maadili kama Rais Samia alivyosema au maisha magumu kwa vijana wa kiume?
2.Lakini kuna vijana wana maisha mazuri mbona hawataki kuoa au kuolewa pia?