Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mwigulu Nchemba, Naomba kutoa ushauri wangu kwenye ushuru wa magari.
HAKIKA ITACHOCHEA UCHUMI MNO
- Nimeona ushuru wa magari unazidi kuongezeka, Mhe Rais/Waziri wa fedha dunia inabadilika kwa haraka sana, Magari ya kutumia umeme EV yanakuja kwa haraka sana na ni jambo lisilozuilika kwa hiyo ni kupindi sahihi cha kuchukua hatua za kuchochea matumizi ya magari Tanzania, PUNGUZA SANA KODI, je utafidiaje hiyo Gap?
- Punguza kodi kwa nusu gari liwe 30% tu ya CIF , ili kuongeza idadi ya magari yatayoagizwa nje mara tatu zaidi na serikali itapata hela zaidi kwenye regstration, renew na kwenye kodi ya mafuta, vipuri vitaagizwa sana mara tatu zaidi, utatengeneza ajira ya mafundi mara tatu zaidi.
- Ushuru uruhusiwe kulipwa kwa awamu kwa makampuni, taasisi na biashara zilizosajiliwa rasmi, wafanyakazi wa umma, wa makampuni, wafanyabiashara wenye 3 yrs tax clearance wawe wanalipa asilimia 40 akiagiza gari iliyobaki aweze kulipa kidogo kidogo kwa mwaka mzima au miwili. KWANINI ILI KUCHOCHEA WATU KUAGIZA MAGARI SANA KABLA HAYA MAGARI YA MAFUTA HAYAJAONDOLEWA SOKONI.
- Kupunguza sana ushuru wa mabasi, malori na magari ya Biashara, Haya ni magari yanayotumia mafuta mengi sana kwa siku na ndo magari yanayoagiza sana vipuri Serikali itafidia kwa kuchukua ushuri mkubwa wa mafuta na vipuri na pia itachochea sana ajira nyingi sana kwa wingi. Inamaana gas stations zitaongezeka sana na zitalipa sana kodi, malori ya kusafirisha hayo mafuta mikoani yataongezeka sana, KODI YA MATAIRI IONGEZEKE SANA KUFIDIA GAP
- Ruhusu magari ya zamani kuanzia mwaka 1990 kusiwe na uchakavu, MAANA YAKE YAKE watu wengi sana watamiliki magari na akishamiliki gari atanunua mafuta na atanunua vipuri atalipia insuarance , atarenew licence na motor vehicle serikali itapata hela sana na usafiri utashuka sana huko vijijini
- Mwisho turasilishe mikopo ya magari yaani kuwe na credit bureau ili wauza magari wawe na uhusiano na mabenki watu wawe wanakopa kama tunavyokopa huku nje ili kila mtu aweze kumiliki gari
Mfano: Tanzania tuna magari milioni 1 laki 6 tu na tupo millioni 62 Canada ina watu millioni 36 wana magari millioni 67 mara 7 ya magari yote ya East Africa. kwa nini kwa sababu tajiri anakopa la level yake analipa kwa miaka 6 na masikini anakopa la level yake kwa muda mfupi na kuna mbulula wanachukua used hoi kabisa kwa cash ila serikali inafaidi sana knye ku renew licence plates , Driving livence na mafuta
HAKIKA ITACHOCHEA UCHUMI MNO