Rais Samia unayo nafasi ya kukemea na kukomesha udhalilishaji wa wanawake nchini, usipowatetea wewe Mungu atainua mtetezi

Benaya-

JF-Expert Member
Jul 31, 2019
4,417
7,610
Mheshimiwa rais na amiri Jeshi mkuu Samia Suluhu shikamoo.

Ninaandika machache kuhusu udhalilishaji unaoendelea nchini kwa masikitiko makubwa sana.

Kwa wasomi wa Biblia wanafahamu vyema hadithi ya Binti wa Kiyahudi jina lake Ester.
Binti huyu hakuwa na wazazi bali alilelewa na mjomba/binamu yake aitwaye Modekai.

Ester alishawishiwa na Modekai ambaye alikuwa mmoja wa watumishi wa Mfalme Ahasuero kuwa ajitokeze kwenye tafrija ya mfalme ya kutafuta mwanamwali awe mkewe.

Ester alifanikiwa kuibuka mshindi na kuwa mke wa mfalme, jambo ambalo lilikuwa gumu sana kwa Myahudi kuibuka mshindi kwani yeye alikuwa ni mtoto wa mmoja wa watumwa wa mfalme Ahasuero.

Baada ya Ester kuwa mke wa mfalme kwa kiasi flani alijitenga na Wayahudi wenzake ambao waliendelea kuteswa kubaguliwa nk.

Lakini ulifika wakati mgumu wa Wayahufi wote kuuawa kwa amri ya mfalme.

Modekai mjomba wake alimwendea ali awatetee lakini Ester hakuonekana kujali sana.

Ndipo Modekai alipomwambia Ester.
IKIWA HUONI UMUHIMU WA KULITETEA TAIFA LAKO MUNGU ATATOKEZA MSAADA MWINGINE LAKINI WEWE NA NYUMBA YAKO UTATEKETEA.

Rais wangu, kumekuwa na udhalilishaji mkubwa sana wa wanawake nchini kwa neno maarfu KONEKSHENI.

Hii inafanywa sana na dada aitwaye Mange Kimambi, jambo hili limeleta hofu na mashaka kwa watu maarufu na wenye ushawishi katika jamii hasa wasanii.

Jambo hili lisipodhibitiwa mapema hakika litasababisha vifo vitokanavyo na msongo wa mawazo.

Mheshimiwa rais wewe ni mwanamke Mungu ameruhusu uwe rais sio kwasababu wewe ni bora kuliko wanawake wote Tanzania bali imempendeza akuchague wewe ili uvae viatu vya mateso ya wanawake wa Tanzania.

Mange anakusikiliza sana...ukimwagiza msaidizi wako Yunus akipiga simu moja tu wanawake watakuwa salama.

Mama kemea kemea hii kitu ni mbaya.

Ninatanguliza shukrani nikiamini utalifikiria jambo hili.
 
Tuna mfumuko wa Bei bhana mwacheni Rais kwanza adeal na vitu muhimu kwanza 😁😁 Hadi wa connection wakati walio wengi wanajirekodi wenyewe !!

Eti i"naawathiri kisaikolojia watajiua" ukijiua si tunabaki million 59 😁 Fanya mambo yako kwa siri , yaishie ndani huko huko

Wazazi tukomae na malezi ya watoto !! Kila mzigo tunamlaumu shetani na serikali !!
 
Tuna mfumuko wa Bei bhana mwacheni Rais kwanza adeal na vitu muhimu kwanza Hadi wa connection wakati walio wengi wanajirekodi wenyewe !!

Eti i"naawathiri kisaikolojia watajiua" ukijiua si tunabaki million 59 Fanya mambo yako kwa siri , yaishie ndani huko huko

Wazazi tukomae na malezi ya watoto !! Kila mzigo tunamlaumu shetani na serikali !!
Mama zako kuendelea kudhalilishwa sio hoja kwako?
 
Mama zako kuendelea kudhalilishwa sio hoja kwako?
Rekebisha hii kauli ya "mama zako" isomeke mama Yako kwani mama kinabaolojia ni mmoja TU na hao wengine ni shangazi!

Hoja Yako ni dhaifu Sana na inaonyesha hujafanya utafiti wa kutosha juu ya unayoyalalamikia! Hao wanawake wanachonga mchongo na wafanyakazi wa mange Kwa kuwauzia picha zao za matukio ya kipuuzi walizojirekodi wenyewe Kwa hiyari Yao Kisha wanagawana mpunga ambayo ni zaidi ya laki mbili Kwa Kila video!

Na pia wanatangaza biashara Yao ya ukahaba inayowaweka mjini ili wanaume wakware wawatafute na kuwatumia Kwa malipo makubwa!

Mshauri huyo uliyemwomba msaada apeleke mswada bungeni wa kuhalalisha biashara ya ngono ili apanue wigo wa Kodi kwani inalipa Sana na ni chanzo kizuri Cha mapato.

Usibweke Sana humu kwani huijui biashara ya ukahaba kuwa ndio kongwe mno tangu kuumbwa Kwa ulimwengu huu na inalipa kwani wenzetu huko ughaibuni wameiwekea sheria na kuwatambua Kama sex workers na wametengewa maeneo Yao ya biashara na kuwapa leseni kabisa!
 
Nani atamgusa Mange zaidi ya rafiki yake Samia?

Hao nibwashkaji. Amemrudishia passport, wamepiga picha pamoja.

Story nyingi zilivuja awamu ya tano sasa hivi walikuwa wanavujisha kwa mange wote wanalamba asali, ni timu moja.
 
Hao nibwashkaji. Amemrudishia passport, wamepiga picha pamoja.

Story nyingi zilivuja awamu ya tano sasa hivi walikuwa wanavujisha kwa mange wote wanalamba asali, ni timu moja.
Naona hilo li akaunti limefungwa rasmi na insta
 
1659731132808.png
 
Ila Mange kafanya watu waamke. Sasa mambo ya kurecordiana,video call,kutumiana video za uchi yataisha.
 
Huwa simwamini kabisa mwanamke anayevaa mawigi. Raisi afanye mpango aje bongo ana tuhuma za kujibu.
 
Mheshimiwa rais na amiri Jeshi mkuu Samia Suluhu shikamoo.

Ninaandika machache kuhusu udhalilishaji unaoendelea nchini kwa masikitiko makubwa sana.

Kwa wasomi wa Biblia wanafahamu vyema hadithi ya Binti wa Kiyahudi jina lake Ester.
Binti huyu hakuwa na wazazi bali alilelewa na mjomba/binamu yake aitwaye Modekai.

Ester alishawishiwa na Modekai ambaye alikuwa mmoja wa watumishi wa Mfalme Ahasuero kuwa ajitokeze kwenye tafrija ya mfalme ya kutafuta mwanamwali awe mkewe.

Ester alifanikiwa kuibuka mshindi na kuwa mke wa mfalme, jambo ambalo lilikuwa gumu sana kwa Myahudi kuibuka mshindi kwani yeye alikuwa ni mtoto wa mmoja wa watumwa wa mfalme Ahasuero.

Baada ya Ester kuwa mke wa mfalme kwa kiasi flani alijitenga na Wayahudi wenzake ambao waliendelea kuteswa kubaguliwa nk.

Lakini ulifika wakati mgumu wa Wayahufi wote kuuawa kwa amri ya mfalme.

Modekai mjomba wake alimwendea ali awatetee lakini Ester hakuonekana kujali sana.

Ndipo Modekai alipomwambia Ester.
IKIWA HUONI UMUHIMU WA KULITETEA TAIFA LAKO MUNGU ATATOKEZA MSAADA MWINGINE LAKINI WEWE NA NYUMBA YAKO UTATEKETEA.

Rais wangu, kumekuwa na udhalilishaji mkubwa sana wa wanawake nchini kwa neno maarfu KONEKSHENI.

Hii inafanywa sana na dada aitwaye Mange Kimambi, jambo hili limeleta hofu na mashaka kwa watu maarufu na wenye ushawishi katika jamii hasa wasanii.

Jambo hili lisipodhibitiwa mapema hakika litasababisha vifo vitokanavyo na msongo wa mawazo.

Mheshimiwa rais wewe ni mwanamke Mungu ameruhusu uwe rais sio kwasababu wewe ni bora kuliko wanawake wote Tanzania bali imempendeza akuchague wewe ili uvae viatu vya mateso ya wanawake wa Tanzania.

Mange anakusikiliza sana...ukimwagiza msaidizi wako Yunus akipiga simu moja tu wanawake watakuwa salama.

Mama kemea kemea hii kitu ni mbaya.

Ninatanguliza shukrani nikiamini utalifikiria jambo hili.
Kwa hiyo hapo Rais akisoma "Konnection" na Mange Kimambi,atakuwa ameshajua unasema nini?
 
Mama zako kuendelea kudhalilishwa sio hoja kwako?
Lakini hsys mambo hayajaanza kwa Mange wala hastaisha hata huyo Mange akiacha

Mimi nafikiri ni wasichana ambao wengi wao ni wahanga kuwa makini tu, usiende kulala na mwanaume ambaye sio mchumba wala mume ni danga tu mmekutana

Mwanaume anayejielewa aliyetoka naye mbali nafikiri ngumu sana kukulewesha na kuvujisha video zako au kurekodi tu

Halafu mara nyingi wasichana wanakubali kurekodiwa baadae inavujishwa
 
ULIVYO ANZA NA SIMULIZI ZA KUTOKA BIBLIA NILIJUA KUNA LA MAANA ULILO ANDIKA.
KWA SASA HII POST KAMA ZILIVYO ZINGINE NI ZA KUMTUKUZA MANGE KIMAMBI

GUEST UWENDE WEWE,
ULIPIE WEWE,
UJIREKODI WEWE,
VIDEO USAMBAZE WEWE.
MANGE AJE KULAUMIWA??
HALAFU RAIS AINGILIE KATI??
 
Back
Top Bottom