Rais Samia kuongoza Matembezi Maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza matembezi ya hiyari, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, ambayo ndiyo iliyoandaa matembezi hayo yatafanyika kwa kuzunguka mji Mkongwe wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Asma Ali Mwinyi, alisema azma ya matembezi hayo ni kuwafikia wanawake zaidi ya 100 pamoja na watoto ambao wana mahitaji maalum kufuatia kutekelezwa baada ya ndoa zao kuvunjika.

Asma alisema fedha itakayopatikana katika matembezi hayo itawasadia kuinuliwa kiuchumi wanawake paroja na Watoto wenye mahitaji maalum kutokana na uhitaji wao.
 
Pauline Gekul atajwe kabisa kama adui wa haki za binadamu 2023, kamnyanyasa vibaya kijana mdogo wa kazi kwa kumuigizia chupa ya Coca njia ya haja kubwa na kumtesa sana mtoto wa maskini
 
Haaa. Ajitayarishe kabisa kuelezea mbunge wa CCM aliyemdhalilisha kijana kwa chupa atafikishwa lini mahakamani. Justice kwa vijana wa kiume!!!
Kabisa mkuu, huyu mbunge mdhalilishaji achukuliwe hatua kali za kisheria, kuvuliwa unaibu waziri tu hakutoshi na hiyo sio hukumu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza matembezi ya hiyari, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, ambayo ndiyo iliyoandaa matembezi hayo yatafanyika kwa kuzunguka mji Mkongwe wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Asma Ali Mwinyi, alisema azma ya matembezi hayo ni kuwafikia wanawake zaidi ya 100 pamoja na watoto ambao wana mahitaji maalum kufuatia kutekelezwa baada ya ndoa zao kuvunjika.

Asma alisema fedha itakayopatikana katika matembezi hayo itawasadia kuinuliwa kiuchumi wanawake paroja na Watoto wenye mahitaji maalum kutokana na uhitaji wao.
Mbona alimdhalilisha Mh Mbowe kwa kumbambikia kesi ya ugaidi?
 
Back
Top Bottom