Rais Samia tusaidie Wilaya ya Ubungo kuna kero kubwa

winky

Senior Member
May 8, 2013
136
101
Naomba kuchukua nafasi hii kuelezea changamoto zetu na kutoa pendekezo kuwa wilaya ya ubungo igawanywe itoke wilaya ya ubungo na kibamba ili tupate mbunge, dc, das na halmashauri yetu. Kwa kuwa sisi wakazi wa kipande cha kuanzia Mbezi makabe, msakuzi,Msumi, mpiji yote na kidimu hawa viongozi hatuna, hawakumbuki wala kujali kuwa hili eneo lipo chini yao. Matatizo ni mengi sana na wala hawajishughulishi.
Naelezea kama ifuatavyo:

1.Bara bara ni mbovu sana kiwango hazipitiki. Ndio sababu hata wao hawawezi kupita maeneo haya. Mbunge aliulizwa kuhusu bara bara bungeni akajibu kisiasa sana na kusema iko kwenye matengenezo lakini kilichofanywa ni uhuni yani ni kipande kilichowekwa kutoa lawama hakina mwanzo wala mwisho. Na hili la ubovu wa barabara lilisababisha ajali kubwa sana ya dala dala kugongana na watu wengi kuumia sana na wakaa kimya wakati wanajua tatizo ni bara bara.

2.Hakuna Masoko. Maisha ni ghali sana mana kama soko ni mbezi mwisho nalo sio rasmi yaani vyakula ni ghali sana.

3.ulinzi na usalama ni mdogo maana vituo vya polisi ni vichache sana. Eg: huko kidimu njia ya kupita pande watu saa 2 tu unakabwa tena hadi na boda boda aliokubeba hakuna kituo cha polisi inabidi uende gogoni almost 2 hrs. So watu wamekimbia makazi yao hali ya usalama ni mbaya kote. Wezi wanapishana mtaa huu mara mtaa huu.

4. Suala la maji tunamshukuru waziri Aweso walau baada ya malalamiko akalivalia njuga.

5.Domestic violence ni kiwango kikubwa sana na hakuna msaada. Wanawake na watoto wanafanyiwa ukatili na hakuna msaada kwa mjumbe wala mtendaji. Eg:Mtu kachomwa hadi pasi mgongo wote wanamwambia rudi tu nyumbani sababu aliofanya ukatili huwa wanakunywa naye na yupo kwenye kamati yao ya ulinzi.

6.Makelele na sauti za mziki ni kubwa sana sana na wamepewa baraka na serikali za mitaa baada ya kupewa chochote. eg: mtaa mmoja una bar kama tatu na makanisa 4 yote yameweka spika za sauti ya juu wanashinda hadi usiku wa manane.

7.wajumbe n wenyeviti wa serikali za mtaa kazi yao kubwa ni kufatilia tu hela za ujenzi ambayo si chini (80,000 - 250,000) yaani ukimwaga mchanga tu hawa hapa wapewe chao na hela ya muhuri kwenye mauziano ambacho kiwango sio chini ya (200,000-500,000) lakini kinyume na hapo hakuna wanachotatua ama kufatilia. Ukiipenda nafasi ya bara bara ya mtaa unampa tu mjumbe chake na mwenyekiti basi unaziba bara bara na hakuna wa kukuuliza hii hasa ipo sana Msakuzi.

8.Tunashukuru dispensary za watu binafsi lakini za serikali ni kilio kikubwa sana.

9. Mjumbe anasimamia mitaa mingi na mikubwa kiasi anashindwa kufanya kazi kikamilifu. Mapitio ya mitaa yafanyike upya. Nyumba mpya ni nyingi sana.

Nb:
1. haya yote yanayotokea sababu hatuna viongozi wanaofatilia, viongozi waliopo wanapewa taarifa feki na hao watendaji na wenye viti
Wao hawathubutu hata siku moja kutembea na kuongea na wananchi, RC ndo hatumfahamu kabisa yeye anapitia kwenye lami tu wala hana idea ukubwa wa sehemu na mahitaji ya watu wake sababu anaamini hizo report feki wanazompa.

2.Mbunge ndo hatuna kabisa hata mahojiano yake ya mwisho alitaja barabara mbili tu ndo zinamsumbua. Yaani maelezo yake hayatambui hiki kipande kabisa. Kiukweli sisi huyu hatumuhesabu.

3.DC na watu wake hawajawahi hata kujisumbua kusikiliza hata kero za wananchi.yaani sio kipande chao hiki.

4.Madiwani ndo kabisa hatuwaoni hadi tunasahau kama wapo kwenye haya maeneo.

Tunaomba Mheshimiwa Rais atuangalie kwa upya kero ni nyingi na hatuna viongozi wa kutusikiliza na kututatulia changamoto zetu.
 
Back
Top Bottom