Rais Samia Suluhu umemtuma Makonda kuwavuruga watendaji wa serikali au kueneza siasa?

SHANTI

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
296
365
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia ya kumsemea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

Tujiulize maswali machache?

(1) Makonda anamhoji kamishina wa TRA? au mtumishi wa umma mwenye mamlaka yeyote kwa hadhi gani? wakati mamlaka ya Uteuzi ya mtendaji wa Serikali sio chama cha mapinduzi?

-Mfano: kuna wakati wenyeviti wa CCM walikuwa wanafanya mchezo kama wa makonda wakawa wana waonea madkatari mpaka ikabidi itoke kauli kuwataka viongozi wa chama wasiiingilie majukumu ya taaluma zisizo wahusu kwa sababu wanaleta mkanganyiko.

Vuta Taswira umeajiriwa Tamisemi .TCRA,sijui wapi huko halafu unawajibishwa na katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi? huuu si mzaha unaopitiliza, Job Description haisemi kwamba utawajibika kwa katibu wa CCM inasema utawajibika kwa mamlaka iliyokuteua, hapa elewa neno mamlaka iliyokuteua?

(2) Je, Rais umemkambidhi mamlaka yako Bwana Makonda? Maana anaingilia kila sekta na anatoa maagizo na kuleta mkanganyiko usio na Tija?

Mfano: Mama Samia yeye ni Rais , wa Nchi kiongozi mkuu na M/kiti wa CCM. Akitembelea mradi kwa kofia ya Rais ana mamlaka kamili ya kuwajibisha mtendaji wa serikali kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi. Vivyo hivyo kwa makamu wa Rais , Waziri mkuu na watendaji wakuu wa serikali inaswihi.

(3) Nauliza Tena mama umemtuma Makonda kwenda kuwaruga watendaji wako wa serikali? washike lipi sasa? Vipi waendelee kupokea maagizo ya makonda au watekeleze mahitaji ya J.D za kazi zao?

(4) Nauliza tena mama wewe hauoni kuna mkanganyiko unaenda kutokea kwa watendaji walio chini yako, hauoni huyu anakwenda kuwachonganisha watendaji na mamlaka zao za kuwajibika? ni kweli watendai na mawaziri wafanye presentation ofisi za chama ?

Ndio maana nauliza umemtuma kueneza itikadi ya chama au kuwavuruga watendaji wa seriakli?

Usipoziba ufa utajenga ukuta, nashauri tu aendelee kukisemea chama ila ajiweke mbali na shughuli za serikali, huyu mtu atabeba majukumu ya cheo chako kwa kivuli kukisemea chama kukusemea wewe Mh. Rais na mwishowe watendaji wataaacha kufanya kazi. Nchi ilikuwa imetulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.
 
Hatujui tushike lipi,
La serikali, la chama ama la uswahiba.
Screenshot_20231022-153235~2.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachosumbua nii hii concept ya chamade kaunda serikali. Na serikali inatekeleza ilani ya chamade hicho.

Ukiwa ndani ya Chama cha mapinduzi na ukawa na elimu ya hapa na pale basi unaweza ukajiaminisha kabisa kwamba kila aliyeko kwenye ofisi ya umma basi anatakiwa kuwajibika kwa kiongozi wa chama cha mapinduzi wa ngazi yoyote ile.

Unaweza ukaamini kbisa kwamba katika nchi hakuna mtu au taasisi au mhimili ulioko juu ya chama cha mapinduzi.
 
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia i ilikuwa imetulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.

Mfumo dume ni mfumo wa Mungu.
 
Kinachosumbua nii hii concept ya chamade kaunda serikali. Na serikali inatekeleza ilani ya chamade hicho.

Ukiwa ndani ya Chama cha mapinduzi na ukawa na elimu ya hapa na pale basi unaweza ukajiaminisha kabisa kwamba kila aliyeko kwenye ofisi ya umma basi anatakiwa kuwajibika kwa kiongozi wa chama cha mapinduzi wa ngazi yoyote ile.

Unaweza ukaamini kbisa kwamba katika nchi hakuna mtu au taasisi au mhimili ulioko juu ya chama cha mapinduzi.
Sadtruth 😔
 
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia ya kumsemea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
etulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.
Akili zako ni ndogo kuweza kuelewa mambo yalivyo nchini ... kwa sasa tz uwezi kupewa uongozi wowote wa kiserikali bila ya kuwa mwanachama wa ccm....isipokuwa kwenye majeshi tu napo kuna wanachama wa siri wasio tambulika rasmi ..... kama ujui huo mfumo nenda kajifunze burundi . Burundi uwezi kuwa na cheo cha serikalini chochote hadi wakuone ni mwanachama wa chama tawala. Inapo kuwa hivyo ndiyo maana makonda anaweza kuwa hoji ni watu wake chamani
 
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia ya kumsemea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

Usipoziba ufa utajenga ukuta, nashauri tu aendelee kukisemea chama ila ajiweke mbali na shughuli za serikali, huyu mtu atabeba majukumu ya cheo chako kwa kivuli kukisemea chama kukusemea wewe Mh. Rais na mwishowe watendaji wataaacha kufanya kazi. Nchi ilikuwa imetulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.
Tuliwambia Makonda hana mbele wala Nyuma😆😆😆
 
Kinachosumbua nii hii concept ya chamade kaunda serikali. Na serikali inatekeleza ilani ya chamade hicho.

Ukiwa ndani ya Chama cha mapinduzi na ukawa na elimu ya hapa na pale basi unaweza ukajiaminisha kabisa kwamba kila aliyeko kwenye ofisi ya umma basi anatakiwa kuwajibika kwa kiongozi wa chama cha mapinduzi wa ngazi yoyote ile.

Unaweza ukaamini kbisa kwamba katika nchi hakuna mtu au taasisi au mhimili ulioko juu ya chama cha mapinduzi.
Ndivyo ilivyo hata wale wakuu wa vyombo vizito wanajua hivyo na ni lazima watekeleze hayo.
 
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia ya kumsemea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

Tujiulize maswali machache?

(1) Makonda anamhoji kamishina wa TRA? au mtumishi wa umma mwenye mamlaka yeyote kwa hadhi gani? wakati mamlaka ya Uteuzi ya mtendaji wa Serikali sio chama cha mapinduzi?

-Mfano: kuna wakati wenyeviti wa CCM walikuwa wanafanya mchezo kama wa makonda wakawa wana waonea madkatari mpaka ikabidi itoke kauli kuwataka viongozi wa chama wasiiingilie majukumu ya taaluma zisizo wahusu kwa sababu wanaleta mkanganyiko.

Vuta Taswira umeajiriwa Tamisemi .TCRA,sijui wapi huko halafu unawajibishwa na katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi? huuu si mzaha unaopitiliza, Job Description haisemi kwamba utawajibika kwa katibu wa CCM inasema utawajibika kwa mamlaka iliyokuteua, hapa elewa neno mamlaka iliyokuteua?

(2) Je, Rais umemkambidhi mamlaka yako Bwana Makonda? Maana anaingilia kila sekta na anatoa maagizo na kuleta mkanganyiko usio na Tija?

Mfano: Mama Samia yeye ni Rais , wa Nchi kiongozi mkuu na M/kiti wa CCM. Akitembelea mradi kwa kofia ya Rais ana mamlaka kamili ya kuwajibisha mtendaji wa serikali kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi. Vivyo hivyo kwa makamu wa Rais , Waziri mkuu na watendaji wakuu wa serikali inaswihi.

(3) Nauliza Tena mama umemtuma Makonda kwenda kuwaruga watendaji wako wa serikali? washike lipi sasa? Vipi waendelee kupokea maagizo ya makonda au watekeleze mahitaji ya J.D za kazi zao?

(4) Nauliza tena mama wewe hauoni kuna mkanganyiko unaenda kutokea kwa watendaji walio chini yako, hauoni huyu anakwenda kuwachonganisha watendaji na mamlaka zao za kuwajibika? ni kweli watendai na mawaziri wafanye presentation ofisi za chama ?

Ndio maana nauliza umemtuma kueneza itikadi ya chama au kuwavuruga watendaji wa seriakli?

Usipoziba ufa utajenga ukuta, nashauri tu aendelee kukisemea chama ila ajiweke mbali na shughuli za serikali, huyu mtu atabeba majukumu ya cheo chako kwa kivuli kukisemea chama kukusemea wewe Mh. Rais na mwishowe watendaji wataaacha kufanya kazi. Nchi ilikuwa imetulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.
Mambo ya 4Rs.
 
Back
Top Bottom