Makonda asisitiza uwajibikaji

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,399
3,916
đź“Śđź“ŚMAKONDA ASISITIZA UWAJIBIKAJI NA KAULI NZURI KWA WATENDAJI WA SERIKALI.

Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda amewataka watendaji wa serikali ya mkoa wa Shinyanga kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo yao.

Mwenezi Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipofika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kahama ili kukagua utekelezaji wa agizo lake alilolitoa jana jumanne la kutaka siku ya leo itengwe kusikiliza kero za wananchi.

Katika maelezo yake Mwenezi Makonda pia amesisitiza watendaji kuwa na kauli na lugha nzuri kwa wananchi ili kuondoa chuki na hasira zisizokuwa na sababu kwa serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi wa ngazi za mikoa na wilaya kuwa na utamaduni wa kusikiliza wananchi badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa kutoka serikali ama kwenye Chama Cha Mapinduzi.

#VitendoVinaSauti
 
Makonda ni mtu hatari, anataka cheo cha mwenezi kiwe na nguvu kuliko cha mwenyekiti au katibu mkuu, nchi nzima imsikilize yeye, kama ambavyo Stalin alilofanya cheo cha katibu mkuu wa CPSU kuwa na nguvu kuliko vyeo vyote USSR.
 
Ujinga mtupu.

Huyu ni sehemu ya genge la wahalifu wanaojiita ccm

Zaidi ya miaka 60 wakishikilia maamuzi yote ya kijamii na kiuchumi wameshindwa kuwapatia Watanzania hata basic social needs kama vile umeme, maji, barabara, elimu.

Mjinga pekee ndiyo atawasikiliza hao majambazi.

Kingine, raia wa Tz punguzeni ujuha.

Unakuta mtu anatokwa jasho anakusikiliza hao wahuni.

Una akili wewe?
 
Back
Top Bottom