Wanabodi Shaloom!
Ninakuomba kama itakupendeza futilia mbali Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili fedha za umma zinazoteketea kuligharamia zitumike kwingine. Ni kitengo cha upigaji.
Nikukumbushe: mwaka 2005 baada ya Jakaya kuingia madarakani ndipo kitengo hiki kiliundwa mahsusi kumpa Salvatory Rweyemamu ulaji kwa kazi kubwa aliyoifanya kumpamba Jakaya na kuwachafua wapinzani wake kupitia gazeti la RAI Nguvu ya Hoja.
Nafasi za Ubunge, Uwaziri, U-DC au RC hazikuonekana "kumtosha" Salva ndipo alipopendekeza kuwepo na Kurugenzi hiyo ili asafiri na Rais popote duniani na posho ya dola 6700 kwa siku kwa kila safari nje ya nchi.
Rais Magufuli alipoingia naye akaridhi kitengo hiki cha upigaji hela za umma akimweka Gerson Msigwa ambaye naye akawaalika "washikaji" wake kujazana hapo bila kazi maalum zaidi ya kupiga hela. Ofisi ina watu 13 lakini uliza kazi ya kila mmoja ni nini?
Magufuli alisambaratisha kitengo cha Jikoni-Ikulu iliyokuwa na watu zaidi ya 100 akisema, "nitapikiwa na mke wangu". Kilikuwa cha upigaji sawa na hii Kurugenzi.
Unajiuliza Rais anaye Katibu wake, Mwandishi wake wa Habari, Mpigapicha, nini kazi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu? Hivi kuandika barua za teuzi na tenguzi ni za kuajiri Mkurugenzi na Idara hewa chini yake? Nini kazi ya Msemaji Mkuu wa Serikali?
Sasa tunaona Msigwa ndiye Msemaji wa Serikali na wakati huo ndiye Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu (Serikali). Huku ni kuchanganya Mawasiliano ndio maana tulishuhudia JPM akikana uwepo wa Covid-19 na Dk. Abbas akikiri kuwepo Corona. Ikulu vs Idara ya Habari MAELEZO.
Fedha za kugharamia Kurugenzi hii zielekezwe kwenye matumizi mengine. Nawasilisha!
#FreedomIsBack