Rais Samia: Sekta binafsi ndiyo itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,829
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).

Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.

“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”

“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”


Alisema Rais Samia

 
Mbona Serikali ya Emirate Dubai inafanya Biashara kwani hao mliowauzia Bandari si ni Kampuni ya Serikaki DP Dubai hata Kampuni za China mlizowapa Bagamoyo ni za Serikali pia, huyu raisi wenu aisee, duh, mnakodisha Qatar Airways Serikali nzima kwenda USA Qatar Airways ni za Serikali pia, …
 
Siku zote ana majibu ya kukaririshwa, na akishasema hivyo ndio kamaliza..

Mpaka atakaporudi kwa mabosi wake awaulize kesho aseme nini tena!.

Kwake muhimu ni kutoa kila kitu kwa sekta binafsi, huku hata hiyo mikataba wanayoingia serikali yake na hiyo sekta binafsi ya shemeji zake akiwa haijui!.

Aisee tuna hasara!.
 
Back
Top Bottom