Rais Samia ni zaidi ya mzalendo wa kweli

octi

New Member
Aug 27, 2019
3
4
Nimetafakari kwa kina kwa nilichokiona kikitokea juzi kwenye mkutano wa Mkuu Wa nchi na vyama vya kumuonyesha changamoto zilipo ni KITU CHA KIUNGWANA NA HESHIMA KUBWA .

Mwanamke huyu Mkuu Wa nchi kwanza ni HODARI SHUJAA SHUPAVU MSTAHIMILIVU NA MWENYE ROHO YA KIPEKEE kitendo ambacho binadamu wa kawaida mwana CCM na Mtanzania Jamii ya Kiafrika KAMWE SII RAHISI NEVER EVER kukubali KUAMBIWA AMEKOSEA MAHALI.

Mwanzoni nilikuwa na mashaka kuwa may be akili za Mkuu wetu wa nchi ziko mikononi mwa mmoja wa wajanja na wakongwe waliowahi kuwa wakuu katika taasisi hiyo ya Urais lakini nachelea kusema HAPANA.

Mama anatumia akili za kisomi na kibinaadamu zaidi kuliko nguvu za kiutawala na cheo alichonacho.

Hebu fikiri katika dunia hii na katika nafasi TAMU NA YA JUU KAMA Urais pamoja na changamoto zake mbalimbali Nani YUKO TAYARI KUKOSOLEWA ASITUNISHE MISULI?

KAMA JESHI, POLICE na vyombo vingine vya usalama viko chini Yako lazima utagadhabiaka na kuchukua maamuzi yasiyokuwa ya busana pale unapokosolewa.

Maamuzi ya mwenda zake kuzuia mikutano ya hadhara ilikuwa ni KUOGOPA KUKOSOLEWA NA KUAMBIWA UKWELI KUHUSU SEREKALI ALIYOIONGOZA.

Wapendwa niombe radha kuwa Sina nia mbaya kwa kauli yangu hiyo kwa mwendazako HAPANA ila najaribu kuonyesha utofauti wa UTAWALA ULIOPITA NA ULIOPO.

Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni Mh SAMIA SULUHU HASSAN anaROHO ya KIPEKEE, ana HOFU YA MUNGU na nahisi akipata nafasi ya dakika 2 ya kusoma mstari huu atakiri kuwa toka azaliwe na kuwa mama mwenye Roho ya umama HAJAWAHI KUSHUHUDIA AU KUPITIA MAUMIVU MAKALI NA KADHIA ZENYE MAJOZI KAMA ALIZOPITIA AKIWA MAKAMO WA RAIS...... Mmmmh kama namuona jinsi kashtuka kwa aliyoyaona ndotoni yaliyokuwa yakitokea wakati ule... POLE MAMA YANGU yameshapita hebu tenda wema na Mungu alie sirini atakujaza Baraka zake.

Kwa mtazamo wangu nafikiri Mkuu wetu wa nchi kila anachokiamua kwa sasa ni fadhila anazoamua kuzikarimu kwa wa Tanzania ili kuwafata machozi ya vipigo walivyovipata toka kwenye serekali iliyopita.

Japokuwa binadamu hatuna fadhila hata tufadhiliwe vipi haturidhiki ila MAMA tunazidi kukuomba kila penye korongo au mlima ukapate nguvu ya kusawazisha na Mungu akutie nguvu na uhodari wa vita wa kufanya maamuzi mengine mazito na mapana zaidi ya Haya ya kukutana na vyama vya siasa hata kama wana CCM wenzako watakunyooshea vidole usiogope kwani Mungu yuko pamoja nawe na hutashindwa kwa lolote.

Mwisho ila Sii kwa umuhimu nikuombe MAMA hebu kuwa na utamaduni wakuwatuma wasaidizi wako kwenye kila mikoa kuchunguza utendaji kazi wa kila taasisi zako za kiserekali kuhakikisha wanawajibika ipasavyo na sii vinginevyo

Hii itazidi kukujengea heshima Kubwa katika taifa ambalo walisema MWANAMKE HAWEZI KUTUONGOZA.

JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LIMEKUWA JIWE KUU LA MSINGI.

NAWASALIMU KWA JINA LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA . KAZI IENDELEE

2:30 midnight
DAAAAH KWELI NI USIKU WA MANANE

WAPENDWA HUO NI WANGU MTAZAMO TUU MSIJENGE CHUKI... ngoja nilale....
 
IMG-20230104-WA0110.jpg
 
Back
Top Bottom