Rais Samia: Mungu kanipa mtihani si haba

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kwa nafasi aliyopewa, Mwenyezi Mungu amempa mtihani si haba.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 - Hijiria.

“Mungu kanipa mtihani si haba, pale aliponiweka, na ukisikiliza ya watu Samia Suluhu yule mmm…mtihani si haba nilio nao, nijiusie nafsi yangu kwanza, na niwausie na wengine, wote tushiriki na wote tuige mifano mizuri tunayooneshwa na viongozi wa dini hasa kutumia njia bora na hekima katika kuendesha maisha yetu.

“Tulioshika madaraka tuwe thabiti, tuwe na hekima katika kutoa maamuzi, sio unapewa dhamana husikilizi wengine, mtu anakuja na shida zake fulani msikilize huyo, kuweni wastarabu, sio kuweka mabega juu kama mizani ukipewa madaraka wanaume koti zinaninginia, wanawake shungi zipo sivyo,” amesema.
 
Imefanyiwa uwekezaji mkuu. Haijauzwa na jitahidi kuacha kuburuzwa na CHADEMA na kanisa kijana.

Hivi mbona mkibanwa kuwa mtoe maelezo vizuri kuhusu bandari, mnakwepa hoja na kuingiza mambo ya vyama?
Leteni majibu ya hoja zinazotolewa na si kutukana na kutoa majibu marairaisi.

Kama huu mkataba ukipita kwa namna ulivyo, basi hakuna chama wala mwananchi atakaye salimika. Cunsequences huu mkataba zitawapata wote
 
Hakuna hoja hapo. Waarabu wakaribie upesi watuboreshee bandari na ulinzi tutawapa basi.
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kwa nafasi aliyopewa, Mwenyezi Mungu amempa mtihani si haba.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 - Hijiria.

“Mungu kanipa mtihani si haba, pale aliponiweka, na ukisikiliza ya watu Samia Suluhu yule mmm…mtihani si haba nilio nao, nijiusie nafsi yangu kwanza, na niwausie na wengine, wote tushiriki na wote tuige mifano mizuri tunayooneshwa na viongozi wa dini hasa kutumia njia bora na hekima katika kuendesha maisha yetu.

“Tulioshika madaraka tuwe thabiti, tuwe na hekima katika kutoa maamuzi, sio unapewa dhamana husikilizi wengine, mtu anakuja na shida zake fulani msikilize huyo, kuweni wastarabu, sio kuweka mabega juu kama mizani ukipewa madaraka wanaume koti zinaninginia, wanawake shungi zipo sivyo,” amesema.
Yeye mbona ndiyo tabia yake,alikuja Mwanza kuna Mama alipiga yowe,akitaka kuongea na yeye,Samia akasema atasikilizwa na viongozi wa Wilaya.Pia wakati wa Meimosi kuna mtu alitaka kuongea naye akaagiza atolewe nje.Sasa huo wosia ni kinafiki!
 
Sawa bwana chauongo.
 
Wrwe unachukia waswahili? Sasa kaa kwavkutuliabwatafululiza kukutawala kamavifuatavyo:
1. Mama mpaka 2030.
2. Hussein Mwinyi mpaka 2040.
3. January Makamba mpaka 2050.
Ridhiwani Kikwete mpaka 2060.
Umeelewa dogo?
Haya yatatokea kwenye nchi ya kusadikika siyo Tanzania.
 
Back
Top Bottom