Rais Samia: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na mustakabali kusonga mbele

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan:

Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.

Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu

Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao

Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye.

Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba.

Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema "Zidumu Fikra za Mwenyekiti". Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema "acha maua 100 yamee kwa pamoja".

Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari hii. Viongozi wa CCM na Serikali walioona umuhimu wa kuruhusu vyama vingi kabla vita na vurugu havijatulazimisha, na wanaharakati na wasomi waliokuwa wakisaidia kutuonesha kuwa tunatakiwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi

Hata hivyo, yatakuwa makosa makubwa kama tutaona kuwa kazi ile imemalizika. Naamini, sasa tunapita katika mazingira yale yale magumu yaliyokuwapo wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi. Kuna vita katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwaqmo kwenye nchi zilizoendelea, mfumo wa kidemokrasia wa kiliberali unapitia katika changamoto na nchikubwa zinapambana kuwania kutawala Dunia. Ni changamoto ambazo

Viongozi wa kizazi chetu wanatakiwa kuzivuka kama walivyofanya watangulizi wangu. Ndiyo sababu kwenye uongozi wangu, naamini katika kile kinachojulikana kama 4R - ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya).

Maridhiano Katika tamthilia maarufu ya karne ya 19 ya Lolanthe, waandishi Gilbert na Sullivan walieleza jambo moja kuhusu Taifa la Marekani wakati huo; "kila anayezaliwa ni ama mtoto mhafidhina au mtoto mliberali", Mimi siamini kwenye misimamo ya namna hii. Kwamba mwanadamu, awe mwanasiasa, kiongozi au mwananchi wa kawaida, kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu

Mambo yenye maslahi kwa Taifa. Msimamo au hali Fulani inaweza kueleweka au kukubalika wakati Fulani lakini si wakati wote. Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana. Kwenye kujenga Tanzania bora natamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Natamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.

Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote. Ninaamini maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale, ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.

USTAHIMILIVU
Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ujenzi wa Taifa si lelemama, Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi wananchi na viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu.

Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinzoikumba Dunia, kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamiii, kisiasa, lakini ni lazima tujenge ustahimilivu. Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana namna walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee

MABADILIKO
Kuna usemi mmoja maarufu, kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika. Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa a lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache. Kujenga upya Ninafahamu, kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamilivu wala mabadiliko. Mwisho wa siku kama walivyofanya watangulizi wangu wengine kwenye karne hii, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii, yaliyo nchini.

Tayari tunaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini

Na nishati. Juhudu zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour, zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na Uviko-19. Katika kilimo tunakwenda kufanya mabadiliko mengine makubwa ili sekta kubwa ya miundombinu na mengine makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu. Ninaamini, kwamba kwa jitihada zetu za R4 tutatimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa, bali kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu.

Hii ndiyo namna bora ya kuendeleza ndoto za waliopigania vyama vingi.

Kazi na iendelee

96FC2A0F-FEBC-41AC-BFE6-C7F0E3A48F37.jpeg
AE6F9AAF-D972-4080-8446-D3925EB38F64.jpeg
85AB1329-2344-41E9-8C98-E129CEB84A5A.jpeg
 
"Ninachojua wananchi hawali maridhiano, ustahimilivu, wala mabadiliko" - SSH.

Hii mentality ndio kila siku wanaenda kukaa nayo ikulu, matokeo yake wakitoka huko tunasikia covid 19 bado wako bungeni Spika anawalinda, na Rais naye yupo kimya hasemi chochote.

Tukisema waondoke kwenye mazungumzo wengine wanasema tuendelee kuwa wavumilivu!, mpaka lini? hiyo mentality itakapobadilika? ok when?

So for now, tuendelee kuvumilia uvunjifu wa sheria wa makusudi mpaka hiyo mentality itakapobadilika, complete wastage of time!.

Generally nilivyomsoma Samia kwenye hiyo makala yake, kwake kukuza uchumi ndio jambo la msingi zaidi, lakini hayo maridhiano huwa anapitisha muda tu ili kuwaliwaza wale wenye kiu nayo.

Ukweli ni kwamba, hana nia ya dhati ya mabadiliko kama walivyo CCM wenzake, na yale mawazo ya Katiba Mpya na mengine ni usanii mtupu, wataleta igizo kama lile la 2014 habari iishie hapo.

Mabadiliko ya kweli yataletwa na watanzania wenyewe siku watakapoamua.
 
Uchambuzi makini sana.

Mwaka 1992 CCM ilikuwa na umri wa miaka 15,lakini leo vyama vingi vina umri wa miaka 30.

Ni jambo jema lilifanyika kipindi kile kwa wachache kupewa nafasi,hata hivyo ni wajibu kwa Vyama vingi kufanya tathmini ya miaka 30 kulinganisha na miaka 15 ya Wakati ule kwa CCM.
 
Take my words Rais Samia anaweza kuwa Best President Ever wa nchi hii,na angeukuta Uchumi haujaharibiwa angeweka Historia ya pekee Afrika na kuliliwa na kila mtu siku akiondoka hapa Duniani.
 
Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.

Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu

Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao.

Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye. Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba.

Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema "Zidumu Fikra za Mwenyekiti". Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema "acha maua 100 yamee kwa pamoja".

Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari hii. Viongozi wa CCM na Serikali walioona umuhimu wa kuruhusu vyama vingi kabla vita na vurugu havijatulazimisha, na wanaharakati na wasomi waliokuwa wakisaidia kutuonesha kuwa tunatakiwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, yatakuwa makosa makubwa kama tutaona kuwa kazi ile imemalizika. Naamini, sasa tunapita katika mazingira yale yale magumu yaliyokuwapo wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi. Kuna vita katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwaqmo kwenye nchi zilizoendelea, mfumo wa kidemokrasia wa kiliberali unapitia katika changamoto na nchikubwa zinapambana kuwania kutawala Dunia. Ni changamoto ambazo viongozi wa kizazi chetu wanatakiwa kuzivuka kama walivyofanya watangulizi wangu.

Ndiyo sababu kwenye uongozi wangu, naamini katika kile kinachojulikana kama 4R - ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya).

MARIDHIANO

Katika tamthilia maarufu ya karne ya 19 ya Lolanthe, waandishi Gilbert na Sullivan walieleza jambo moja kuhusu Taifa la Marekani wakati huo; "kila anayezaliwa ni ama mtoto mhafidhina au mtoto mliberali", Mimi siamini kwenye misimamo ya namna hii. Kwamba mwanadamu, awe mwanasiasa, kiongozi au mwananchi wa kawaida, kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu mambo yenye maslahi kwa Taifa. Msimamo au hali Fulani inaweza kueleweka au kukubalika wakati Fulani lakini si wakati wote. Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana. Kwenye kujenga Tanzania bora natamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Natamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.

Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote. Ninaamini maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale, ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.

USTAHIMILIVU
Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ujenzi wa Taifa si lelemama, Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi wananchi na viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu.

Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinzoikumba Dunia, kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamiii, kisiasa, lakini ni lazima tujenge ustahimilivu. Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana namna walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee.

MABADILIKO
Kuna usemi mmoja maarufu, kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko. Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika. Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa a lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.

KUJENGA UPYA

Ninafahamu, kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamilivu wala mabadiliko. Mwisho wa siku kama walivyofanya watangulizi wangu wengine kwenye karne hii, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii, yaliyo nchini.

Tayari tunaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini na nishati. Juhudu zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour, zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na Uviko-19. Katika kilimo tunakwenda kufanya mabadiliko mengine makubwa ili sekta kubwa ya miundombinu na mengine makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu.

Ninaamini, kwamba kwa jitihada zetu za R4 tutatimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa, bali kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu. Hii ndiyo namna bora ya kuendeleza ndoto za waliopigania vyama vingi.

Kazi na iendelee
 
Attachments

  • 4 (8).jpg
    830.7 KB · Views: 34
Noble Price Laureate! Yuki vizuri sana. Ila tusianye kuwaenzi viongozi waliopita ila kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho. Pi kwa matakwa mapana ya dunia hii, twende na dunia, vinginevyo tunaachwa kwa mbali.

Ni kweli na ndio maana hata yeye kwenye hii makala ametambua mchango wa watangulizi wake na kusema kwamba ataendeleza yale yote yalioanzishwa na kuachwa.
 
Mawazo ni mazuri ila tatizo ni lile kokolo(CCM) na watu waliomzunguka wamejaa uhafidhina,ataweza.Hili hii nchi isonge mbele ni lazima adhibiti ufisadi serikalini na asifumbie macho wakwepa kodi,kauli za kusema waliokuwa wanadaiwa Kodi miaka ya nyuma wasilipe bali walipe mwaka mmoja nyuma,zife.Sheria iwekwe mbele ya ukada na kujuana.
✓Uteuzi uzingatie sifa stahiki na siyo ukada ambao umesababisha watu wenye Brain nzuri kuachwa na mfumo wakizagaa mtaani na kukumbatia vilaza kwenye taasisi za serikali.
✓Kingine aache kuteua wazee maana mbwa mzee awezi kujifunza mbinu mpya.Kama anawahitaji aunde Baraza la Rais la ushauri.
✓Akemee kauli za kibaguzi za kina Nape ambao wanaona CCM na nchi hii mali yao.Kauli za kusema wenye chama tumerudi,mara wana-CCM wengine kuitwa viroboto kwasababu ya kutofautiana mtazamo,hizi kauli za kibaguzi zife.
✓Ahakikishe wanasiasa wote waliofungwa kwa kesi za kisiasa wanaachiwa huru bila masharti.
✓Ahakikishe maoni ya Wananchi yaliyotolewa kwenye Rasmu ya katiba ya Warioba ndiyo yanaheshimiwa na mchakato uanzie kwenye Rasimu ya Warioba na siyo kwenye Rasimu iliyotokana na mgawanyiko wa wanasiasa katika Bunge la Katiba.
✓Bunge la Katiba liundwe upya na lisiwe na sura ya kisiasa kama la awali ambapo liligeuzwa Bunge la Muungano na kuongeza uwakilishi mwingine kwa uchache.Inatakiwa makundi yote ya kiraia yapate uwakilishi na si Kama awali.
✓Watu wote ambao wanahusishwa na tuhuma za ufisadi au wameshawahi kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi,iwe ni marufuku kujihusisha na utumishi wa umma ama kugombea nafasi za uongozi wa nchi.
✓Jeshi la Polisi nalo lifumuliwe na kusukwa upya maana taswira yake si nzuri machoni pa watanzania waliowengi,na Askari wote ambao uadilifu wao unatiliwa mashaka na jamii waondolewe kwenye jeshi.
Tukifanya haya machache na mengine wataongezea wengine,4R itakuwa na maana pana sana.
 
Kusema rahisi sana ila shughuli ipo ktk kutenda,nikikumbuka namna mzee wa msoga alivyomwaga ugali wa katiba mpya cna hamu
Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan:

Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.

Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu

Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao

Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye.

Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba.

Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema "Zidumu Fikra za Mwenyekiti". Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema "acha maua 100 yamee kwa pamoja".

Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari hii. Viongozi wa CCM na Serikali walioona umuhimu wa kuruhusu vyama vingi kabla vita na vurugu havijatulazimisha, na wanaharakati na wasomi waliokuwa wakisaidia kutuonesha kuwa tunatakiwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi

Hata hivyo, yatakuwa makosa makubwa kama tutaona kuwa kazi ile imemalizika. Naamini, sasa tunapita katika mazingira yale yale magumu yaliyokuwapo wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi. Kuna vita katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwaqmo kwenye nchi zilizoendelea, mfumo wa kidemokrasia wa kiliberali unapitia katika changamoto na nchikubwa zinapambana kuwania kutawala Dunia. Ni changamoto ambazo

Viongozi wa kizazi chetu wanatakiwa kuzivuka kama walivyofanya watangulizi wangu. Ndiyo sababu kwenye uongozi wangu, naamini katika kile kinachojulikana kama 4R - ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya).

Maridhiano Katika tamthilia maarufu ya karne ya 19 ya Lolanthe, waandishi Gilbert na Sullivan walieleza jambo moja kuhusu Taifa la Marekani wakati huo; "kila anayezaliwa ni ama mtoto mhafidhina au mtoto mliberali", Mimi siamini kwenye misimamo ya namna hii. Kwamba mwanadamu, awe mwanasiasa, kiongozi au mwananchi wa kawaida, kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu

Mambo yenye maslahi kwa Taifa. Msimamo au hali Fulani inaweza kueleweka au kukubalika wakati Fulani lakini si wakati wote. Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana. Kwenye kujenga Tanzania bora natamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Natamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.

Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote. Ninaamini maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale, ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.

USTAHIMILIVU
Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ujenzi wa Taifa si lelemama, Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi wananchi na viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu.

Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinzoikumba Dunia, kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamiii, kisiasa, lakini ni lazima tujenge ustahimilivu. Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana namna walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee

MABADILIKO
Kuna usemi mmoja maarufu, kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika. Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa a lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache. Kujenga upya Ninafahamu, kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamilivu wala mabadiliko. Mwisho wa siku kama walivyofanya watangulizi wangu wengine kwenye karne hii, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii, yaliyo nchini.

Tayari tunaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini

Na nishati. Juhudu zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour, zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na Uviko-19. Katika kilimo tunakwenda kufanya mabadiliko mengine makubwa ili sekta kubwa ya miundombinu na mengine makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu. Ninaamini, kwamba kwa jitihada zetu za R4 tutatimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa, bali kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu.

Hii ndiyo namna bora ya kuendeleza ndoto za waliopigania vyama vingi.

Kazi na iendelee
View attachment 2278102
View attachment 2278096
 
madam President anastahili pongezi kwa makala yake yenye maono haya mambo ya kuandika alifanya Mzee Nyerere na Mkapa viongozi wengi wenye maono huandika....Fidel Castro...Nkurumah...Mandela...Samora na wengine wa calibre hiyo...waliandika sana
 
Makala yenye maono?
Nchi hii ina majuha mengi
 
Back
Top Bottom