Rais Samia mama wa haki, hekima na busara

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Tangu Tarehe 19 Machi alipoapishwa kuwa Rais wa Awamu ya sita kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa ni kama mwanzo wa matumaini, nguvu mpya, maisha mapya na heshima kwa Taifa la Tanzania.

Rais Samia alikula kiapo cha Utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalitendea wema Taifa hili kadiri Mwenyezi Mungu anavyomjalia heri na Baraka.

Kwa Mara ya kwanza Taifa likampata Jasiri na shujaa mwenye shauku ya kuliongoza vyema Taifa hili shauku ya kupigania maendeleo na usawa wa kijinsia.

Tangu kuapa kwake aliweka msisitizo ukusanyaji wa kodi kimabavu ufike kikomo, Aliwaamuru watoza ushuru wa TRA kipi kisichowezekana kumalizika mezani..? Hili lilimuongezea wafuasi kuleta imani kwenye Biashara yawezekana Biashara kufanyika na kodi kukusanywa bila kushikiana mtutu wa Bunduki.

Alikabidhiwa nchi angali ugonjwa wa UVIKO 19 unasumbua, Biashara zimesimama na vilio vya kina Mama juu ya ukosefu wa huduma bora za Afya na mitaji kwa Vijana kila kona. Haya yote kwake yanabakia kuwa historia.

Hajarithi mfumo wa mabavu, amejaliwa Busara nchi imetulia na vilio vya bring back our people slogan zilizotapaka kila kona enzi za sipangiwiiii siku hizi ni hazipo mtaani.

Tunamkabidhi bendera ya HEKIMA, UTU na BUSARA ametatua vilio vyetu kupitia kauli za R nne kwa ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza yaani maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya, ni ahadi ambazo amezitekeleza kwa matendo. Asante sana Mama, kesho kwa Mungu una hesabu yako daraja la juu.

Ameondoa zuio haramu la mikutano ya hadhara ikiwa ni kutekeleza matakwa ya Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa.

Ameunda tume ya ukweli, juu ya haki na usuluhishi ambayo itasikiliza na kuchunguza masuala yote ya uvunjaji wa haki za binadamu na utawala bora na kuwezesha hatua za ziada kuchukuliwa zenye kufungua ukurasa mpya katika nchi.

Ameibeba agenda ya mabadiliko amesema wazi muda si mrefu madai ya katiba mpya yatapatiwa ufumbuzi, sheria mpya ya vyama vya siasa na mageuzi katika Jeshi la Polisi haya yanaendelea kufanyika kufikia kiasi Polisi wameomba wataniwe na wananchi wakiona gari la Polisi waombe lifti.

Hakuna Siasa Safi bila kuwa na Uongozi bora wenye kujali Uchumi wa Vijana wake, Ni wakati huu ambapo kuna matukio makubwa mawili Rais Samia ameyaona yataleta faida na hamasa kwa Vijana ni kutoa ruhusa kwa biashara mpya zote zinazoanza ndani ya miezi sita hadi Mwaka wasilipe Kodi. Je Vijana mna deni na Rais Samia? Wanangu tuchapeni kazi nyinyi si ndiyo mkiumwa ukoo mzima unaumwa wakati wenu huu kutoboa.

Hii ni siku moja baada ya Mhe. Rais kutoka kwenye kongamano la siku ya Wanawake lilioandaliwa na baraza la Wanawake Chadema yaani BAWACHA hii ni historia nyingine katika nchi yetu Mwenyekiti wa CCM kuhudhuria mkutano wa chama kikuu cha Upinzania kama mgeni Rasmi. Ile nchi ya kusadikika ya asali na Maziwa kwenye ndoto ndiyo Tanzania ya Samia tunayoishi leo.

Mambo mengi ambayo Rais Samia anayatekeleza ni kwa uwazi na ukweli, hususan suala la maridhiano na utulivu wa kisiasa. Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiona mfumo wa vyama vingi kama ugomvi au vita vya kugombania madaraka baina ya vyama vya siasa. Kwa Rais Samia hali ni tofauti kabisa ameketi nao mezani na kuzungumza pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani.

Rais Samia anataka maridhiano na ustahimilivu ni vitu vya msingi na ni kweli, tulikuwa tunakwenda vizuri, baadaye tukarudi nyuma demokrasia ilikuwa haipo kabisa, Kimsingi ametumia hekima kuliweka Taifa kwa pamoja tena, Mungu ambariki zaidi Amiin.

Awamu ya Tano Tanzania ilishuka kwa kiasi kikubwa katika uwanja wa diplomasia na hiyo ilisababishwa na kuminywa kwa demokrasia nchini, huku nchi ikibaki kuwa kama ya chama kimoja. Hatukuwa na Uhuru wa kukusanyika wala uhuru wa vyombo vya Habari.

Rais Samia aliingia madarakani akiwa na mfumo mpya ambapo amefungua Anga kwa kutembelea nchi zote zinazohusudu demokrasia, amehudhuria vikao vingi vya wakuu wa nchi mbalimbali, ikiwemo mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (Unga) na mingine akituma wawakilishi. Ameileta Tanzania kwenye ramani yake kama Mama wa diplomasia.

Ameonyesha Uhuru wa kisiasa na tayari kuna wananchi wanashiriki katika masuala ya kisiasa bila woga na ndiyo inaleta maana ya demokrasia ya vyama vingi,. Chadema wanakusanyika, ACT wanakusanyika na hoja zitatupwa huku na kule Vijana makini wa CCM tunazipangua kama Djugui Diara mdaka mishale. Utamu wa siasa hoja.

Ni wazi kama nchi inakosa uhuru wa kisiasa kwenye uchumi, watu wengi wataogopa kuja kuwekeza, nchini kwako, angalia Somalia, Congo, Eritrea, Chad, Mali huwezi kuona watu wanakwenda kuwekeza huko wakati hawana uhakika, hivyo hiki kinachofanywa na Rais Samia ni kuhakikisha nchi inajijenga kiuchumi. Tumpongeze kwa sheria mpya ya Uwekezaji. Kesho yetu ni njema china ya Mama.

Tunakuombea Dua usiku na mchana mwanzo mwisho.
 
FB_IMG_1675375753319.jpg
 
Mchele shs 4000 kilo

Walamba asali mmeshiba sana..mnakuja kupumulia huku...mkaandike hizi vitu Facebook mpige na selfie...
 
Haki za mashoga
 
Back
Top Bottom