Rais Samia, kataa ombi la Jenerali Venance Mabeyo kustaafu

Tufuate sheria kama umri umefika ni muhimu akastaafu.

Hii tabia ya kuongeza muda wa kustaafu huku vijana wakiozea mitaani ni ujinga na upumbavu.

Tanzania ni kubwa na wapo wajeda kibao ambao wana sifa na uwezo wa kuongoza JWTZ.
Wapo wajeda wengi wenye uwezo wa kuongoza JW akiwemo Luteni Urio.....😅😅. Hivi Urio yuko wapi sasa? Stori zake zinataka kuyeyuka kimyakimya.
 
Umeandika kitu gani,yaani umejikunja mda wote huo kuleta upuuzi wako huu
Ovyo!usinitafte la rohoni
 
duh!! mtoto wa mabeyo hutaki baba aachie ngazi? au unamashaka na ratiba za Ugali wa hapo nyumbani kuporomoka?

Ondoa shaka hata mzee akistaafu, ratiba ya Ugali ipo palepale, alishazikusanya za kutosha.
 
Amestaafu Mwamunyage
Amestaafu Msuguri
Amestaafu Mboma.

Wamestaafu maafsa wengi sana huki JWTZ...kustaafu kwake ndio mwanzo wakuja mwingine..
 
Hakuna mwenye hati miliki na Taasisi yoyote ya umma nchi hii. Ukifika wakati wa kuwapisha wengine huna budi kufanya hivyo. Jeshi lina viongozi wenye weledi wa kutosha ambao, mmoja wao akipewa hiyo nafasi nina hakika ataimudu.

Remember:
No matter how good you are, you can always be replaced!

Hakuna mtu mwema na muadilifu mmoja hapa tz wapo wengi tuu tusiongozwe na hisia , furaha ya mida mfupi au huzuni ya temporary tufute matakwa ya sheria tafadhal
 
Tz ina wajeda wa kutosha wenye izo sifa akae kando wengine washike jahazi
 
Nimeangalia video ambayo Mkuu wa majesho yetu, Jenerali Venance Mabeyo akiongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ujenzi wa moja ya parokia ya Kanisa Kaoliki, nadhani ni ya Kawe kama sijakosea.

Katika misa na hafla ile Generali Mabeyo aliwaongoza vizuri sana wanajeshi wenzake wakachangia fedha nyingi sana. Wanajeshi wakajitoa, siyo kwa sababu bosi wao kasema bali kama wanaompenda.

Shughuli ile iliongozwa na mmoja wa maaskfou ambao sikumshika jina lake.

Kikubwa kwangu siyo shughuli yenyewe ya kikanisa bali ni hotuba aliyotoa Jenerali Mabeyo. Katika hotuba yake amesema hata yeye sasa hivi amekaribia kuitwa mstaafu yaani amebakiza miezi takribani minane.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kufikia January 2023 Jenerali Venance Mabey atakuwa amestaafu na hivyo tutakuwa na Mkuu wa Majeshi mwingine.

Chondechonde Jenerali Mabeyo. Kama ulikuwa huju basi huku mitandaoni na mtaani kuna watu tulikupenda kuliko unavyojijua. Hatutaki kamwe kusikia hilo neno kustaafu. Unastaafu ili iweje. Bado una nguvu za kufanya kazi na kikubwa ni kwamba tunakupenda.

Tunajua uadilifu wako. Tunajua uchapakazi wako. Wewe ni mmoja wa wanajeshi wachache walio hai waliopigana vita ya kumuondoa Idi Amini pale Kagera na kumuondoa kabisa Uganda. Kuwepo kwako kama Mkuu wa Majeshi walau kunatukumbusha hilo.

Sasa unasema unaondoka, inawezekana umri umefikia. Lakini kwa kuwa tunakupenda na umeanza kusemasema unaondoka basi sisi tunaokupenda tunakuandika mitandaoni kwamba htatutaki uondoke.

Bado tunapenda uwepo. zipo tetesi kadhaa zinasema ulifanya kazi nzuri isiyosahaulika wakati Rais Magufuli anafariki na hadi Rais Samia kutangazwa kuwa Rais wa Tanzania.

Sasa unaondoka, kaa ukijua kwamba kazi ya mitandao siyo kuikosoa serikali tu bali hata kukosoa watu kamawewe mnaoondoka wakati tunawapenda.

Maadam umesema tunakujua kwamba ukishasema hurudi nyuma. Sasa tunachofanya ni kuandika hivi mitandaoni iliRais Samia akuongezee miaka mingine ikibidi mitano zaidi tuendelee kuona alama yako.

Siyo kwamba anakosekana mwanajeshi mwingine kuchukua nafasi yako, bali jua kwamba tupo tunaokupenda na hili si jamba la ajabu. Majaji wengi wakifikia umri miaka 65 hasa Mahakama ya Rufani wanastaafu lakini Rais anawaongezea muda.

Tumeona wengi wastaafu wanapewa uongoziwa bodi kadhaa. Hapana wewe hatukutaki kwenye bodi, tunakutaka bado uendelee kuwa CDF wetu.

Andiko langu hili linawakilisha mimi na yeyote anayekupenda. Hata Nyerere alipoangaza kustaafu mwaka 1980 watu wakamkatalia ikabidi aende hadi mwak 1985.

Hata mtangulizi wako Jenerali Davis Mwamunyange alipofikisha miaka fulani akataka kustaafu Rais Magufuli akakataa akasema asubiri na hadi ukapita mwaka mmoja.

Ombi kwa Rais Samia, kata katakata kustaafu kwa Jenerali Venance Mabeyo mwaka huu. Mwache aendelee kuwa Mkuu wa Majeshi ikibidi hadi baada ya 2025.

Wenu Mwanajamii
Sukuma gang mnachekeshaaa,mnajifanya wajanjaaaaa !!
 
Mabeyo Kishafikia umri wa Kustaafu tokea 2019.
Ni Mzee ambaye chini yake, Nchi imekuwa na Magenge ya Watekaji, Wasiojulikana, na watu Kupigwa risasi hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom