Rais Samia, kataa ombi la Jenerali Venance Mabeyo kustaafu

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Nimeangalia video ambayo Mkuu wa majesho yetu, Jenerali Venance Mabeyo akiongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ujenzi wa moja ya parokia ya Kanisa Kaoliki, nadhani ni ya Kawe kama sijakosea.

Katika misa na hafla ile Generali Mabeyo aliwaongoza vizuri sana wanajeshi wenzake wakachangia fedha nyingi sana. Wanajeshi wakajitoa, siyo kwa sababu bosi wao kasema bali kama wanaompenda.

Shughuli ile iliongozwa na mmoja wa maaskfou ambao sikumshika jina lake.

Kikubwa kwangu siyo shughuli yenyewe ya kikanisa bali ni hotuba aliyotoa Jenerali Mabeyo. Katika hotuba yake amesema hata yeye sasa hivi amekaribia kuitwa mstaafu yaani amebakiza miezi takribani minane.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kufikia January 2023 Jenerali Venance Mabey atakuwa amestaafu na hivyo tutakuwa na Mkuu wa Majeshi mwingine.

Chondechonde Jenerali Mabeyo. Kama ulikuwa huju basi huku mitandaoni na mtaani kuna watu tulikupenda kuliko unavyojijua. Hatutaki kamwe kusikia hilo neno kustaafu. Unastaafu ili iweje. Bado una nguvu za kufanya kazi na kikubwa ni kwamba tunakupenda.

Tunajua uadilifu wako. Tunajua uchapakazi wako. Wewe ni mmoja wa wanajeshi wachache walio hai waliopigana vita ya kumuondoa Idi Amini pale Kagera na kumuondoa kabisa Uganda. Kuwepo kwako kama Mkuu wa Majeshi walau kunatukumbusha hilo.

Sasa unasema unaondoka, inawezekana umri umefikia. Lakini kwa kuwa tunakupenda na umeanza kusemasema unaondoka basi sisi tunaokupenda tunakuandika mitandaoni kwamba htatutaki uondoke.

Bado tunapenda uwepo. zipo tetesi kadhaa zinasema ulifanya kazi nzuri isiyosahaulika wakati Rais Magufuli anafariki na hadi Rais Samia kutangazwa kuwa Rais wa Tanzania.

Sasa unaondoka, kaa ukijua kwamba kazi ya mitandao siyo kuikosoa serikali tu bali hata kukosoa watu kamawewe mnaoondoka wakati tunawapenda.

Maadam umesema tunakujua kwamba ukishasema hurudi nyuma. Sasa tunachofanya ni kuandika hivi mitandaoni iliRais Samia akuongezee miaka mingine ikibidi mitano zaidi tuendelee kuona alama yako.

Siyo kwamba anakosekana mwanajeshi mwingine kuchukua nafasi yako, bali jua kwamba tupo tunaokupenda na hili si jamba la ajabu. Majaji wengi wakifikia umri miaka 65 hasa Mahakama ya Rufani wanastaafu lakini Rais anawaongezea muda.

Tumeona wengi wastaafu wanapewa uongoziwa bodi kadhaa. Hapana wewe hatukutaki kwenye bodi, tunakutaka bado uendelee kuwa CDF wetu.

Andiko langu hili linawakilisha mimi na yeyote anayekupenda. Hata Nyerere alipoangaza kustaafu mwaka 1980 watu wakamkatalia ikabidi aende hadi mwak 1985.

Hata mtangulizi wako Jenerali Davis Mwamunyange alipofikisha miaka fulani akataka kustaafu Rais Magufuli akakataa akasema asubiri na hadi ukapita mwaka mmoja.

Ombi kwa Rais Samia, kata katakata kustaafu kwa Jenerali Venance Mabeyo mwaka huu. Mwache aendelee kuwa Mkuu wa Majeshi ikibidi hadi baada ya 2025.

Wenu Mwanajamii
 
Kustafu ni muhimu ili kupisha damu changa , kama umri wa kustafu umefika kisheria kwa Nini asistafu, wewe ni nani upinge kustafu kwake. Muhimu kupokezana vijiti na kutengeneza viongozi wapya , mleta uzi ni type ya watulikuo kuwa mnataka jiwe atawale milele hata baada ya mda wake kuisha.
 
Mleta uzi una emotions za kusikitisha sana Ulivyoona michango inatolewa ukasisimkwa mwili wote hadi ukasahau kwamba maisha ni hatua.Maisha ni kupokezana.

Kama si hivyo,Yesu angeondoka duniani akiwa na miaka Mia na hamsini.Is he better than Jesus himself?😂😂😂😂
 
Tufuate sheria kama umri umefika ni muhimu akastaafu.

Hii tabia ya kuongeza muda wa kustaafu huku vijana wakiozea mitaani ni ujinga na upumbavu.

Tanzania ni kubwa na wapo wajeda kibao ambao wana sifa na uwezo wa kuongoza JWTZ.
 
Nimeangalia video ambayo Mkuu wa majesho yetu, Jenerali Venance Mabeyo akiongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ujenzi wa moja ya parokia ya Kanisa Kaoliki, nadhani ni ya Kawe kama sijakosea...
Sheria lazima zifuatwe, kama unampenda sana nenda kawe house boy au girl wake nyumbani kwake ili umuone kila siku. Lazima tuzingatie misingi tuliojiwekea, la sivyo tutakuwa tupo tupo tu bila muelekeo.
 
U
Nimeangalia video ambayo Mkuu wa majesho yetu, Jenerali Venance Mabeyo akiongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ujenzi wa moja ya parokia ya Kanisa Kaoliki, nadhani ni ya Kawe kama sijakosea.

Katika misa na hafla ile Generali Mabeyo aliwaongoza vizuri sana wanajeshi wenzake wakachangia fedha nyingi sana. Wanajeshi wakajitoa, siyo kwa sababu bosi wao kasema bali kama wanaompenda.

Shughuli ile iliongozwa na mmoja wa maaskfou ambao sikumshika jina lake.

Kikubwa kwangu siyo shughuli yenyewe ya kikanisa bali ni hotuba aliyotoa Jenerali Mabeyo. Katika hotuba yake amesema hata yeye sasa hivi amekaribia kuitwa mstaafu yaani amebakiza miezi takribani minane.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kufikia January 2023 Jenerali Venance Mabey atakuwa amestaafu na hivyo tutakuwa na Mkuu wa Majeshi mwingine.

Chondechonde Jenerali Mabeyo. Kama ulikuwa huju basi huku mitandaoni na mtaani kuna watu tulikupenda kuliko unavyojijua. Hatutaki kamwe kusikia hilo neno kustaafu. Unastaafu ili iweje. Bado una nguvu za kufanya kazi na kikubwa ni kwamba tunakupenda.

Tunajua uadilifu wako. Tunajua uchapakazi wako. Wewe ni mmoja wa wanajeshi wachache walio hai waliopigana vita ya kumuondoa Idi Amini pale Kagera na kumuondoa kabisa Uganda. Kuwepo kwako kama Mkuu wa Majeshi walau kunatukumbusha hilo.

Sasa unasema unaondoka, inawezekana umri umefikia. Lakini kwa kuwa tunakupenda na umeanza kusemasema unaondoka basi sisi tunaokupenda tunakuandika mitandaoni kwamba htatutaki uondoke.

Bado tunapenda uwepo. zipo tetesi kadhaa zinasema ulifanya kazi nzuri isiyosahaulika wakati Rais Magufuli anafariki na hadi Rais Samia kutangazwa kuwa Rais wa Tanzania.

Sasa unaondoka, kaa ukijua kwamba kazi ya mitandao siyo kuikosoa serikali tu bali hata kukosoa watu kamawewe mnaoondoka wakati tunawapenda.

Maadam umesema tunakujua kwamba ukishasema hurudi nyuma. Sasa tunachofanya ni kuandika hivi mitandaoni iliRais Samia akuongezee miaka mingine ikibidi mitano zaidi tuendelee kuona alama yako.

Siyo kwamba anakosekana mwanajeshi mwingine kuchukua nafasi yako, bali jua kwamba tupo tunaokupenda na hili si jamba la ajabu. Majaji wengi wakifikia umri miaka 65 hasa Mahakama ya Rufani wanastaafu lakini Rais anawaongezea muda.

Tumeona wengi wastaafu wanapewa uongoziwa bodi kadhaa. Hapana wewe hatukutaki kwenye bodi, tunakutaka bado uendelee kuwa CDF wetu.

Andiko langu hili linawakilisha mimi na yeyote anayekupenda. Hata Nyerere alipoangaza kustaafu mwaka 1980 watu wakamkatalia ikabidi aende hadi mwak 1985.

Hata mtangulizi wako Jenerali Davis Mwamunyange alipofikisha miaka fulani akataka kustaafu Rais Magufuli akakataa akasema asubiri na hadi ukapita mwaka mmoja.

Ombi kwa Rais Samia, kata katakata kustaafu kwa Jenerali Venance Mabeyo mwaka huu. Mwache aendelee kuwa Mkuu wa Majeshi ikibidi hadi baada ya 2025.

Wenu Mwanajamii
Unampenda kama Mabeyo au unapenda huadirifu wa kazi yake? Maana kila paragrafu ninaona nakupenda au tunakupenda nyingi sana
 
Back
Top Bottom