Rais Samia aungwa mkono kuachana na vizuizi vya biashara mipakani

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Baadhi ya Mawaziri wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameunga mkono na kujipanga kutekeleza ushauri wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuachana na mifumo ya kuzuia bidhaa na biashara mipakani.

Wakati wa ufunguzi wa Mutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi za EAC, Rais Samia alishauri EAC kuachana na mfumo wa kuzuia bidhaa katika vituo vya pamoja vya mpakani kwa sababu unachelewesha maendeleo kwa kujikita katika kuzuia bidhaa zaidi badala ya kupitisha bidhaa kwa haraka.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo aliwataka watendaji wote wa serikali katika vituo vya pamoja mpakani kufanya kazi kwa weledi ili kutekeleza ushauri wa Rais Samia.

Jafo alisema hayo mkoani Arusha pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari.

Aidha, Dk Jafo alisema kwa kufanya hivyo kutawawezesha wawekezaji kupata na kutumia fursa ya. kuja kuwekeza nchini na kuiwezesha Tanzania kupata mafanikio katika sekta ya uwekezaji kwa sababu kutakuwa na mazingira rafiki yanayokubali uwekezaji.

Alisema mawaziri wa nchi wanachama wa EAC wamepata fursa ya kukaa na kujadili athari za mabadi-liko ya tabianchi, kuangalia mifumo ya chakula nchini pamoja na kuafikiana kuelekea Mkutano wa Mazingira Duniani wa COP 28 utakaofanyika mjini Dubai, Falme za Kiarabu.

Alisema malengo ya mifumo hiyo ni kumwezesha mwekezaji anapokuja aweze kupata huduma zake zote katika eneo moja kama vile Baraza la Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wengine.
 
Back
Top Bottom