Rais Samia asilalamike Mchawi anaye Kabatini, DP WORLD!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Rais wa JMT,Mh Samia! Alisema ameamua kukaa kimya kuhusu mkataba wenye utata wa Bandari na DP-WORLD.kulingana na tamko lake kwa umma wa Watanzania akiwa kanisani huko Arusha.

Ukweli ni kwamba ukimya wake unamchosha zaidi kuliko ambapo angeongea na kuiweka huru nafsi yake.
Matamshi na kauli zake kwenye hotuba kadhaa anazoendelea kuzitoa,zinaonyesha kifua kilichojaa na kinachotafuta pa kupumulia bila mafanikio. Ni kama vile anatembea na shinikizo kubwa kichwani huku asijuwe la kufanya.

Vema kama kuna kundi au wahafidhina ndani ya chama chako.Ifike mahali sasa achaguwe upande wa kufanya nao kazi.

Baina ya Wahafidhina wa kichama au wananchi na wapiga kura wa nchi hii.

Badala ya kuendelea kujichosha kila uchao kwa jambo ambalo mpishi wake ni yeye mwenyewe.

UKWELI...Ni kwamba hali ilikuwa ya kawaida kabisa kabla ya ile ziara ya Dubai. Hali ilikuwa shwari kabisa kabla ya ujio wa DP-WORLD nchini na kuanza mikakati ya kuchukuwa tunu zetu za taifa kwa mkataba wa kinyonyaji.
Huu ndio ukweli...Mama utaongea sana, atalalamika sana,lakini suluhisho ni pale atakapoongea na kutoa tamko la kuiondoa DP-WORLD kwenye makabati ya ofisini kwake.

Hapo ndipo ataweza kueleweka kwa Watanzania.

Haya mengine ni kama kurusha mchanga hewani halafu usitegemee kuchafuka usoni.

Alamsikhi!

JamiiForums590940298_remastered.jpg
 
Back
Top Bottom