Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea. Kumbukumbu zinaonyesha Zuhuru atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhfa huu wa kuisemea taasisi kubwa zaidi nchini kimamlaka.

Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba pekee na pengine ndio anaweza kuwa mtu aliyehudumu muda mfupi zaidi katika nafasi hiyo.

Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua
===

Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia akihudumu kwenye shirika hilo kwa miaka 14. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.

Mwaka jana Zuhura aliandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor, mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura katika utumishi wake amewahoji viongozi wa Afrika kama vile Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kama sehemu ya taarifa kuhusu biashara haramu ya wanyama pori pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Mahojiano aliyoyafanya na mgombea urais wa upinzani, Edward Lowassa mwaka 2015 yalizua gumzo katika vyombo vya habari nchini.

Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Zuhura Yunus Ikulu.jpg
 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
 
Mwaka wa waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afute kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Hapa ndugu unakosea sana...mbona hao waislam wakati wa Magufuli akifanya teuzi walikuwa hawasemi kuwa mwaka wa wakristo huu! Usitake niamini "the lights are on,but nobody is home!
 
Back
Top Bottom