seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Rais Magufuli alirithi nchi yenye mzunguko wa pesa imara na Ukuaji ulioimarika toka kwa Jakaya Kikwete, Uchumi wa Jakaya Kikwete wa kuajiri maelfu ya watu kila mwaka, na kulipa malimbikizo, Kuongeza mishahara, Kulipa wastaafu kwa wakati, Biashara na wawekezaji kushamiri. Ilituchukua zaidi ya miaka ishirini kufika uchumi wa Jakaya Kikwete.
Faida aliyoipata Jakaya Kikwete hakuvuruga miundo mbinu na matajiri ambao Rais Mkapa aliwajenga ambao ndio wazalishaji wakubwa Nchini bali aliboresha na Kutengeneza mazingira bora zaidi ya kuajiri na kulipa kodi.
Rais Magufuli aliamua Yeye kuvuruga na kufilisi nchi, Hakuishia kuvuruga akaamua na kujaza wasukuma ili waongee kisukuma kwenye sekta muhimu, Bora ingekuwa wasukuma smart wenye ABC za uchumi bali aliwajaza chawa wa kusifu, kuimba na Wengine kama kangi Lugola na Kabudi wakaamua kukufuru kabisa kuwa Rais Magufuli Yeye ni Alfa na Omega.
Rais Samia amepokea nchi ambayo haina uwezo wa kujenga miradi ya SGR na Bwawa la umeme la Nyerere.
Magufuli alikopa pesa za miradi ya SGR na Bwawa la Nyerere kwa pesa ambayo hata nusu ya miradi haiwezi kukamilika, Wakati watu wanahoji kuhusu gharama za mikopo hii na itakuaje baadae waliitwa hao watu sio wazalendo na Wanatumika na Mabeberu, Alipoulizwa Bwawa la zaidi ya Trilioni tano pesa za kumalizia zitatoka wapi alijibu pesa za ndani na nchi ni tajiri huku akishindwa kulipa wastaafu na malimbikizo.
Nani yupo tayari tukakope pesa zingine matrilioni ya pesa kumalizia Bwawa la umeme ambalo maji yake hayana uhakika na mabadiliko ya tabia nchi tayari yanaonekana kwa mkoa wa Dar es Salaam kuwa na baridi ya kutosha na watu kuvaa makoti asubuhi na jioni kama tupo Iringa au Mbeya.
Chawa wakuu walikuwa hawajasoma uchumi wala hawajui maana ya Demand and Supply, Chawa kama Bashiru Ally na Humprey Polepole hawakuwa na ABC za uchumi au mambo yanayohusu mikopo lakini hawa ndio waliaminiwa kama wa shauri wa kujenga SGR.
Rais Magufuli baada ya kuona uchumi ni imara na wawekezaji wanaiamini Tanzania akaanza kuvuruga mifumo ya demokrasia na uwekezaji.
Rais Magufuli alifilisi viwanda na kufilisi wamiliki wa hivyo viwanda walioajiri watu wengi kwa ahadi yake Wataishi kama mashetani.
Ni kweli wazalishaji wakubwa kwenye uchumi wetu waliishi kama mashetani wakati wa Magufuli, Kodi inaongezeka kutokana na uzalishaji, Sasa kama miaka mitano unatumia kuua uzalishaji wa nchi baadae ukimaliza muda wako au ukaondoka kama alivyo Ondoka tunapata wapi kodi.
Leo ameacha nchi yenye madeni kila kona kuanzia madeni ya ndani kwa wastaafu wa PSSf na NSSF, Wazee wastaafu walilimia meno awamu ya tano.
Wafanyakazi waliishia pia kama mashetani kwa kuamua kutolipa malimbikizo yao baada ya kuona uchumi unaporomoka na Yeye ndie Chanzo akabaki anaimba Tazara Interchange na Kijazi Interchange wakati hayo ni madaraja ya kawaida ambayo hakuifuata ramani halisi ya ujenzi kama ilivyotakiwa.
IMF na World Bank waliionya awamu ya tano kuhusu Ukuaji wa uchumi, Lakini Rais aliyekuwepo kushirikiana na ofisi za Takwimu hapa Tanzania waligoma kuhusu Ukuaji wake wakaja na data zao feki kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 kuelekea 8%, Takwimu za IMF na Bank ya dunia zilionyesha uchumi wetu umeporomoka na kufika asilimia 4%.
Baadae awamu ya tano kupitia Spika Ndugai wakatunga sheria bungeni kudhibiti utoaji wa Takwimu ili kuwafunga mdomo wachambuzi kama Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe alimuonya Rais Magufuli na hata kumuandikia barua kuhusu Madhara ya anachokifanya kwenye uchumi wetu kuwa itachukua miaka zaidi ya kumi tena kujenga Uchumi aliouacha Jakaya Kikwete.
Tutapata wapi pesa za kuendesha nchi tena, Ni miaka mingapi itatuchukua tena kurudisha uchumi aliouacha Jakaya Kikwete wa asilimia 6.5%-7.5%
Rais Samia ana mapungufu yake lakini suala la kutuweka wazi anatuweka wazi kila kitu kinachoendelea, Suala la ushauri, Rais Samia anapokea ushauri na amewaacha watanzania waongee wanavyotaka.
Tunamlalamikia Mama Tozo lakini ukweli watu waliovuruga nchi hii kwa Mamlaka waliyopewa ni kiongozi wa awamu ya Tano yaani Rais.
Kwa principal za uchumi mkubwa itatuchukua miaka zaidi ya kumi tena nchi kukaa sawa na hata Rais Samia atamaliza muda wake uchumi wa Kikwete hatutaufikia kabisa.
Rais Samia anahangaika na nchi ambayo uzalishaji umeshuka, Uwezo wetu wa kuuza nje umeshuka, Rais Samia atakusanya wapi kodi wakati uzalishaji ndani ya nchi umeshuka?
Hussein Bashe anajitahidi kumsaidia Rais Samia uzalishaji ukue kwa kuja na mbinu mbalimbali lakini Kumbuka uchumi ulivurugwa na tukarudi hatua zaidi ya miaka kumi nyuma.
Rais Samia na Hussein Bashe watapambana kwenye kuboost uzalishaji lakini wataondoka bado uchumi wetu hautafika asilimia alizoziacha Jakaya Kikwete.
Katiba ni muhimu sana ili kudhibiti watawala wanaoturudisha nyuma.