Rais Samia amepoteza ushawishi kwa wananchi

Hayo ni mawazo yenu Wana chadema
Mama ana wafuasi kibao na tumeridhika na mambo anayoyafanya
kwanza hatuna uchovu wa kisiasa kwani Mwendazake ameshaondoka na tumegundua tulipigwa sana akiwemo Gwajima na Makonda
Pia Mama ni mvumilivu sana kuna ka kitu kanaitwa mfumo dume kanamtaka aondoke
Ungesikiliza Bunge leo ndio ungejua Mama anahitajika kwa miaka mingine 9
hata Clouds 360 huko Mbeya wananchi wanamkubali sana
Mahali wanapomkataa kwa asilimia chache ni JF na Chadema,
lkn TLP, ACT wote wameridhika
Tanzania ina bunge au kikundi cha wahujumu uchumi wa taifa?
 
Tuko vyuoni tuliaminishwa Mwinyi hafai, tukapoteza tukafukuzwa vyuoni na vyuoni vikafungwa kwa mwaka mzima, akaja Mkapa tukaambiwa hakufai, akaja Kikwete tukaaminishwa hafai, akaja Magufuli tumeambiwa hakufaa. Na sasa yuko Samia tukaambiwa hivyo hivyo, na wote hawa wana staili tofauti ya Uongozi.
Jee nyinyi mnaona nani anafaa Lissu?, Mbowe? au nani?

Mnacho sahau hawa ni kuwa viongozi hawa wote ni wa Tanzania wenzetu tunaongea nao, tunakunywa não, tuna cheka não na tunasikitika não.

Tuna wafahamu uzuri, Ubaya na upungufu wao. Mnapo tushawishi kuwa wanafaa watu pumbavu pumbavu mnafanya kila mnae ona anafaa tumuangilie kwa jicho la tatu, na tunapogundua hafai hatuwasikilizi tena..

Watanzania tunapata viongozi kutoka miongoni mwetu na uwakilishi wa sisi tulivyo na sio kutoka mbinguni.
Hawawezi kukuelewa kamwe.

Hawa ni watu ambao wanapigania maslahi yao binafsi
 
Lakini pia tuseme tu ukweli. Kuwaongoza Watanzania siyo kazi rahisi kivile. Hata kama tungekupa wewe leo hii uwe rais. Watanzania hawa hawa wangekupiga madongo tu hata kama ungefanya mazuri kiasi gani.

Mimi nadhani kwa viongozi hawa njia ni rahisi tu. Watambue kuwa hawatapendwa na kila mtu hata kama wangefanyeje. Cha muhimu tu wafanye kila wakifanyacho kwa kuzingatia katiba na sheria zilizopo basi. Mengine wawaachie keyboard warriors na watukanaji wa mitandaoni humu.
Huwezi kupendwa na kila mtu lakini ukubalike na asilimia kubwa ya unaowaongoza.

Kama asilimia kubwa haikukubali ujue kuna walakini..!
 
95% wanamkataa. Anatumia ubabe, analeta umaskini kwa raia wake yaan ni mateso mateso.

Kapunguza kwenye tozo kaongeza kwenye mafuta....
 
Lakini pia tuseme tu ukweli. Kuwaongoza Watanzania siyo kazi rahisi kivile. Hata kama tungekupa wewe leo hii uwe rais. Watanzania hawa hawa wangekupiga madongo tu hata kama ungefanya mazuri kiasi gani.

Mimi nadhani kwa viongozi hawa njia ni rahisi tu. Watambue kuwa hawatapendwa na kila mtu hata kama wangefanyeje. Cha muhimu tu wafanye kila wakifanyacho kwa kuzingatia katiba na sheria zilizopo basi. Mengine wawaachie keyboard warriors na watukanaji wa mitandaoni humu.
Yesu alichukiwa na baadhi ya watu, Mtume Muhammad (s.a.w) alichukiwa na baadhi ya watu sembuse Mama Samia??

Mama amepikwa akapikika, anajua kwamba hata afanye nini hawezi pendwa na kila mtu.

Kwahiyo yeye anapiga kazi tu.
 
Bora jiwe alikuwa muwazi , alifanya mchana kweupe na ujinga wake aliumbuka na balozi zilimtenga lakini sio huyu anae lisha watu maneno na kujifanya yupo na wananchi, eti tumekubali tozo ,madini yanatoka yaliyo zuiwaa mpaka waziri mkuu kulitolea maelzo kamwe tusingejua,analisha wananchi maneno bado wanao mpinga anawalisha maneno ambayo sio yao Maajab zaidi toka niijue hii nchi

sikuwahi kutegemea ubalozi wa nchi kama denmark ufunge ubalozi wake 2024,
sijawahi fikilia mtu afanye tukio la mauaji karibu na ubalozi ,
sijawahi fikilia kama kiongozi mkuu anaweza pewa kesi ya ugaidi mchana kweupe,
hii roho ya huyu mama sio ya kawaida na anachukulia mambo kirahisi sana.

halafu rais hapaswi kutamka maneno kama ugaidi mbele za watu hajui kama rais huamsha mambo ambyo hayapo kwa kauli zake.

natoa salamu kwa kimbuga job na serikali ya mama samia kauli ya job juu ya igp haina usalama na afya kwa serikali yetu kiburi chake cha uhakika wa kutofungwa sio upelekee amkebehi igp hii ni hatari.

naona mpasuko mkubwa, usaliti na utii kupungua kati yao ambao hujawahi kutokea ndani ya hii nchi na hili nalithibitisha kwa kauli za slowslow baada ya kusema tusitishane rais kasema hili jambo ni hiari.

Mungu ailinde hii nchi.
Leo ndio mnajua Bora jiwe alikuwa muwazi????

Mta....mba cheche safari hii.

Si mnajifanya hamuelewi nyie
 
Mm sijawahi hata kukaaa kusikiliza hotuba zake sijui hata kwa nn maana naishiaga kushikwa hasira tu.Mzee wa chato alinifanya mpaka niipende tbc taifa maana ulikua ukisikia mwamba anahutubia unajisikia raha na kupata matumaini kua nchi inakiongozi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mama ameshapoteza usikivu amekuwa kama mtangulizi wake.
Hahaahaahahahahahahaah.

Alipoamua kuwa msikivu na kuongoza kistaarabu mlimtangazia mtamnyoa.

Sasa vilio kila kona. Ni kwa kwaaa kwaaa kwaaa. Ni vilio vya mbwa koko tu huko
 
Tafiti gani ni "pang'ang'a" tu 🤣🤣
Wakimaliza kufanya tafiti itakuwa ni July 2025. Tume ya uchaguzi itatoa masharti na miongozo na wao kwa kuwa kila wakiitwa na tume hawataki basi watakosea masharti na miongozo yote.

Kitakachofuata ni wao mapambano na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. 25th October 2025 wakipasuliwa tutakayoyaskia ni vilio

😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄
 
🤣🤣

Mh.SSH yeye anawaza yafuatayo-

-Aendelee kutoa ajira zaidi ya zile 8000 za TAMISEMI+ WIZARA YA AFYA(ikumbukwe ilipita miaka mingi mno hazipo)

-Atimize ahadi yake ya kuwaongeza mishahara watumishi wa umma mwaka ujao wa fedha

-Amalize miradi ya kimkakati(BWAWA LA UMEME MWALIMU NYERERE ,SGR ,MELI MPYA ,UPANUZI WA BANDARI n.k

-Ainue kilimo kwa kujenga barabara mpaka mashambani.....

-Aongeze VITUO VYA AFYA maeneo yasiyofikika kirahisi kwa ajili ya UZAZI SALAMA

Mh.SSH hafanyi TAFITI KOKO....ANATENDA......
Mama ana mikakati mizito.

Nimepata kuhudhuria tafrija flani huku Mama alivyokuja juzi. Kwa kweli Mama yuko vizuri mno!

ANAUPIGA MWINGIIIIIIIIIIIII

Watakaa tu kudaadeki
 
Tangu julai nilipoteza matumaini maana lile punguzo la Payee ya asilimia 1 kuwa sh 2500/= liliniletea maumivu makali maana ahadi yake aliyoitoa mei mosi ikawa ni uwongo dhahiri
 
Nijuavyo hakuna wakati wowote Tanzania hii kulikuwa na hali nzuri kiasi cha kumridhisha kila mtu lakini wakati wa Magufuli ilikuwa watu wakilalamika waliishia kubezwa na kutukanwa tu.
 
Nijuavyo hakuna wakati wowote Tanzania hii kulikuwa na hali nzuri kiasi cha kumridhisha kila mtu lakini wakati wa Magufuli ilikuwa watu wakilalamika waliishia kubezwa na kutukanwa tu.
Zamani mimi nikiwa natembea barabarani,nikiona noah nyeusi imenipita na kusimama mbele nageuza njia haraka sana,,nikiona imepark mbele hiyo njia sipiti ng'o
 
Nakubaliana na wewe kiukweli mama Samia ni kana kwamba Kuna watu kawaachia nchi waongoze and kwakweli atapata tabu Sana 2025, alianza vzuri ila mvuto wake kwa Sasa umeporomoka kafanya tofaut namatarajio ya wengi
 
Hayo ni mawazo yenu Wana chadema
Mama ana wafuasi kibao na tumeridhika na mambo anayoyafanya
kwanza hatuna uchovu wa kisiasa kwani Mwendazake ameshaondoka na tumegundua tulipigwa sana akiwemo Gwajima na Makonda
Pia Mama ni mvumilivu sana kuna ka kitu kanaitwa mfumo dume kanamtaka aondoke
Ungesikiliza Bunge leo ndio ungejua Mama anahitajika kwa miaka mingine 9
hata Clouds 360 huko Mbeya wananchi wanamkubali sana
Mahali wanapomkataa kwa asilimia chache ni JF na Chadema,
lkn TLP, ACT wote wameridhika
Sio kweli mimi nimshabiki wa mama na alipoingia nilitegemea makubwa na mabadiliko makubwa ila naona Kuna watu wanampoteza mama wanataka aendeshe nchi kama magufuli hii imempunguzia mvuto Sana na sikweli kwamba ni kwa wapinzan pekee, kumbuka siku 100 za kwanza kila pande ilimkubali ila kwa Sasa Sio siri amepoteza mvuto
 
Zamani mimi nikiwa natembea barabarani,nikiona noah nyeusi imenipita na kusimama mbele nageuza njia haraka sana,,nikiona imepark mbele hiyo njia sipiti ng'o
Inatakiwa mtu uwe na amani ya nafsi hata kama huna hela sio kutishana tishana kila wakati,sijasikia muda mrefu viongozi kutia ndani watu hovyo wala mtu kucharazwa bakora hadharani.
 
sasa hivi tunakatwa tozo baada ya hapo tunakatiwa umeme. a collapsing corrupt regime.
 
Hayo ni mawazo yenu Wana chadema
Mama ana wafuasi kibao na tumeridhika na mambo anayoyafanya
kwanza hatuna uchovu wa kisiasa kwani Mwendazake ameshaondoka na tumegundua tulipigwa sana akiwemo Gwajima na Makonda
Pia Mama ni mvumilivu sana kuna ka kitu kanaitwa mfumo dume kanamtaka aondoke
Ungesikiliza Bunge leo ndio ungejua Mama anahitajika kwa miaka mingine 9
hata Clouds 360 huko Mbeya wananchi wanamkubali sana
Mahali wanapomkataa kwa asilimia chache ni JF na Chadema,
lkn TLP, ACT wote wameridhika
Umeambiwa Fanya utafiti

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
When she firstly came into power, people were optimistic that maybe the country could return to sanity.

Unfortunately, they didn't know that the newly introduced head of state had inherited the same repressive and utterly ruthless machinery with which her predecessor used to bulldoze the nation with relish.

Now that that has become known to the majority of her subjects is the main reason why her approval rating has quickly plummeted and will definitely continue to fall alongside the party she leads.

For a considerable period of time now, the ruling party has been heavily relying on the brutal state security apparatus to survive in power against the people's will backed by the existing authoritarian constitution.
 
Back
Top Bottom