Rais Samia afanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kama ifuatavvo:
  1. Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.
  2. Amemteua Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Balozi Mapuri ameteuliwa kuwa Mjumbe kwa kipindi cha pili.
  3. Amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza tarehe 01 Julai, 2023.
  1. Amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA). Prof. Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili.
  2. Amemteua Bw. Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 25 Juni, 2023.

IMG_7781.jpeg
 
Halafu utegemee hao walioteuliwa na Samia kwenye hiyo tume ya uchaguzi waje watende haki kwenye uchaguzi mkuu ujao ambao yeye [Samia] atakuwa anagombea urais!

Uwendawazimu mtupu.

Sijui ni lini tu tataachana na huu upumbavu???

Wananchi kwa wingi wanatakiwa kuzigomea chaguzi zetu mpaka pale itapopatikana tume huru ya uchaguzi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kama ifuatavvo:
  1. Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.
  2. Amemteua Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Balozi Mapuri ameteuliwa kuwa Mjumbe kwa kipindi cha pili.
  3. Amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza tarehe 01 Julai, 2023.
  1. Amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA). Prof. Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili.
  2. Amemteua Bw. Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 25 Juni, 2023.

View attachment 2673170
Huyu Mapuri mzanzibar bado yupo?Nilijua alishakufa.Prof Mshoro ndani. Haya mama zamu ya wazanzibari hii.Vamos
 
Udini udini udini udini. Huyu mama tutamoa zawadi yake 2025.

Maaskofu shtukeni mmependishwa mtumbwi sio. Anawapiga huku anawapuliza. Huyu mama ni mdini mno
huna haja ya kusema udini, mimi ni mkristu nafahamu kuwa wakristu wapo wengi wameshikilia nafasi mbalimbali serikalini kuliko waislamu lakini baadhi ya wakristu wenzangu mna nongwa sana.
narudia kusema kuwa nchi hii ni ya watu wote waislam na wakristu na wasio na dini, wote wanayo haki ya kuitumikia hii nchi, tusijifanya kuwa sisi wakristu ndio tunahaki zaidi ya wengine, tunakosea sana ndugu zangu.
nakemea tabia hii tuiache.
 
Back
Top Bottom